USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Hivi majukumu ya "Viti maalumu" na Wabunge wa "Kuteuliwa" na wa "kuchaguliwa" yanatofautiana?

Hakuna kinachotafautiana......na hata huo "wajibu" wao wa kutetea wanawake hawaufanyi. Ndio maana Zitto Kabwe akawachinjia baharini wabunge wa viti maalum Chadema, akasem hawana thamani sawa na wabunge wa kuchaguliwa
 
Inashangaza wanawake wanapodhalilishwa (kwa kupewa viti maalum) na wakashangilia kabisa....
 
Inashangaza wanawake wanapodhalilishwa (kwa kupewa viti maalum) na wakashangilia kabisa....

Hapo mkuu unakosea... kupewa viti maalum sio udhalilishaji... inavotumika ndio udhalilishaji.... Maana ni wazi kuwa katika eneo kubwa la nchi yetu wanawake wanadhauliwa... hivo naomba ubadilishe dhana ya kusema tunashangilia kupewa viti maalum hali ni udhalilishaji...
 
Believe me or not, bila viti maalumu hakuna wakuwatetea wanawake, watoto wala wenye uhitaji zaidi(walemavu)

Mkuu Remmy,
Najua hapa unasema kwa hisia kuliko uhalisia...
Kwani wanawake (au hata wanaume) wanaochaguliwa hawawezi kupokea na kuyapeleka bungeni matatizo ya wanawake?
Kuna uwakilishi gani wa muhimu kiasi cha kuhitaji mtu maalum wa kuwakilisha?

Nakubaliana na uwezeshaji wa wanawake (kwamba walikandamizwa), ili waweze kushindana na wanaume (na mfumo dume?).....ila kwamba ni wawakilishi wa matatizo ya wanawake...hapana!
 
Hapo mkuu unakosea... kupewa viti maalum sio udhalilishaji... inavotumika ndio udhalilishaji.... Maana ni wazi kuwa katika eneo kubwa la nchi yetu wanawake wanadhauliwa... hivo naomba ubadilishe dhana ya kusema tunashangilia kupewa viti maalum hali ni udhalilishaji...

ADii...
Kupewa viti maalum ni kupendelewa....na kupokea ni kukubali kupendelewa....na kupendelewa na kukubali udhaifu na unyonge.......kukubali udhaifu na unyonge ni kudhalilishwa......
 
Hakuna kinachotafautiana......na hata huo "wajibu" wao wa kutetea wanawake hawaufanyi. Ndio maana Zitto Kabwe akawachinjia baharini wabunge wa viti maalum Chadema, akasem hawana thamani sawa na wabunge wa kuchaguliwa
Katibu wa Bunge alisha sema Viti Maalumu ni Mzigo kwa serikali aisee walimjia juu, sidhani kama atarudia tena kuseama!!
Kazi yoyote ambayo mwisho wa siku huna pa kuwajibika lazima utaifanya kwa matakwa yako, maana mwisho wa siku hakuna wa kukuhoji we ulikua bungeni miaka mitano nini umekifanya ila tusikuhukumu? ndo maana hawana presha kazi ni kuleta mipasho tu huko bungeni!!
 
Hapo mkuu unakosea... kupewa viti maalum sio udhalilishaji... inavotumika ndio udhalilishaji.... Maana ni wazi kuwa katika eneo kubwa la nchi yetu wanawake wanadhauliwa... hivo naomba ubadilishe dhana ya kusema tunashangilia kupewa viti maalum hali ni udhalilishaji...
Inavyotumika ki vipi?
2015 ingia kwenye mchakato bana, achana na hii dhana ya kupewa!
Mkiamua mnaweza bana sio mkiwezeshwa?
 
ADii...
Kupewa viti maalum ni kupendelewa....na kupokea ni kukubali kupendelewa....na kupendelewa na kukubali udhaifu na unyonge.......kukubali udhaifu na unyonge ni kudhalilishwa......

Ukiiweka in a way umeelezea yaweza sound hivo... But ukweli ni kwamba majority ya wanawake wa Tanzania have a long way to go before hajakubalika na jamii iwe wake kwa waume kwa yeye kuweza kufika mbali katika uongozi... Itachukua mda - maeneo ya mjini yaweza onekana kama vile wamejikomboa (but that is just on the surface) for mwanamke kugombea nafasi katika jamii hasa katika masuala ya siasa inatumia hata mara kumi ya energy katika Campaigns but napo aweza shindwa....

Kama nilivo point out katika my first post... wangewezeshwa zaidi wanawake wakapewa nafasi ya kuweza simamia mambo katika jamii (for jamii bado kumkubali kwa hiari...) ingesaidia sana.... Hivo kwa sasa useless.... pamoja na kusema i don't agree kuwa kupewa hio nafasi ikatumika genuinely ni udhalilishaji....
 
  • Thanks
Reactions: RR
Inavyotumika ki vipi?
2015 ingia kwenye mchakato bana, achana na hii dhana ya kupewa!
Mkiamua mnaweza bana sio mkiwezeshwa?

