USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Tumeona michango yao. Ila kama uwakilishi upo, hakuna haja ya kuwa nao.
 
hii mimi bado napinga na kataa
kuna nini wamefanya, unategemea nini kutoka kwa mbunge kama viki kamata, mchungaji rwekatare kama
sio kwenda kula mafao tu, wiki end yeye ni askofu na baadhi siku za juma,
lado hajasimamia biashara zake za shule
mbaya zaidi wako wengi mno na tunapoteza pesa nyingi sana kwa huu upuzi wa viti maalum

Tumeona michango yao. Ila kama uwakilishi upo, hakuna haja ya kuwa nao.
 
Hata spika wa sasa si ni kiti maalum?
BTW: Kati ya ajira milioni 1 hizi 100 sio haba...!
 
Bravo Dr. Kashilila, pendekezo kila jimbo liwe na wabunge wawili mmoja mwanamke mwingine mwanaume. Kuhakikisha kila wakati wananchi wana uhakika wa kuwapo japo mwakilishi mmoja ndani ya Bunge, endapo mwingine atakuwa mgonjwa au ana majukumu ya kitaifa na kimataifa yanayoweza sababisha asiwepo ndani ya Bunge. Pili mmoja ashughulikie uwakilishi wa wananchi na matatizo yao. mwingine ashughulikie uratibu wa serikali, ahadi zake na uwajibikaji wa serikali kwa wananchi. Tatu tuwe na bunge Kuu la Seneti au House of Lords, litakalosimamia Sera za Nchi (Policy) na liwe lina Madaraka ya Juu kuliko Rais. Liteue Viongozi wakuu, Kama Wakuu wa Majeshi, Liidhinishe Mawaziri, Majaji, Mabalozi Govana wa Banki Kuu nk. Muundo wake ningependa upendekezwe na Wana JF.
 
Mimi sijawahi kuwaunga mkono hata mara moja. Wapiga kura wengi ni wanawake sasa kwa nini hawa wasiende majimboni?
 
Natumaini VITI MAALUM vitaondolewa na KATIBA MPYA. Kwa sasa sio rahisi kuviondoa kwa kuwa vyama vyote vyenye uwakilishi mzuri bungeni vinao hao watu. CHADEMA wao wameweka dada zao, binti zao, wakezao wa zamani, wafuasi wao, yaani! Aibu tupu.
 
wildcard shukurani kwa maoni yako mkuu
na lakini tukiongea vyama vya siasa nadhani ccm, ndio mwasiasa na
mwenye manufaa ya haya maviti kuliko chama chochote
katafiki yule MKONGWE Anna Abdallah ni Mke wa nan?
na mchungaji Getruda Rwakatare kapewa hiyo siti kwa kumwakilisha nani? wanawake au dini yake huyo naye ni ccm kumbuka?
je na viki kamata,
tafadhali njoo kwa hoja vinalenga kujenga taifa huwezi kuwalaumu CHADEMA kwa viti maalumu bila kuitaja ccm,
mbona siku hizi CHADEMA watu mnaihukumu kama chama TAWALA
chama ni chama pinzani ndugu, au ndi ile kusema kwamba CHADEMA ndio chama pekee safi kwa hiyo unajaribu kusema wale makini na katiba ya nchi iliyotengenezwa na ccm inaweza kuwachafua
kwa hilo nitakuelewa.
Natumaini VITI MAALUM vitaondolewa na KATIBA MPYA. Kwa sasa sio rahisi kuviondoa kwa kuwa vyama vyote vyenye uwakilishi mzuri bungeni vinao hao watu. CHADEMA wao wameweka dada zao, binti zao, wakezao wa zamani, wafuasi wao, yaani! Aibu tupu.
 
haya ndio matokeo ya matumizi mabaya ya PESA

NI jambo la fedheha na aibu isiyo kifani kwa Watanzania kwamba nchi yetu imeendelea kulemewa na madeni kiasi kwamba sasa hata vizazi vyetu vijavyo pia vitapaswa kulipa madeni hayo. Ni maisha ya kero na aibu kwamba familia nzima, yaani baba, mama, watoto na wajukuu kila mmoja anajikuta akiishi na mzigo wa madeni makubwa ambayo anatakiwa awalipe wadai wake.

Lakini maisha hayo ya udhalilishwaji yanazidishwa na kutiwa uchungu na ukweli kwamba madeni hayo ya familia hiyo yalikopwa na baba aliyedai anafanya hivyo kwa niaba ya familia, ingawa familia hiyo haikuhusishwa wala kutaarifiwa kwa namna yoyote katika suala hilo. Baya zaidi ni pale baba alipokopa fedha hizo na kuzitumia kufuatana na matakwa yake binafsi.

Ni katika muktadha huo, mzigo wa deni la taifa ambao umefikia zaidi ya Sh 10.5 trilioni na unaoendelea kuwaelemea Watanzania unapaswa kuangaliwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema katika ripoti yake ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 kuwa deni la taifa katika kipindi hicho liliongezeka kwa asilimia 38 kutoka Sh7.6 bilioni hadi Sh10.5 trilioni.

Hizi ni habari za kushtusha sana kwani kuongezeka kwa deni hilo ni pigo kubwa kwa wananchi kwa kuwa ndio walipaji wakubwa wa kodi mbalimbali licha ya wengi wao kuwa fukara. Ripoti hiyo ya CAG inazidi kuibua maswali kuliko majibu inaposema kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh2.8 trilioni.

