Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Hamna jema, Jiwe mkali sana, SSH mpole sana. Amin Amin nakwambia atokaye ni Bora kuliko ajaye siku zote so twenda na mama Hadi 2030.
 
Mabadiliko ya jamii hayaji yenyewe. Mabadiliko yanaletwa kiongozi mwenye maono na aliyeunda timu yenye maono. Ukiwa na watoto wazembe ni jukumu lako kama mzazi kuhakikisha unafanya kila njia ili waondokane na hiyo hali. Nakubaliana na wewe kuwa tuna jamii iliyooza na tunatakiwa kubadilika. Tumefikaje hapa tulipo? Ni CCM imetufikisha. Tutatokaje? Inabidi tuache kurudia kufanya kitu kile kile na kwa namna ile ile huku tukitegemea matokeo tofauti. Tuanze na kufumua mfumo wetu wa kupata viongozi na namna tunavyoongoza ASAP! Yes, ASP, na siyo ngonjera za ''subirini tujenge uchumi kwanza''.
 
Majinga sana haya matahila, wao kila Rais hafai hata akiwa mwema kama Samia
Wema wake unaupima na nini? Kuweka tozo za kumliza mwananchi huku akiwa kimya huko ama? Dikteta ni yupi, anayekuonesha wazi kuwa hapa kakuliza ama? Wote madikteta tu njia ndo tofauti za kuliza watu. 😁
 
Sasa mbadala wa CCM uko wapi? Maana pamoja na yote hayo, bado CCM ndio yenye uafadhali mkubwa sana, ukiwalinganisha na vyama vingine ni mbingu na nchi.
 
Na hicho ''kiasi fulani'' ni bora kuliko kuendelea kubaki kwenye hii hali. Ni muhimu sana tuwe na mfumo mzuri na makini wa kupata viongozi wazuri haraka sana sana. Ukiwa na mahindi na ukigundua mengi ni mabovu, bila shaka hatua ya kwanza ni kuwa makini sana kwenye kuyachambua. Jamii haiwezi kuamua kustaarabika yenyewe kila mazingira ya kuleta mabadiliko kuwekwa. Ukiwa na jamii yenye vibaka wengi, huwezi kupiga kelele tu kwa kusema badilikeni bila kuchukuwa hatua.
 
Umeandika ujinga tuu..Mama atapumzika 2035 maana ndio kwanza awamu yake itaanza 2025.
 
Kelele nyingi kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Umeongea ukweli,hao fala waambie walete Takwimu hapa za Mama hadi sasa na za Marasi wao waliokaa miaka ya kutosha..

Jitu linaongea upuuzi tuu usio na maane eti kuchukua hatua 😆😆
 
Nenda ukapumzike wewe mwenyewe maana sisi wananchi bado tunamhitaji Sana mh Rais wetu mpendwa kututumikia maana ameonyesha uwezo mkubwa Sana katika kutuongoza na utatuzi wa kero zinazotukabili

Swala la mfumuko wa Bei mh Rais amelikabili kwa kadiri ilivyowezekana, kwanza ametambua kuwa mafuta ndio injini ya uchumi, hivyo kupanda kwake lazima kuathiri secta zote, hapa mh Rais wetu akaamua kutoa Ruzuku ya shilingi billioni Mia moja kila mwezi ili kupunguza makali ya Bei na kumsaidia mwananchi mnyonge asiathiriwe Zaid kiuchumi kwa Bei za vitu

Kuhusu kuchukua hatua Napo umepotosha maana mh Rais wetu mpendwa amekuwa Hana mzaha Wala Subira kwa mtu au kiongozi yoyote atakaye gusa pesa za umma kwa maslahi yake binafsi, hapa haangalii sura ya mtu Wala kumvumilia mtu,

Kuhusu sensa bado zoezi linaendelea vizuri naamini pia serikali itaangalia Cha kufanya iwapo kuna baadhi ya watu watakuwa hawajahesabiwa mpaka kesho

Unanishangaza unasema sensa imetumia gharama kubwa halafu hapo hapo unataka katiba mpya uanze mchakato wake, kwani mchakato wa katiba siyo gharama? Au hela utatoa wewe au utafanya wewe?
 
Sasa mbadala wa CCM uko wapi? Maana pamoja na yote hayo, bado CCM ndio yenye uafadhali mkubwa sana, ukiwalinganisha na vyama vingine ni mbingu na nchi.
Again tunarudi kule kule kwenye ushabiki wa vyama vya siasa. Kama unaona hakuna mbadala wa CCM, basi hata hiyo hiyo CCM tuiundie mfumo madhubuti ili wapatikane viongozi wazuri na siyo kama sasa wamejaa wapiga dili na waropokaji. Tufumue mfumo wote tuunde upya ili hata kama CCM ndiyo itaendelea kutawala basi viongozi wake wapitie kwenuye chekeche, ili kupata viongozi bora na siyo rais kuteua watu kwa fadhila na kuwapelekea watu.
 
Kelele nyingi kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Walewale. Kwa magufuli kelele hazikupigwa? Alikuwa mzanzibar? Muislamu? Au hakuwa na jinsia? Kelele hujitokeza kuongelea udhaifu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wote. Usitegemee kwenye madhaifu watu wakae kimya kwa kuhofia kuambiwa hoja za kisengerema kama hizo ulizotoa. Hatutafutiani huruma hapa
 
Acha kupuuza mamlaka alikuwa nayo Rais. Usifanye aonekane Sanamu.
 
Inflation now is a global issue , kusema samia apumzike kwa sababu ya Inflation ni sawa na kusema Putin, Biden, Xi jiping na Marais wote duniani wasigombee tena!

Huna hoja
 
Jisemee wewe siyo uweke sisi wananchi, yeye siyo mwananchi? Ulipewa mamlaka hayo na nani uwe msemaji wa wananchi?
 

Kimsingi hatuhitaji kiongozi muungwana, bali tunahitaji katiba bora. Hayo mambo ya uungwana au ukatali yabanwe na katiba. Tunakwama sana tunapoendelea kukumbatia katiba ambayo inampa rais maamuzi yote ya nchi.
 
Hilo la kuwajengea uwezo watu ndani ya vyama ili wawe viongozi bora nakubaliana nawe kabisa. Suala hili tulishalizungumzia sana kwamba; kwa mtu kujiunga na chama, hilo pekee halimsababishi awe kiongozi bora , bali ni lazima pawe na namna ya kumjengea uwezo kwa nguvu kubwa ili akipata nafasi ya kuwa kiongozi awe kiongozi wa maana.

Kwa bahati mbaya jambo hii halijawahi kuchukukiwa kwa uzito unnaostahili na chama chochote nchini.
 
Kimsingi hatuhitaji kiongozi muungwana, bali tunahitaji katiba bora. Hayo mambo ya uungwana au ukatali yabanwe na katiba. Tunakwama sana tunapoendelea kukumbatia katiba ambayo inampa rais maamuzi yote ya nchi.
You are right. Hii itahakikisha kuwa nchi haiwi tegemezi kwa aina ya rais tuliyenaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…