Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,717
- 13,176
tia chaka wagema ulimbo hao hawana mpango wowote hao,kupeana kula gani huko?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dhana nzima ya viti maalum IFUTWE KABISA. Miaka 50 ya Uhuru watu hawajakomaa mpaka wabebwe na viti maalum? Hao wanaosema kuwa wabunge wa viti maalum wana mchango mkubwa ni upi huo? na hawawezi kuutoa huo mchango mpaka wawe bungeni? mambo ya kujiuliza;
1. Kuna wabunge viti maalum-vijana je vijana wamefaidika nini kupitia kwa uwakilishi wao? ajira? elimu bora?
2. Wabunge wa wanawake - ni kitu gani wamesaidia wamama? watoto wa kike wanabakwa kila kukicha hawa wabunge wanawakilisha nini hasa? Mbona TAMWA wanatoa mchango mkubwa tu kwa wanawake bila uwepo wao bungeni?
3. Na hawa wabunge viti maalum - vyama vya wafanyakazi wanateteaje maslahi ya wafanyakazi? Bunge lililopita Mh. Mnyika alikuwa anatetea uwakilishi wa wafanyakazi idara fulani hakuna mbunge kupitia vyama vya wafanyakazi aliyejitokeza kumuunga mkono! Mishahara ya wafanyakazi mgogoro wako wapi hao wabunge wa viti maalum?
4. Ndugu zetu maalbino wanapata shida sana na wengine wameuliwa kinyama. Mh. Shymaa (sorry my spelling) kafanya nini tangu alipoteuliwa? Alishaleta hata hoja binafsi kutetea haki za maalbino? Hivi Mh.Shymaa anaweza kusema ni kesi ngapi zinazousiana na maalbino ziko mahakamani? na ajenda yake ni nini hasa kuhusu haki za maalbino?
5. Mama Ana Abdallah amekuwa bungeni kwa kipindi kirefu kuliko wabunge wote walioko bungeni kwa sasa. Na tunajua kipindi hiki kapitia viti maalum -NGOs. (yeye pamoja na Rita Mlaki). Sasa NGOs zinafaidika vipi na uwakilishi wa hawa watu?. Kuna nini hasa kimebadilika tangu wawili hawa waingie bungeni kwa tiketi hiyo ya NGOs?
Hivi vijana, wanawake, wafanyakazi, NGOs vikundi vyote hivi haviko kwenye majimbo? Mfano kwenye jimbo la Temeke mbunge atakuwa anahudumia watu walio nje ya hivyo vikundi?
Note: Yapo majimbo mengi yenye wakazi wengi. Kwa mfano, jimbo la Ubungo lina watu zaidi ya laki moja (100,000). wakati huo huo kuna majimbo yana watu wachache i.e chini ya 8,000. Kama Serikali ina uwezo kwa kulipa wabunge wa majimbo ya kinadharia kwa nini basi wasigawe/kupunguza ukubwa wa majimbo yenye watu wengi ili kila mbunge apata pa kugembea na zaidi awajibike kwa wananchi na sio kwa vyama vya siasa.
KATIBA MPYA inakuja. ni vizuri TUFUTE KABISA viti maalum. Hivi viti ni maalum kulinda sheria za kinyonyaji, maalum kusifia serikali hata pale inapozembea kutimiza wajibu wake kwa wananchi, maalum kupumbuza watu kuwa maslahi yao yanawakilishwa wakati sio kweli, maalum kuendeleza nidhamu ya woga na unafiki. Hivi viti ni maalum kuangamiza umma ili mradi wakubwa waneemeke. Viti maalum wafutwe. Kabisa.
...NAMUUNGA MKONO KABISA DR KASHILILA...HIVI VITI MAALUM VIHARAMISHWE KWENYE KATIBA MPYA KWANI IMEKUWA CHANZO CHA WAANASIASA KUWAPA ZAWADI WATU BILA KUANGALIA UWEZO...KUNA WABUNGE HASA HAO WA VITI MAALUM WANANUKA TU MIDOMO BUNGENI ...YAANI WAMEKUWA MABUBU........
KUNA WENGINE WAAJANJA WAJANJA KAMA KINA RITA MLAKI NA WENGINE WAO WANACHEZA TU KARATA HUKO....WAKAPAMBANE KAMA KINA HALIMA MDEE NA ANNA TIBAIJUKA..
