Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Yah tupo pamoja mkuu ....japo hapo nyuma kidogo michango yako iliadimika ila ni Jambo jema kukuona tena tu-pamoja.
 
Yah tupo pamoja mkuu ....japo hapo nyuma kidogo michango yako iliadimika ila ni Jambo jema kukuona tena tu-pamoja.
Nashukuru karibu muda wowote hata kama una jambo lako pia unaweza nifuata pm tu, tuko pamoja sana ndugu.
 
wasikulaumu mwaya,

kukaa na mtu usiyempenda is not healthy kwako na huyo mwenzio,

utam miss treat kwa kuwa humpendi,

then utaishia kuwa GUILTY kwa kufanya hivyo,

na yeye kuonyeshwa hapendwi kutamfanya awe angry at herself and guilty to why you dont love her,thinking why...

Kwa kifupi tunakaa kwenye mahusiano sio kwa kuwa tunapendana 100% bali tuna compromise vitu fulani,

Ukiona unasema humpendi,then hivyo vitu vya ku compromise vimekua vingi mno, na mambo hayako sawa

Solution ni kuondoka kwenye uhusiano wa hivyo,

kama unaweza ongea nae kwa upole au tafuta mtu anayemuheshimu aongee nae,

unaweza kushangaa miezi mitatu baada ya kuachana,yuko happy labda kapata somebody else na ana amani akashukuru uhusiano wenu uliisha...
 
Rebeca umepotea, nimekumiss sana rafiki,
 
Umeongea sana point mzee wangu
 
Aisee mtu huna malengo nae halafu unamwambia aje muishi wote?!
Na ni dhahiri kwenye hii insha yako hata mwanao humpendi pia....sasa subiri ulimwengu ukunyooshe perpendicularly!
 
Kwanza huenda mwanamke ni mshirikina,ukizubaa yatakukuta Kama Mimi watoto watatu na sijui nimefikaje hapa nilipo,alivyokuja rafiki yangu anaenijua deep down akasema mbona umepoteza dira,umelogwa mpaka umewekwa kwenye chipa na Sasa inafanyika mipango ya kukua kabisa,wallah ndo akili ikaanza kuzinduka nakumbuka jinsi nikivyopoteza pesa kukaribu kuweka mambo sawa,lakini mchezo wa kuniyumbisha anaucheza yeye akijua siku zitaenda na nitadhika kuwa yeye ndiye wakati sivyo.Hii maisha ya kuganda masomoni na kusahau mambo ya kitaa Ni shughuli,na usijetafuta mwanamke wa kupoozea unapokuwa umetendwa hell noo,inaleta wrong decided fact.Ni shiida Hawa wa kupoozea,kila Mara Tafuta viwango vyako hakuna shortcut hata Kama umetendwa mazima.
 
Umeshapata tuhela kidogo unaona utelekeze familia. Hata huyo unayemtamani sasa usidhani mapenzi yatakuwa hot milele. Tunaoa ili maisha yaendelee tu.
 
Sasa umemuacha aondoke na binti yako?! Ujinga wa kutotumia condom wakati unajua huna malengo wala mapenzi kwa wanawake zenu ...unapelekea watoto wengi kulelewa na mama/baba wa kambo(hii ni mbaya).
Na hapo umejifikiria wewe umesahau kuna mtoto ako.
Hivi kuna "utalaamu" wa kutumia condom kwa mwanamke unayeishi naye kama mke na mme.

For me I can only manage to use condom for a "one night stand"
 
Ubaya sio kwambia humpendi huyo mwanamke ila shida ni kwamba umeishi nae mda wote mpaka umemzalisha na umemtelekeza kwa hiyo utalipwa tu
 
Nimesoma comment zote so far zilizotolewa
Zaidi ya asilimia 90% wanashauri kuwa usifanye hivyo kwani karma itakuja kukuwajibisha. Ni wachache wenye mtazamo kinzani na huo kuwa usiogope kutafuta kile unachokipenda coz sio afya either kuishi kwa kuogopa kuonekana mbaya.

Kundi la kwanza mbali na kusisitiza uwajibikaji ila hoja yao imejengeka kihisia ya hofu, kuwa bila shaka utalipia na utateseka pia. Swali ni kuwa mbona hata sasa unavyoishi nae pia unateseka na hauna furaha???

Maisha siku zote ni kuchagua. Hakuna maisha yaliyokamilika ila ni vizuri kuchagua yale yanayokupa amani na kijisikia vizuri. Maisha yana maudhi sana hivyo ni busara kujaribu kuyaishi katika mazingira yenye shock absorber and stress relief.

Sina uzoefu mkubwa na maisha haya ila naamini always kuna fursa ya kuchagua vyema Kama unahisi umekosea. Kuanza upya sio ujinga wala udhaifu ila ni kuwa na mtazamo chanya wa kuwa you deserve the best.

Daima Kuna changamoto kupata ushauri wa mambo ya mahusiano hasa kunapokua na msingi wa kihisia ndani yake Kama hilo la kutojulikana hatima ya mtoto, na bahati mbaya hujaeleza unavyowajibika au una mipango ipi umeiweka juu ya future ya mwanao.

Ni vizuri kuwa mwajibikaji. Sifa hii ndo inafanya watu ku surcrifice maisha na ku compromise a lot ili tu kubalance mambo . Ndoa nyingi Kama sio zote wanandoa sio kuwa wanafurahia Sana na kulizika bali kinachowaweka pamoja ni hiyo sense ya uwajibikaji.

Hivyo bro ni wakati wako wa kufanya maamuzi. Zingatia mantiki na uhalisia wa mambo na sio hofu pale unapotaka kufanya maamuzi. Zaidi Sana zingatia ndoto zako na maono ya maisha yako. Tunaishi mara moja huna sababu ya kuishi maisha yako kwa huzuni na majuto.
 
Mapenzi sio huruma. Ni bora uishi na mtu unayempenda katika maisha yako kuliko usiyempenda. Hata angekuwa dada yangu siwezi kulazimisha aishi na mtu ambaye hampendi
Sure mkuu...hakuna kitu kigumu kama kukaa na mwanamke usiempenda ndani...yani unakua unamuona kero tu,kila analofanya unaona kero hata liwe jema vipi. Utakua unamnyanyasa sana kihisia na utajidhulumu nafsi..na hata wakiendelea kukaa pamoja hawatofika mbali maana hakuna mhimili (upendo) ambao unawaunganisha..
 
Huyu Karma anayo hakuna namna ataikwepa! Kama anataka kuikwepa aamua moja Amrudie karma isimpate au achomoe Betri Karma iwe sehemu yake ya Maisha. Mdau mmoja hapo juu kapendekeza ufanyapo ngono na mtu usiye mjua vizuri tumia condom.
hakuna haja ya kujitesa kwa kivuli cha karma mkuu....imagine akiendelea kukaa na huyo mwanamke afu maisha yao ya ndoa yasiwe na amani wala furaha daima..inakua haina maana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…