Hivi majukumu ya "Viti maalumu" na Wabunge wa "Kuteuliwa" na wa "kuchaguliwa" yanatofautiana?
Inashangaza wanawake wanapodhalilishwa (kwa kupewa viti maalum) na wakashangilia kabisa....
Believe me or not, bila viti maalumu hakuna wakuwatetea wanawake, watoto wala wenye uhitaji zaidi(walemavu)
Hapo mkuu unakosea... kupewa viti maalum sio udhalilishaji... inavotumika ndio udhalilishaji.... Maana ni wazi kuwa katika eneo kubwa la nchi yetu wanawake wanadhauliwa... hivo naomba ubadilishe dhana ya kusema tunashangilia kupewa viti maalum hali ni udhalilishaji...
Katibu wa Bunge alisha sema Viti Maalumu ni Mzigo kwa serikali aisee walimjia juu, sidhani kama atarudia tena kuseama!!Hakuna kinachotafautiana......na hata huo "wajibu" wao wa kutetea wanawake hawaufanyi. Ndio maana Zitto Kabwe akawachinjia baharini wabunge wa viti maalum Chadema, akasem hawana thamani sawa na wabunge wa kuchaguliwa
Inavyotumika ki vipi?Hapo mkuu unakosea... kupewa viti maalum sio udhalilishaji... inavotumika ndio udhalilishaji.... Maana ni wazi kuwa katika eneo kubwa la nchi yetu wanawake wanadhauliwa... hivo naomba ubadilishe dhana ya kusema tunashangilia kupewa viti maalum hali ni udhalilishaji...
ADii...
Kupewa viti maalum ni kupendelewa....na kupokea ni kukubali kupendelewa....na kupendelewa na kukubali udhaifu na unyonge.......kukubali udhaifu na unyonge ni kudhalilishwa......
Inavyotumika ki vipi?
2015 ingia kwenye mchakato bana, achana na hii dhana ya kupewa!
Mkiamua mnaweza bana sio mkiwezeshwa?
Ukiiweka in a way umeelezea yaweza sound hivo... But ukweli ni kwamba majority ya wanawake wa Tanzania have a long way to go before hajakubalika na jamii iwe wake kwa waume kwa yeye kuweza kufika mbali katika uongozi... Itachukua mda - maeneo ya mjini yaweza onekana kama vile wamejikomboa (but that is just on the surface) for mwanamke kugombea nafasi katika jamii hasa katika masuala ya siasa inatumia hata mara kumi ya energy katika Campaigns but napo aweza shindwa....
Kama nilivo point out katika my first post... wangewezeshwa zaidi wanawake wakapewa nafasi ya kuweza simamia mambo katika jamii (for jamii bado kumkubali kwa hiari...) ingesaidia sana.... Hivo kwa sasa useless.... pamoja na kusema i don't agree kuwa kupewa hio nafasi ikatumika genuinely ni udhalilishaji....
Believe me or not, bila viti maalumu hakuna wakuwatetea wanawake, watoto wala wenye uhitaji zaidi(walemavu)
Hivyo viti maalum ushamuona mtu alotoka kijijini as kijijini akapewa?
Chadema wao waliweka vigezo ambavyo mtu hasa anaehitaji kuwezeshwa hawezi kuvipata hata kidogo. Points zinaongezwa ukiwa na phd, ukiwa umefanya kazi mashirika ya kimataifa, n.k.
Hivi mwenye PhD na aliyefanya kazi za uongozi kwenye taasisi za kimataifa anahitaji kuwezeshwa kweli?
Vifutwe mara moja
Gaijin labda nikuulize... kuna ubaya wa kuweka vigezo kama hivo hapo juu... (Phd thou ni extreme)
Na unaposema vifutwe mara moja... sababu hio nafasi haifai kwa vilivo tumika sasa OR sababu tu wanawake wasiwezeshwe (as the saying goes...)
Kuna ubaya sana wa kuweka vigezo vya namna hiyo. It means wale wanaotaka kuwezeshwa hasa waliokosa fursa bado hawatapata, watapata wale waliosoma sana na kufanya kazi sehemu nzuri ambao tayari wameshaweza na hawahitaji kuwezeshwa. Besides hakuna utafiti wowote unaoonyesha kuwa kila ukiwa na elimu kubwa ndio unaweza kuongoza vizuri na kuwa mwakilishi bora wa wananchi (angalia Juma Kapuya, Chenge, ulinganishe labda na Mbowe et al. )
Vifutwe mara moja kwa sababu the whole system is crap. Na pia kwa kuwa mwanamke hahitaji kuwezeshwa huko. Kama wanahamu sana na nia madhubuti ya kumuwezesha mwanamke na wampe elimu bora na hata kufungua chuo kikuu cha wanawake. Hii ya kuwapa fish wanawake mia moja badala ya kuwafundisha how to fish wanawake wote Tanzania ni upuuzi usio mithilika
Dhana nzima ha viti maalum ilikua kuwezesha wanawake (wale ambo ni dhahiri wanaweza tokana na u-active wao) waweze jaza hizo nafasi ili kuonesha kua mtu yeyote aweza ongoza regardless ya Sex (female/male) ya mtu.... Hii ilikua proposed as one of the strategies ya kuweka equality na equity kati ya wake kwa waume kweny nchi ambayo bado i wazi kua inakumbatia mfumo dume in some elements... Hivo it was the best decision in politics katika nchi (kwa wanawake)... Pia tokana na ukweli kwamba wanawake wengi hata kama anaweza kuliko hata huyo mwanaume ambae ni candidate mwenzie hutokea kushindwa kwa kudharauliwa kua ni mwanamke - akakae nyumbani na kulea watoto...
Regardless ya maelezo yangu hapo juu... Viti maalum kwa sasa katika hali halisi ni moja ya maeneo ambayo ni useless na taka taka kabisa... hio tokana na ukweli kua hizo nafasi zimechakachuliwa na walowekwa hapo in most cases ni nyumba ndogo au relatives wa karibu... wadada wadogo wadogo wameshika nafasi kubwa mno (sisemi hawawezi but in most cases wanauza sura...) Kuna wilaya niliwahi tembelea... yaani mkuu wa wilaya ni mdada ambae anaonekana kabisa kabebwa na wala haelewi zaidi ya kukaa ofisini afanye nini la ziada.... Sad. Hao ndio wanafanya tuonekane wanawake woote hatuwezi kitu ambacho si kweli... ukweli unabaki means zilizotumika kuchaguliwa zimevuka kabisa sababu na vigezo za kucover hizo nafasi...
My Stand: Hizo nafasi ni muhimu mno for once in a while kuna issues katika aspect mbali mbali nchini zinahitaji a woman's touch. However kama hawatabadilisha vigezo vya mtu kuteuliwa kua speacial seats... ni bora wafute kabisa kuliko kuendelea kutumia mamailioni kwa ajili ya watu wasio faa wala kuwajibika...
Luna De Silva kaiongoza Brazil akiwa na elimu ya msingi tu, na alichokifanya kwa maendeleo ya Brazil kinaonekana wazi.
Cheti cha elimu hakina msingi wowote kwenye uongozi bora.
Luna De Silva kaiongoza Brazil akiwa na elimu ya msingi tu, na alichokifanya kwa maendeleo ya Brazil kinaonekana wazi.
Cheti cha elimu hakina msingi wowote kwenye uongozi bora.