NAPENDEKEZA KUWA VITI MAALUM VYA BURE VIONDOLEWE TUJE NA UTARATIBU MPYA WA KUPATA KINAMAMA WANNE KILA MKOA KWA UTARATIBU WA KUPIGIWA KURA ...UCHAGUZI MKUU TUCHAGUE RAIS ,WABUNGE JIMBO,WABUNGE WA MIKOA [4 KILA MKOA] KINAMAMA,NA MADIWANI...NA MADIWANI WA UPENDELEO PIA WAFUTWE.....TUSIWE NA MTU AMBAYE HAKUCHAGULIWA KWA KURA BUNGENI...SIO SASA AMBAPO KUNA AMBAO HADI WANAKILISHA NGO,VYUO ..etc wakati hizo taasisi baadhi haziwatambui.
Mkuu vipi? Kuna akina John Komba yeye hulala tu
Mkuu Rev Fr Masanilo, wako wengi wanalala tu bungeni na wengine hawalali ila hakuna wanachochangia kwenye mijadala kama Rostam Aziz. Lakini wana justification kwamba wamechaguliwa na wanawakilisha wananchi wa jimbo fulani, tatizo hapa ni wale wanaowachagua (yaani wananchi wenyewe). Kwa upande wa viti maalum, hakuna kabisa sababu ya msingi ya kuwa na wabunge wa viti maalum, hawana tija zaidi ya kula kodi zetu na kuleta mipasho na ushabiki wa kisiasa bungeni.Wafutwe tu!!
...NAMUUNGA MKONO KABISA DR KASHILILA...HIVI VITI MAALUM VIHARAMISHWE KWENYE KATIBA MPYA KWANI IMEKUWA CHANZO CHA WAANASIASA KUWAPA ZAWADI WATU BILA KUANGALIA UWEZO...KUNA WABUNGE HASA HAO WA VITI MAALUM WANANUKA TU MIDOMO BUNGENI ...YAANI WAMEKUWA MABUBU........
KUNA WENGINE WAAJANJA WAJANJA KAMA KINA RITA MLAKI NA WENGINE WAO WANACHEZA TU KARATA HUKO....WAKAPAMBANE KAMA KINA HALIMA MDEE NA ANNA TIBAIJUKA..
NAPENDEKEZA KUWA VITI MAALUM VYA BURE VIONDOLEWE TUJE NA UTARATIBU MPYA WA KUPATA KINAMAMA WANNE KILA MKOA KWA UTARATIBU WA KUPIGIWA KURA ...UCHAGUZI MKUU TUCHAGUE RAIS ,WABUNGE JIMBO,WABUNGE WA MIKOA [4 KILA MKOA] KINAMAMA,NA MADIWANI...NA MADIWANI WA UPENDELEO PIA WAFUTWE.....TUSIWE NA MTU AMBAYE HAKUCHAGULIWA KWA KURA BUNGENI...SIO SASA AMBAPO KUNA AMBAO HADI WANAKILISHA NGO,VYUO ..etc wakati hizo taasisi baadhi haziwatambui.
- Kusiwepo kabisa na hivyo viti kila mmoja agombee mwenyewe kwa ubavu wake, wengine walale vijijni wanatafuta kura wengine wanazunguka mijini na kupata ubunge wa bure, unfair deal kwa taifa!
FMEs!
Wabunge wa viti maalum ni kirima tu, ndio maana tumeshuhudia vigogo wa CCM mume na mke wamekuwa bungeni mume wa kuchaguliwa na mke wa ubunge wa kirima. Wabunge wengine ni mabishow bungeni labda wana mabosi wao waliowaweka pale, maana wanachosubiri ni posho tu na hakuna mchango wanaotoa ila kuzomea tu.
Ni kweli kaka umenena. Lkn umesahau wale kina Mughwai Likisu wa kule Singida(kitu na dada yake), demu wa zamani wa silaha , Nyerere (brother n sister), Ndesa, Owenya na Kiwelu (Baba ,mtoto na mkwe)
tena hawa hawakuchaguliwa hata kwenye hivyo viti maalum bali waliteuliwa na Kamati maalum. sasa swali ni Je! wanamuwakilisha nani? Chama, Kamati iliyowateuwa au Wananchi?
Wabunge maalum 102 ikiwa ni sawa na kupoteza zaidi ya bilion 50, basi kihalisia ni sawa na kupoteza barabara ya kilometre 50 ya kiwango cha lami kila miaka 5.
Unaumwa sana, ni chama gani chenye wabunge wengi wa namna hii? Jibu ni CHAMA CHA MAGAMBA, wabunge zaidi ya 60 ni wahudumu wa mabosi wenu.