USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

tia chaka wagema ulimbo hao hawana mpango wowote hao,kupeana kula gani huko?
 
Ni nadra sana kwa nchi hii wazo zuri km hili kutolewa kutoka CCM, kwanza tumpongeze kashililla kwa wazo tamu na constructive km hili, Sasa wana JF Wote tupiganie kwa njia zozote zile hawa wa sasa iwe mwisho, Ni upumbavu uliokithiri kujaza watu wale.
 
kwenye nyeusi ni TAMAA mbaya tu ya maisha inawasumbua hao kina mama

TAMWA-wawezeshwe zaidi na serikali wana nguvu kuliko hao waokwenda bungeni kwa viti maalum
Huyo kwenye nyekundu ni kumnyanyapaa, kwani albino sio watu kuwakilishwa na wabunge wao wa majimbo ina maana wakiwa na shida hao wabunge wa majimbo wanayotoka hawawasikilizi na kama ndio hivyo huyo mmoja tu bungeni hataweza nini? anawezaje kuwakilisha albino nchi nzima, huu ni ujinga wa kupindukia.
mimi bado sijaona faida ya kuunguza mabilioni ya pesa kwa watu wasio na tija kwa TAIFA ili mradi tusifiwe na mashirika ya kimataifa kwamba tuna uwakilishi mkubwa wa wanawake wakati hakuna wanachofanya au hata hao wanaopatikana wanapatikana kwa njia za panya!!!
nchi kama marekani wanawake ni asilimia 19% ya uongozi na Tanzania ni 36%

ni lakini hao ndio tunawaomba misaada na tunawaiga kila siku, ukifanya utafiti unaweza kukuta nchi yetu hivi nafasi za kupeana ni nyingi mno tena kuanzia shuleni na ndio maana tunazidi kuwa masikini kila kukicha,
kama kuna chama kinaona kuna umuhimu wa kuwa na wanawake kuingia bungeni wawasimamishe kwenye majimbo na wawape pushi huko, kuliko kupoteza zaidi ya bilion 50, kununua sifa za kimataifa na tunazikufa na njaa hata vyandalua tunaomba msaada

 
Hii imekaa sawasawa Dr. Kashilila, umepoza hasira zetu baada ya juzi kutuletea mada ya kumbeba Spika madhaifu yake kwa kuwasingizia Wabunge wapya!
 
...NAMUUNGA MKONO KABISA DR KASHILILA...HIVI VITI MAALUM VIHARAMISHWE KWENYE KATIBA MPYA KWANI IMEKUWA CHANZO CHA WAANASIASA KUWAPA ZAWADI WATU BILA KUANGALIA UWEZO...KUNA WABUNGE HASA HAO WA VITI MAALUM WANANUKA TU MIDOMO BUNGENI ...YAANI WAMEKUWA MABUBU........
KUNA WENGINE WAAJANJA WAJANJA KAMA KINA RITA MLAKI NA WENGINE WAO WANACHEZA TU KARATA HUKO....WAKAPAMBANE KAMA KINA HALIMA MDEE NA ANNA TIBAIJUKA..
NAPENDEKEZA KUWA VITI MAALUM VYA BURE VIONDOLEWE TUJE NA UTARATIBU MPYA WA KUPATA KINAMAMA WANNE KILA MKOA KWA UTARATIBU WA KUPIGIWA KURA ...UCHAGUZI MKUU TUCHAGUE RAIS ,WABUNGE JIMBO,WABUNGE WA MIKOA [4 KILA MKOA] KINAMAMA,NA MADIWANI...NA MADIWANI WA UPENDELEO PIA WAFUTWE.....TUSIWE NA MTU AMBAYE HAKUCHAGULIWA KWA KURA BUNGENI...SIO SASA AMBAPO KUNA AMBAO HADI WANAKILISHA NGO,VYUO ..etc wakati hizo taasisi baadhi haziwatambui.
 
huu ulikuwa ujanja wa ccm wakati ule kutumia hela yetu ya kodi vibaya
hakuna hata cha mikoa, bunge liwe na wabunge wa majimbo na kila chama kiakishe kina weka wagombea wa kutosha kutoka wanawake kutoka majimboni,
KWANZA hao wanaoingia kwa viti maalumu ni vilaza wote wanaojiweza wanachukua majimbo na hao wako wengi tu, TAMWA iwezeshwe kuwasaidia wanawake kuingia mjengoni kwa kutumia majimbo, na wakifanya hivyo watapata wanawake makini na wengi kuliko sasa, kwa mfano kama mwanamke ni makini anashindwa kung'a mbunge kama KOMBA kweli, au huyo kutoka zanzibar mwenye asilimia 19% ya wapiga kula,
WOTE WATOKE MAJIMBONI INAWEZEKANA KABISA na hao wa vyuoni ndio kabisa tuandamani wafukuzwe wakasome,
huu wizi jamii duh,
 
