Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mabadiliko ya jamii hayaji yenyewe. Mabadiliko yanaletwa kiongozi mwenye maono na aliyeunda timu yenye maono. Ukiwa na watoto wazembe ni jukumu lako kama mzazi kuhakikisha unafanya kila njia ili waondokane na hiyo hali. Nakubaliana na wewe kuwa tuna jamii iliyooza na tunatakiwa kubadilika. Tumefikaje hapa tulipo? Ni CCM imetufikisha. Tutatokaje? Inabidi tuache kurudia kufanya kitu kile kile na kwa namna ile ile huku tukitegemea matokeo tofauti. Tuanze na kufumua mfumo wetu wa kupata viongozi na namna tunavyoongoza ASAP! Yes, ASP, na siyo ngonjera za ''subirini tujenge uchumi kwanza''.Kazi ya kiongozi mkubwa kama Rais sio kuchukua hatua kwa mtu mmoja mmoja ispokuwa kwa wateule wake tu wa moja kwa moja. Kazi ya Rais ni kutoa miongozo, maelekezo na muelekeo wa taifa kwenye mambo makubwa makubwa.
Then kuna mifumo ya kitaasisi ambayo inatakiwa ifanikishe masuala ya kiutendaji kama hayo ya kuchukuliana hatua na.k.
Kwa bahati mbaya kwenye jamii yetu tuna watu wachache wa maana na wengi wa ovyo. Hivyo kutoka kwenye sample hiyo, ndio tunapata wawakilishi wa maeneo mbalimbali. Na tunachoona ni matokeo ya kuwa na jamii ya aina hiyo. Hivyo pamoja na kuwa na kiongozi mzuri, mabadiliko ya kijamii yanayolenga kila mtu kuwa na utamaduni wa kutekeleza wajibu wake ni muhimu kuliko kitu kingine chochote.
Wema wake unaupima na nini? Kuweka tozo za kumliza mwananchi huku akiwa kimya huko ama? Dikteta ni yupi, anayekuonesha wazi kuwa hapa kakuliza ama? Wote madikteta tu njia ndo tofauti za kuliza watu. 😁Majinga sana haya matahila, wao kila Rais hafai hata akiwa mwema kama Samia
Sasa mbadala wa CCM uko wapi? Maana pamoja na yote hayo, bado CCM ndio yenye uafadhali mkubwa sana, ukiwalinganisha na vyama vingine ni mbingu na nchi.Mabadiliko ya jamii hayaji yenyewe. Mabadiliko yanaletwa kiongozi mwenye maono na aliyeunda timu yenye maono. Ukiwa na watoto wazembe ni jukumu lako kama mzazi kuhakikisha unafanya kila njia ili waondokane na hiyo hali. Nakubaliana na wewe kuwa tuna jamii iliyooza na tunatakiwa kubadilika. Tumefikaje hapa tulipo? Ni CCM imetufikisha. Tutatokaje? Inabidi tuache kurudia kufanya kitu kile kile na kwa namna ile ile huku tukitegemea matokeo tofauti. Tuanze na kufumua mfumo wetu wa kupata viongozi na namna tunavyoongoza ASAP! Yes, ASP, na siyo ngonjera za ''subirini tujenge uchumi kwanza''.
Na hicho ''kiasi fulani'' ni bora kuliko kuendelea kubaki kwenye hii hali. Ni muhimu sana tuwe na mfumo mzuri na makini wa kupata viongozi wazuri haraka sana sana. Ukiwa na mahindi na ukigundua mengi ni mabovu, bila shaka hatua ya kwanza ni kuwa makini sana kwenye kuyachambua. Jamii haiwezi kuamua kustaarabika yenyewe kila mazingira ya kuleta mabadiliko kuwekwa. Ukiwa na jamii yenye vibaka wengi, huwezi kupiga kelele tu kwa kusema badilikeni bila kuchukuwa hatua.Itasaidia kiasi fulani lakini sio sana. Jamii yenye wahuni na wasanii wengi hata itokee malaika ashuke na katiba toka mbinguni, haisaidii sana.
