Duu kuna kaka mmoja yeye ana mkewe walikuwa na watoto 3 wakike tupu. Sasa akaamua kwenda kuzaa nje kutafuta mtoto wa kiume alifanikiwa na kwenda kumtambulisha kwa ndugu kama wote mkewe aligombananae ila wakamwambia tuh huyu ni mtoto wake hata ukachukia haisaidii.
akakukubali.
Ndugu wa mwanaume wakamwambia kaka yao huyo ni mtoto wako mchukue ukae nae azoeane na wenzie. Yule kaka akamchukua akawa anaishi nae mkewe akanyamaza. Mawifi wakawa wanamsema tuu dada yule kuwa hamtaki mtoto wa mume wake.
Sasa mkewe nae akaamua kuzaa nje , yeye na mkewe ni weupe kwa hio watoto wote ni weupe mpaka wa mume wa nje.
Ila mkewe akachepuka na mwanaume mweusi , mtoto kazaliwa mweusi , mume eee.
Mkewe wake akamwambia huyu mtoto sio wako anaBaba yake.
Kwenye cheti cha kuzaliwa mama akaandika Baba yake halisi na sio mume wake. Yule kaka alilalamika sana kwao.
ILA baba yale alimwambia kuwa Hata wewe ulifanya hivyo hivyo kuwa mpole tuu najua unaumia kuwa mpole tuu.
Dada zake walimtukuna sana yule dada. Ndoa ya kikristo. Wakawashauri tuu tulieni mlee watoto hao. Sasa hivi wote ni wakubwa kipindi cha likizo wa nje wote wanaenda kwa wazazi wao kuwasalimia likizo ikiisha wanarudi. Familia inawatoto 5 sasa.