Inatumika na viongozi wakubwa kwa ajili ya nyumba bubu ndogo ... hivo kutumika vibaya... In that sense bora vitolewe... 2015 ni mapema mno kwangu kuingia huko... Siasa zenyewe za Tz full propagander.... naona saizi tulee family na kuangalia waliopo kwenye hizo nafasi wanavo dimba...

Na Kimey just for the record nikiamua ku run, najipanga five years before, by the time mda unafika ni with a blast!
 
Ukiiweka in a way umeelezea yaweza sound hivo... But ukweli ni kwamba majority ya wanawake wa Tanzania have a long way to go before hajakubalika na jamii iwe wake kwa waume kwa yeye kuweza kufika mbali katika uongozi... Itachukua mda - maeneo ya mjini yaweza onekana kama vile wamejikomboa (but that is just on the surface) for mwanamke kugombea nafasi katika jamii hasa katika masuala ya siasa inatumia hata mara kumi ya energy katika Campaigns but napo aweza shindwa....

Kama nilivo point out katika my first post... wangewezeshwa zaidi wanawake wakapewa nafasi ya kuweza simamia mambo katika jamii (for jamii bado kumkubali kwa hiari...) ingesaidia sana.... Hivo kwa sasa useless.... pamoja na kusema i don't agree kuwa kupewa hio nafasi ikatumika genuinely ni udhalilishaji....

Hivyo viti maalum ushamuona mtu alotoka kijijini as kijijini akapewa?

Chadema wao waliweka vigezo ambavyo mtu hasa anaehitaji kuwezeshwa hawezi kuvipata hata kidogo. Points zinaongezwa ukiwa na phd, ukiwa umefanya kazi mashirika ya kimataifa, n.k.

Hivi mwenye PhD na aliyefanya kazi za uongozi kwenye taasisi za kimataifa anahitaji kuwezeshwa kweli?

Vifutwe mara moja
 
Gaijin labda nikuulize... kuna ubaya wa kuweka vigezo kama hivo hapo juu... (Phd thou ni extreme)

Na unaposema vifutwe mara moja... sababu hio nafasi haifai kwa vilivo tumika sasa OR sababu tu wanawake wasiwezeshwe (as the saying goes...)
 
Kuna ubaya sana wa kuweka vigezo vya namna hiyo. It means wale wanaotaka kuwezeshwa hasa waliokosa fursa bado hawatapata, watapata wale waliosoma sana na kufanya kazi sehemu nzuri ambao tayari wameshaweza na hawahitaji kuwezeshwa. Besides hakuna utafiti wowote unaoonyesha kuwa kila ukiwa na elimu kubwa ndio unaweza kuongoza vizuri na kuwa mwakilishi bora wa wananchi (angalia Juma Kapuya, Chenge, ulinganishe labda na Mbowe et al. )

Vifutwe mara moja kwa sababu the whole system is crap. Na pia kwa kuwa mwanamke hahitaji kuwezeshwa huko. Kama wanahamu sana na nia madhubuti ya kumuwezesha mwanamke na wampe elimu bora na hata kufungua chuo kikuu cha wanawake. Hii ya kuwapa fish wanawake mia moja badala ya kuwafundisha how to fish wanawake wote Tanzania ni upuuzi usio mithilika
 
Ritha mlaki MB, alikuwa mbunge wa kuchaguliwa kwa miaka kadhaa, akasoma alama za nyakati akaingia viti maalum kupitia NGo, wenye NGO wakauliza mbona mchakato hawakuusikia wakaambiwa mchakato ulikuwa wa kimagamba zaidi. hakuna sababu ya kuendelea na viti maalum
 
Kuna ubaya sana wa kuweka vigezo vya namna hiyo. It means wale wanaotaka kuwezeshwa hasa waliokosa fursa bado hawatapata, watapata wale waliosoma sana na kufanya kazi sehemu nzuri ambao tayari wameshaweza na hawahitaji kuwezeshwa. Besides hakuna utafiti wowote unaoonyesha kuwa kila ukiwa na elimu kubwa ndio unaweza kuongoza vizuri na kuwa mwakilishi bora wa wananchi (angalia Juma Kapuya, Chenge, ulinganishe labda na Mbowe et al. )

Vifutwe mara moja kwa sababu the whole system is crap. Na pia kwa kuwa mwanamke hahitaji kuwezeshwa huko. Kama wanahamu sana na nia madhubuti ya kumuwezesha mwanamke na wampe elimu bora na hata kufungua chuo kikuu cha wanawake. Hii ya kuwapa fish wanawake mia moja badala ya kuwafundisha how to fish wanawake wote Tanzania ni upuuzi usio mithilika

Gaijin kuhusu vigezo ni muhimu saana katika kuchagua mtu anaefaa katika aspect yoyote nyeti hasa ya uongozi… ili mradi viwe logical na visiwe extreme… Hawezi mtu akachukuliwa na kupewa uongozi kisa tu anawezeshwa bila kua na elimu walau hata first degree… maisha na kuendeshwa kwake kumebadilika kabisa… ata cope vipi na technology?… ata cope vipi na mambo ya bureaucracies? Na vitu vyote na uongozi related for further research na analysis kuhuku yanayotokea…. Elimu ni relative term but hapa noana tuseme elimu isichukuliwe tu kua PhD (kama nilivosema ktk last post…. Bit extreme)

Nakubalina na wewe kua vifutwe mara moja for the whole system is Crap!! But sikubali kua vingetumika ipasavo ni useless…Na hayo kwenye blue hapo sasa ndo yangeweza simamiwa na hao ambao wamewekwa special seats ambazo bahati mbaya saana vimechakachuliwa…. And Gaijini any woman who has never fished once given the fish and realizes kua she wants it more – kama kweli ni leadership quality – she will even want to know where/how the fishing rod is made….
 