Kinachiweza kusaidia sana (pamoja au bila katiba mpya) ni jamii kuamua kustaarabika. Ustaarabu hujenga imani, imani huleta kuaminiana, kuaminiana huleta maendeleo ya kweli.
Wewe ukifungua tu MPesa, ukaweka mtu, uwezekano wa huyo mtu kukuibia na kutoroka in most cases ni zaidi ya 80℅ sasa hapo Rais au katiba vifanyeje kwa mfano? Au watu wataendelea kukosa ajira tu!
Umeandika ujinga tuu..Mama atapumzika 2035 maana ndio kwanza awamu yake itaanza 2025.Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.
Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.
Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.
Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.
Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.
wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%
Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.
Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?
Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.
Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?
Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?
Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?
Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?
Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.
Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Umeongea ukweli,hao fala waambie walete Takwimu hapa za Mama hadi sasa na za Marasi wao waliokaa miaka ya kutosha..Kelele nyingi kwa sababu hizi
1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Again tunarudi kule kule kwenye ushabiki wa vyama vya siasa. Kama unaona hakuna mbadala wa CCM, basi hata hiyo hiyo CCM tuiundie mfumo madhubuti ili wapatikane viongozi wazuri na siyo kama sasa wamejaa wapiga dili na waropokaji. Tufumue mfumo wote tuunde upya ili hata kama CCM ndiyo itaendelea kutawala basi viongozi wake wapitie kwenuye chekeche, ili kupata viongozi bora na siyo rais kuteua watu kwa fadhila na kuwapelekea watu.Sasa mbadala wa CCM uko wapi? Maana pamoja na yote hayo, bado CCM ndio yenye uafadhali mkubwa sana, ukiwalinganisha na vyama vingine ni mbingu na nchi.
Walewale. Kwa magufuli kelele hazikupigwa? Alikuwa mzanzibar? Muislamu? Au hakuwa na jinsia? Kelele hujitokeza kuongelea udhaifu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wote. Usitegemee kwenye madhaifu watu wakae kimya kwa kuhofia kuambiwa hoja za kisengerema kama hizo ulizotoa. Hatutafutiani huruma hapaKelele nyingi kwa sababu hizi
1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Unaweza kuthibitisha?Kelele nyingi kwa sababu hizi
1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Acha kupuuza mamlaka alikuwa nayo Rais. Usifanye aonekane Sanamu.Mkuu technically iko hivi;
1. Ni kweli mama ni kiongozi muadilifu sana na mpenda haki. Aidha, ni mara chache sana kusikia kiongozi toka zbar asiye mwadilifu.
2. Kuwa na kiongozi mmoja bora peke yake hakutoshi kufanya mambo yaende sawa. Kutegemea mtu mmoja pekee ili kila kitu kiende sawa, ni sawa na kutegemea injini zuri kwenye gari yenye tairi zenye pancha.
3. Kuhusu kuchukulia watu hatua; unapaswa kuelewa kuwa nchi ina sheria lakini pia kuna actors tofauti tofauti waliopewa majukumu tofauti tofauti na mengine ya kitaalamu. Ni kweli kuna maeneo yenye matatizo ila kufikiri kama Rais anaweza kuingilia kila kitu na kuface mtu mmoja mmoja na kumchukulia hatua sio sahihi. Kiongozi mkubwa kazi yake ni kutoa maelekezo sahihi.
4. Kuhusu mfumuko wa bei; kabla ya kupendekeza solution kwenye jambo lolote, ni muhimu sana kuelewa chanzo sahihi cha tatizo.
Mwisho, ili kila kitu kiwe sawa, ni muhimu kila mtu atekeleze wajibu wake kulingana na uwezo wake na sehemu alipo. Tukiwa na watu wengi wanaofanya hivyo, ndio tutaweza kupiga hatua kwa haraka.
Vinginevyo ni sawa na kuwa na kocha mzuri na wachezaji hawana mbio, tutabakia kulaumu makocha tu kumbe ishu sio kocha bali wachezaji.