Mkuu vipi? Kuna akina John Komba yeye hulala tu

Mkuu Rev Fr Masanilo, wako wengi wanalala tu bungeni na wengine hawalali ila hakuna wanachochangia kwenye mijadala kama Rostam Aziz. Lakini wana justification kwamba wamechaguliwa na wanawakilisha wananchi wa jimbo fulani, tatizo hapa ni wale wanaowachagua (yaani wananchi wenyewe). Kwa upande wa viti maalum, hakuna kabisa sababu ya msingi ya kuwa na wabunge wa viti maalum, hawana tija zaidi ya kula kodi zetu na kuleta mipasho na ushabiki wa kisiasa bungeni.Wafutwe tu!!
 

Ingekuwa uwezo wangu hawa wabunge wa viti vya upendeleo aka viti maalum ningewapiga stop mara moja kuanzia bunge lijalo.....hawana uhalali wa kuwepo..........
 
wakuu naona hii ni kero ya wengi, na hakuna sababu ya kusubilia katiba, kwamba hao wabunge hawakuchaguliwa na mtu yeyote ila vyama vyao, kwa sababu tunapoteza hela nyingi kwa hawa wabunge
tufanye mkakati wa kuvisukuma vyama vya siasa kukubali kuwatema hawa wabunge,
najua Dr Slaa , Makamba , NAPE, ZITTO, MZEE MTEI, MNYIKA na wanasiasa wengine wapo humu lakini naona wamekaa kimya au hawajaiona hii hoja lakini tunataka kusikia KUTOKA kwao,
hizi ni pesa nyingi tunaongelea hapa ni zaidi ya bilioni 50, kwa budget ya miaka mitano ukiweka mishahara na posho zao pamoja na magari (japo hawana majimbo yenyewe barabara mbovu)
hii mbona lazima tuimwage hii pesa ikatumika kwenye mahospitali shule na huduma nyingine za jamii, kwa mfano TABORA hakuna barabara za lami, kwa miaka yote kumi ya kikwete na kumi ya mkapa tungekuwa wapi kama hii pesa ingeokolewa
kila mbunge hatoke jimboni kama kuna wanawake wanatakiwa basi tutumie mfumo wa uingereza kuwapata hao kima mama.
 

- Kusiwepo kabisa na hivyo viti kila mmoja agombee mwenyewe kwa ubavu wake, wengine walale vijijni wanatafuta kura wengine wanazunguka mijini na kupata ubunge wa bure, unfair deal kwa taifa!


FMEs!
 
bora wangekuwa wao ni wachapa kazi na wenye uchungu na nchi lakini wao ndio washabiki wakubwa wa vyama na kijipodoa tu, ina maana tunalipia mashabiki wa chama viingilio mjengoni kwa kuwapa posho na magari ya anasa
mbona kilango anaweza, na wao watafute style ya kutokea sio kuchuna mbuzi tu muda wote, tumechoka kupe wamekuwa wengi

- Kusiwepo kabisa na hivyo viti kila mmoja agombee mwenyewe kwa ubavu wake, wengine walale vijijni wanatafuta kura wengine wanazunguka mijini na kupata ubunge wa bure, unfair deal kwa taifa!


FMEs!
 
Mimi binafsi na mpongeza sana dr kwa sababu ameliona hili,ni pesa za wavuja jasho ndizo zinachezewa,nchi inamatatizo makubwa eg wanafunzi hawapati mikopo kwa kiwango kinachohitajika,hakuna madawati ktk shule zetu,walimu hawana nyumba,hivi kwani nini tuwalipe watu mshahara wakati hawana kazi?
 


Ni kweli kaka umenena. Lkn umesahau wale kina Mughwai Likisu wa kule Singida(kitu na dada yake), demu wa zamani wa silaha , Nyerere (brother n sister), Ndesa, Owenya na Kiwelu (Baba ,mtoto na mkwe)
tena hawa hawakuchaguliwa hata kwenye hivyo viti maalum bali waliteuliwa na Kamati maalum. sasa swali ni Je! wanamuwakilisha nani? Chama, Kamati iliyowateuwa au Wananchi?
 
hii sio hoja chama mkuu ni hoja kwa taifa zima kwa ujumla, ukileta mambo ya chama
ccm ndio watapata maumivu zaidi kwa sababu zifuatazo