Dhana nzima ha viti maalum ilikua kuwezesha wanawake (wale ambo ni dhahiri wanaweza tokana na u-active wao) waweze jaza hizo nafasi ili kuonesha kua mtu yeyote aweza ongoza regardless ya Sex (female/male) ya mtu.... Hii ilikua proposed as one of the strategies ya kuweka equality na equity kati ya wake kwa waume kweny nchi ambayo bado i wazi kua inakumbatia mfumo dume in some elements... Hivo it was the best decision in politics katika nchi (kwa wanawake)... Pia tokana na ukweli kwamba wanawake wengi hata kama anaweza kuliko hata huyo mwanaume ambae ni candidate mwenzie hutokea kushindwa kwa kudharauliwa kua ni mwanamke - akakae nyumbani na kulea watoto...

Regardless ya maelezo yangu hapo juu... Viti maalum kwa sasa katika hali halisi ni moja ya maeneo ambayo ni useless na taka taka kabisa... hio tokana na ukweli kua hizo nafasi zimechakachuliwa na walowekwa hapo in most cases ni nyumba ndogo au relatives wa karibu... wadada wadogo wadogo wameshika nafasi kubwa mno (sisemi hawawezi but in most cases wanauza sura...) Kuna wilaya niliwahi tembelea... yaani mkuu wa wilaya ni mdada ambae anaonekana kabisa kabebwa na wala haelewi zaidi ya kukaa ofisini afanye nini la ziada.... Sad. Hao ndio wanafanya tuonekane wanawake woote hatuwezi kitu ambacho si kweli... ukweli unabaki means zilizotumika kuchaguliwa zimevuka kabisa sababu na vigezo za kucover hizo nafasi...

My Stand: Hizo nafasi ni muhimu mno for once in a while kuna issues katika aspect mbali mbali nchini zinahitaji a woman's touch. However kama hawatabadilisha vigezo vya mtu kuteuliwa kua speacial seats... ni bora wafute kabisa kuliko kuendelea kutumia mamailioni kwa ajili ya watu wasio faa wala kuwajibika...

wanawake wote wakifikiri na kuongea kama wewe hakuna haja ya viti maalumu
kwa hoja kama hizi unachukua jimbo la komba na udume wake bila shida

wanaonufaika na hivi viti ni vigogo wala sio wamama na kamwe hivi viti hazitawalenga wamama
vitutwe
 
Luna De Silva kaiongoza Brazil akiwa na elimu ya msingi tu, na alichokifanya kwa maendeleo ya Brazil kinaonekana wazi.

Cheti cha elimu hakina msingi wowote kwenye uongozi bora.
 
Luna De Silva kaiongoza Brazil akiwa na elimu ya msingi tu, na alichokifanya kwa maendeleo ya Brazil kinaonekana wazi.

Cheti cha elimu hakina msingi wowote kwenye uongozi bora.

Ni Lula da Silva na siyo Luna De Silva
 
Luna De Silva kaiongoza Brazil akiwa na elimu ya msingi tu, na alichokifanya kwa maendeleo ya Brazil kinaonekana wazi.

Cheti cha elimu hakina msingi wowote kwenye uongozi bora.

Kitu kimoja Gaijin inabidi ukubali ni kua Watanzania sio wazalendo... Tofauti na Mataifa yalo makubwa makubwa hapa duniani... tunaona Germans, The US, The Chinese na wengine wengi... Huo uzalendo wafanana na Uzalendo wa The Great Man Mandela... for kama ni mzalendo then as a leader everything goes with flow - for you use politics as a means or running the country but never a politician; Thus De Siliva is one of the few exceptions... his history, his interest in welfare of the majority ndo ilimsukuma... Na kwa mwanamke; Great women in the world of politics tunaona Eva Peron - the first lady of Argentina - she was not educated but was a great force in politics sababu tu ya uzalendo (and it was romoured alikua CD huko nyuma thats how ali meet hubby)...

Huo mfano ulotoa bado sijawa conviced kua elimu sio mhimu... kwamba mtu una elimu ya msingi yaani hii ya kiwango cha JK alafu aje kua kiongozi wa nchi?? God Forbid..... Labda awe ni exceptional hasa....
 
We jiulize hivi ni kwa nini Viti Maalumu wengi ni wanawake ambao hawajaolewa?
 
Back
Top Bottom