Sensa ni ujinga kama imetumia pesa nyingi bila sababu.Sensa sio ujinga na haiwezi kuwa ujinga, jisomee faida zake ujionee.
Inflation now is a global issue , kusema samia apumzike kwa sababu ya Inflation ni sawa na kusema Putin, Biden, Xi jiping na Marais wote duniani wasigombee tena!Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.
Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.
Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.
Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.
Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.
wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%
Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.
Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?
Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.
Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?
Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?
Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?
Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?
Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.
Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Jisemee wewe siyo uweke sisi wananchi, yeye siyo mwananchi? Ulipewa mamlaka hayo na nani uwe msemaji wa wananchi?Nenda ukapumzike wewe mwenyewe maana sisi wananchi bado tunamhitaji Sana mh Rais wetu mpendwa kututumikia maana ameonyesha uwezo mkubwa Sana katika kutuongoza na utatuzi wa kero zinazotukabili
Swala la mfumuko wa Bei mh Rais amelikabili kwa kadiri ilivyowezekana, kwanza ametambua kuwa mafuta ndio injini ya uchumi, hivyo kupanda kwake lazima kuathiri secta zote, hapa mh Rais wetu akaamua kutoa Ruzuku ya shilingi billioni Mia moja kila mwezi ili kupunguza makali ya Bei na kumsaidia mwananchi mnyonge asiathiriwe Zaid kiuchumi kwa Bei za vitu
Kuhusu kuchukua hatua Napo umepotosha maana mh Rais wetu mpendwa amekuwa Hana mzaha Wala Subira kwa mtu au kiongozi yoyote atakaye gusa pesa za umma kwa maslahi yake binafsi, hapa haangalii sura ya mtu Wala kumvumilia mtu,
Kuhusu sensa bado zoezi linaendelea vizuri naamini pia serikali itaangalia Cha kufanya iwapo kuna baadhi ya watu watakuwa hawajahesabiwa mpaka kesho
Unanishangaza unasema sensa imetumia gharama kubwa halafu hapo hapo unataka katiba mpya uanze mchakato wake, kwani mchakato wa katiba siyo gharama? Au hela utatoa wewe au utafanya wewe?
Yaan apumzike halafu atoke wa imani hileee,ambayo wakiongoza wao nchi mambo yanakuwa magumu zaidi, ns matukio ya hovyo yanashika kasi.
Nyie watanzania hamjulikani mnataka nini, akipatikana kiongozi muungwana bado mnalialia tu, dawa ndio hiyohiyo, mkamuliwe hadi akili ziwakae sawa ,maana hamjielewi kabisa
Mpuuzi kazini.Umeandika ujinga tuu..Mama atapumzika 2035 maana ndio kwanza awamu yake itaanza 2025.
Hilo la kuwajengea uwezo watu ndani ya vyama ili wawe viongozi bora nakubaliana nawe kabisa. Suala hili tulishalizungumzia sana kwamba; kwa mtu kujiunga na chama, hilo pekee halimsababishi awe kiongozi bora , bali ni lazima pawe na namna ya kumjengea uwezo kwa nguvu kubwa ili akipata nafasi ya kuwa kiongozi awe kiongozi wa maana.Again tunarudi kule kule kwenye ushabiki wa vyama vya siasa. Kama unaona hakuna mbadala wa CCM, basi hata hiyo hiyo CCM tuiundie mfumo madhubuti ili wapatikane viongozi wazuri na siyo kama sasa wamejaa wapiga dili na waropokaji. Tufumue mfumo wote tuunde upya ili hata kama CCM ndiyo itaendelea kutawala basi viongozi wake wapitie kwenuye chekeche, ili kupata viongozi bora na siyo rais kuteua watu kwa fadhila na kuwapelekea watu.
You are right. Hii itahakikisha kuwa nchi haiwi tegemezi kwa aina ya rais tuliyenaye.Kimsingi hatuhitaji kiongozi muungwana, bali tunahitaji katiba bora. Hayo mambo ya uungwana au ukatali yabanwe na katiba. Tunakwama sana tunapoendelea kukumbatia katiba ambayo inampa rais maamuzi yote ya nchi.