Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumeona michango yao. Ila kama uwakilishi upo, hakuna haja ya kuwa nao.
Natumaini VITI MAALUM vitaondolewa na KATIBA MPYA. Kwa sasa sio rahisi kuviondoa kwa kuwa vyama vyote vyenye uwakilishi mzuri bungeni vinao hao watu. CHADEMA wao wameweka dada zao, binti zao, wakezao wa zamani, wafuasi wao, yaani! Aibu tupu.

mtanzania yoyote mwenye akili atakubaliana na hoja zote za msingi alizotoa dr kashila sio siri watanzania ni kama hatuna bunge kibaya zaidi wabunge wote wako pale bungeni kwa ajili ya kuwezeshwa na si vinginevyoInawezekana Kashilila ni mtumishi wa mapacha watatu?
mtanzania yoyote mwenye akili atakubaliana na hoja zote za msingi alizotoa dr kashila sio siri watanzania ni kama hatuna bunge kibaya zaidi wabunge wote wako pale bungeni kwa ajili ya kuwezeshwa na si vinginevyo
Thursday, May 5, 2011
Na Victor Makinda, Dar es Salaam
Futa kauli!
We vipi waambiwa huna masikio!
Jamani hatuko klabu tuko bungeni!
Out!out katuburuza huyo!!
SPIKA: Jamani naomba utulivu!!
Hatoki mtu nje!!
Tutatoka wote .!!!
Tufunge mlango tupigane!! !!
Naona mnafanya mnada badala ya kuendelea na Bunge
Msitumie wingi wenu kutuburuza!!
SPIKA: Watu mmechaguliwa na kura za wananchi kwanini mnafanya mambo ya kitoto hivi hamjui kuwa tunaonwa na wananchi?
Inawezekana Kashilila ni mtumishi wa mapacha watatu?
Pia kungekuwa na utaratibu mwengine wa uwakilishi wa Wabunge kutoka Zanzibar.Dk. Kashilila aliwaponda wabunge wa viti maalumu akisema kundi hilo ni mzigo kwa taifa kwa kuwa hawana kazi wanayoifanya zaidi ya kukidhi maslahi ya kisiasa.
Dk. Kashilila alisema ni Tanzania pekee ndiyo yenye wabunge wa aina hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine zinazofuata mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola (Commonwealth).
Mtendaji huyo wa Bunge alihoji sababu za kuwepo kwa kundi hilo la wabunge, wakati wabunge wa majimbo wapo. Wabunge 102 kati ya wabunge 350 waliopo bungeni hivi sasa ni wabunge wa viti maalumu.
Wabunge wa majimbo wapo 239, ndiyo kusema kwamba katika eneo lote la Tanzania hakuna eneo lisilokuwa na uwakilishi bungeni. Ukisema kila mbunge wa jimbo aende jimboni kwake, utakuta nchi yote ipo covered (ina wabunge).
Sasa unajiuliza kama hivyo ndivyo hawa wabunge wa viti maalumu wa kazi gani? Wanafanya kazi ipi special (maalumu) ambayo haifanywi na mbunge wa jimbo? alihoji.
Alipoulizwa iwapo hoja yake hiyo inalenga kushauri wabunge wa viti maalumu wafutwe, Dk Kashilila alisema: Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaiga affirmative policy ya Uingereza.
Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.
Kwa kufanya hivyo tutajikuta tumewaondoa hawa wabunge wa viti maalumu ambao kimsingi mimi sioni kazi wanayofanya na badala yake tutakuwa na wanawake bungeni, lakini wanaotokana na majimbo, alisema.
Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge walitoa maoni tofauti kuhusiana na kauli hiyo, huku baadhi yao wakiipinga wazi wazi kauli hiyo.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) alimshangaa Dk. Kashilila kwa kutoa mashambulizi makali dhidi ya wabunge wa viti maalumu, huku akisema wabunge hao ni watu wenye mchango mkubwa kwa jamii.
Hayo ni maoni yake, lakini kusema wabunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa mimi nadhani siyo sahihi. Wabunge wa viti maalumu wana mchango mkubwa kwa jamii na hata hao walioweka mfumo huu walijua wabunge wa viti maalumu wana mchango.
Tunafanya shughuli nyingi za kijamii, tumekuwa tukisaidiana na wabunge wa majimbo katika mambo mbalimbali. Pale ambapo wabunge wa majimbo hawatimizi sisi tumekuwa tukiziba mapengo. Kwa hiyo si kweli kusema wabunge wa viti maalumu hawana kazi ya kufanya, alisema
Maoni yangu: tunapoteza zaidi ya bilioni 50 kwa miaka mitano kughalimia hawa wabunge wasio na tija kwa taifa wala kwa hao wanawake wanao wawakilisha nadhani tukifuata mfumo wa kiingereza kwa sababu tunafuta huo itakuwa makini zaidi, au kama vipi tuwe na utaratibu ambao wabunge wanatoka kajimboni tu na uwakilishi na ushawishi wao utaoneka wazi wazi, hizo pesa tunaweza kuzitumia kuleta maendeleo makubwa sana, na hawa wakuu wa mikoa na wilaya watolewe pia hakuna kitu cha maana wanachofanya.
SOURCE: MTANZANIA (Wabunge kikaongoni)