USHAURI: Rais Samia suluhisho pekee kwa Bandari Tanzania ni hili

Leo hii Serikali inataka kufanya hivi watu wanaleta mijadala uchwara humu.

Ujinga ni kipaji
 
Ushauri wako ndo unafanyiwa kazi na Serikali sasa ila kuna mijitu inaleta siasa iki mradi waonekane tu wanajua kuongea na kupinga

Nchi hii ujinga ni kipaji
 
Na watanzania tulivyo……tunashabikia viongozi dhaifu tulionao na hata kufikia kutetea kasi ndogo ya maendeleo yetu!
Mbaya zaidi viongozi wakichukua hatua ili twende na kasi inayotakiwa katika maendeleo tunaanza tena kupiga kelele eti nchi inauzwa.

Tanzania ujinga ni kipaji
 
Ushauri murua ulishatolewaga kwa Rais kupitia JF. Na hii ni mwaka jana na Rais ameufanyia kazi.

JF ni kisima.
 
Ushauri murua ulishatolewaga kwa Rais kupitia JF. Na hii ni mwaka jana na Rais ameufanyia kazi.

JF ni kisima.
Ushauri wako ulihusisha kubinafsisha bandari kwa muda usiojulikana na kwa masharti yanayomnufaisha mwekezaji kuliko nchi?
Au unaropoka tu ili kuonesha ushauri wako ni ushauri
 
Tatixo kubwa sio mwekezaji tatizo ni mkataba wa kihuni
 
Ushauri wako ulihusisha kubinafsisha bandari kwa muda usiojulikana na kwa masharti yanayomnufaisha mwekezaji kuliko nchi?
Au unaropoka tu ili kuonesha ushauri wako ni ushauri
Wapi na lini Bandari imebinafsishwa kwa muda usiojulikana?
 
Kila mtu mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na nane atoe at elfu kumi hela itakayo patikana wapewe T.P.A yote hayo yafanywe na mamlaka ya kitanzania kwa watanzania
 
Leo hii Serikali inataka kufanya hivi watu wanaleta mijadala uchwara humu.

Ujinga ni kipaji
Maaskofu wamejitoa mhanga kwamba lolote na liwe, kitu ambacho sio kizuri. Rais hafanyi kitu kwa maamuzi yake binafsi ni ushauri wa wataalam wengi tena wanachokiongea kinawekwa kwenye kitabu kimoja kinachoitwa ilani ya uchaguzi.

Wasidhani kuwa uwekezaji wa DP World ni maamuzi ya jana au juzi au kama inavyosemekana kwamba Dubai ni wajomba zake SSH, haya ni maamuzi ya miaka na miaka yaliyoanza na ujenzi wa SGR kwanza ambayo imekula matrilioni ya pesa mpaka kufika ilipofika muda huu.

SIdhani kama hao waliowashauri maaskofu walifuatilia masuala mazima ya muendelezo wa ilani ya CCM katika kutekeleza sera zake zaidi ya hoja zao kutegemea zile hisia za SSH kutaka kuwaridhisha jamaa zake wa Dubai.

Walichokifanya ni kutaka kutunishiana misuli na mamlaka ya rais kwa kutumia ukongwe wa kanisa kwa kutumia kuungwa mkono kwa hoja zao, wameamua kujilipua lakini maisha yanaendelea siku zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…