  1. CCM NDIO WAASISI WA VITI MAALUMU (wandio wameshika hatamu)
  2. CCM INA WABUNGE WENGI BUNGENI KAMA WANGEKUWA WANAJARI MASLAHI YA TAIFA WANA NGUVU NA UWEZO YA KUFUTA HUU UPUUZI
  3. TOKA KUPATA UHURU WATAWALA NI CCM
  4. KAMA CHADEMA WAMEFANYA HAYO KWA KUVUNGA SHERIA SERIKALI YA CCM HIKO WAPI?
  5. HAYA MABILIONI TUNAYOPOTEZA NI KUTOKA NA KATIBA MBOVU INAYOTETEWA NA CCM
  6. MKUU WA KAYA ANA WAKE ZAKE WENGINE TU WAMEINGIA BUNGENI KWA HII NJIA
  7. MFUMO MBOVU NA MATOKEO YA HAYA YOTE CHANZO NA MUKUFUNZI NI CCM
  8. UOZO WOTE WA NCHI HII WANAOBEBA LAWAMA NI CCM (WAO WANA SERIKALI NA KAMA WANGETUNGA SHERIA BORA NA KUZIVUATIALIA TUNGEKUWA MBALI NA MIJADALA KAMA HII ISINGEKUWEPO ILA WALIKUWA WANANUFAIKA NAYO, SINA MAANA CHAMA KINGINE KIWAIGE ILA CHANZO CHA HAYA YOTE NI CCM NA UBINAFSI WAKE.
Ningeomba tuweke vyama mbali kwa ili, sio kuja kunyoosha vidole hapa kwa manufaa ya chama furani, mimi sijari nani kafanya nini maana mfumo uliopo ndio tatizo na sasa ni wakati wa kufunga hii milango ya udhalimu hapa nchini, watu wanakufa njaa wengine na vimada wao wanagawana mali za umma hapana, kila mtu arudi nyuma na kuokoa haya mabilioni tunayoliwa,
TAMWA inatosha, wapewe nafasi nyingine katika serikali kama watendaji na viongozi, lakini bungeni kila mtu aingie kwa jimbo,
 
Wabunge maalum 102 ikiwa ni sawa na kupoteza zaidi ya bilion 50, basi kihalisia ni sawa na kupoteza barabara ya kilometre 50 ya kiwango cha lami kila miaka 5.
 
UKIREJEA TOKA IANZE NI SAWA NA MIAKA YA MKAPA NI KARIBU KILOMETA 200, WEKA WA NA WABUNGE WA RAIS ANAOCHAGUA KWENYE VIKAO VYA KAHAWA,
KWA SASA TUNGEKUWA NA HOSPITAL KUBWA ZAIDI YA KUMI ZIKO VIKIWA NA VIFAA AU TUNGEKUWA NA VYUOKA KAMA UDOM KAMA 6 KWA HIYO PESA. WAKATI HUO HUO SERIKALI HAINA 40 BILION KWA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI LINALO GHALIMU JUMLA YA bilioni 100, na chuo cha UDOM ni DENI alijalipwa, sasa kama tuna hali mbaya hivi kwa nini tuokoe hela katika matumizi holela kama haya
Wabunge maalum 102 ikiwa ni sawa na kupoteza zaidi ya bilion 50, basi kihalisia ni sawa na kupoteza barabara ya kilometre 50 ya kiwango cha lami kila miaka 5.
 
Unaumwa sana, ni chama gani chenye wabunge wengi wa namna hii? Jibu ni CHAMA CHA MAGAMBA, wabunge zaidi ya 60 ni wahudumu wa mabosi wenu.

Sasa naona hoja imevamiwa tumeanza kujadili watu binafsi badala ya kada ama kundi, nafikili hapa tunajadili kundi la wabunge wa viti maalum dhidi ya wa majimbo katika kuhudumia wananchi na matumizi ya rasilimali za nchi. Kimsingi hata mimi sioni mantiki ya kuwa na wabunge wa viti maalum wakati kila jimbo katika nchi hii lina mbunge aliyechaguliwa na wananchi wote bila kujali jinsia. Si hao tu bali hata hawa wanaoteuliwa na Rais naona hawana kazi na wenyewe wafutwe ikiwa ni kupunguza matumizi lakini pia dhana ya uwakilishi wa walipa kodi wa nchi hii.
 
Bravo Kashilila, kwa hili umefanya upembuzi yakinifu bila ushabiki.
 
wakifutwa ndo demokrasia itakuwa; na tutakuwa na wabunge wawakilishi wa watu majimboni.naunga mkono hoja ya katibu wa bunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…