Hali hiyo haitoi matumaini kwa ustawi wa taifa letu, kwa maana ya Serikali kujenga uchumi imara kwa kuhakikisha kuwa nchi yetu haitumii kuliko kile inachopata. Ndio maana tunataharuki ripoti hiyo ya CAG inaposema pia kuwa, katika kipindi hicho, Serikali iliongeza deni la nje kwa zaidi ya Sh2.5 trilioni, sawa na asilimia 44, huku deni la ndani likiongezeka kwa zaidi ya Sh521.2 bilioni, sawa na asilimia 23.

Tafsiri ya moja kwa moja ya hali hiyo ni kwamba, pamoja na Serikali kusheheni wataalamu wa uchumi wanaoishauri, ilikopa kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika taasisi mbalimbali za nje kuliko kiasi cha fedha kilichokopwa kutoka katika taasisi zetu hapa nchini. Kama CAG alivyosema katika ripoti hiyo, hii ina maana kuwa Serikali italazimika kuwalipa wadai wake walioko nje na hii kiuchumi ina maana kuwa kiasi kikubwa cha mtaji katika fedha za kigeni kitalipwa nje ya nchi.

Tunaungana na CAG kuishauri Serikali kwamba kwa kuwa uchumi wa nchi yetu umekua kwa asilimia 6.5 tu katika kipindi hicho, ni hatari kwa Serikali kuendelea kukopa pasipo kutilia maanani ukuaji wa hali ya uchumi wetu hasa kwa kutilia maanani kwamba CAG aligundua deni lisilotarajiwa ambapo wizara tisa na mikoa mitatu ilikopa Sh26 bilioni pasipo kuchukuliwa hatua. Madeni yasiyotarajiwa kama hayo ni mzigo kwa Serikali hasa pale yanapoiva na kutakiwa kulipwa.

Lakini jambo la kushangaza ni kuwa, wakati deni la taifa likizidi kukua kwa kiwango tulichotaja hapo juu, ripoti ya CAG inabaininisha kuwapo kwa mikopo isiyorejeshwa ya Sh424 bilioni katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la Sh7.6 bilioni, sawa na asilimia mbili kulinganisha na kipindi kilichotangulia cha mwaka 2008/9. Hii ni ishara mbaya kwa uchumi wetu, hasa ripoti ya CAG inaposisitiza kuwa madeni yamekaa bila kulipwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Sisi tunasema kuwa Serikali iuchukulie ushauri wa CAG kwa umuhimu mkubwa. Tunapendekeza kuwa mtindo wa kukopa pasipo kuzingatia vipaumbele vya taifa letu kiuchumi ukome na ubuniwe mchakato ambao utailazimisha Serikali kupitia kabla ya kutafuta mikopo kwa wafadhili na taasisi za fedha. Serikali isome alama za nyakati na kutambua kuwa wakati wa kukopa fedha na kuitumia itakavyo umepita
 
Thursday, May 5, 2011
Na Victor Makinda, Dar es Salaam




KATIBU wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashilila sasa ameingia rasmi katika malumbano na wabunge.


Kauli mfululizo za Dk. Kashilila dhidi ya wabunge zimezua malumbano ya jibu nikujibu baina yake na wabunge vijana.


Tukijikumbusha kidogo ni kwamba wabunge kutoka kambi ya Upinzani katika kikao cha tatu cha Bunge la 10 walisababisha hali ya sintofahamu ndani ya Ukumbi wa Bunge. Ni wakati ambao Bunge lilikuwa katika mjadala wa kuwapata wawakilishi wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament).


Katika mjadala huo uliojikita kuhusu kanuni za kuwapata wabunge wawakilishi katika Bunge la Afrika ndipo palipozuka hali ya tafrani. Hali hiyo ilizua mabishano kati ya wabunge wa upande mmoja waliokuwa wakipinga na wa upande mwingine waliokuwa wameikubali hoja. Kipande cha maneno ya majibizano yalikuwa hivi. Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (Chadema) ndiye aliyekuwa amesimama akitoa pendekezo nao wabunge wenzake wakadakia.


“Akanywe kikombe cha babu huyo…!”

“Futa kauli!”
“We vipi waambiwa huna masikio!”
“Jamani hatuko klabu tuko bungeni!”
“Out!out katuburuza huyo!!”
SPIKA: “Jamani naomba utulivu!!”
“Hatoki mtu nje!!”
“Tutatoka wote….!!!”
“Tufunge mlango tupigane!!…!!”
“Naona mnafanya mnada badala ya kuendelea na Bunge”
“Msitumie wingi wenu kutuburuza!!”
SPIKA: “Watu mmechaguliwa na kura za wananchi kwanini mnafanya mambo ya kitoto hivi hamjui kuwa tunaonwa na wananchi?”

Nataka kutoa picha kidogo ya nini kilijiri na kuzusha hali ya sintofahamu ndani ya Ukumbi wa Bunge na sasa sintofahamu hiyo imetanda nje ya ukumbi huo na kuzua mjadala miongoni mwa wanasiasa, wanadiplosia na wananchi mbalimbali.


Kabla ya kwenda mbali zaidi msomaji ni vema ukayatafakari maneno hayo hapo juu ya majibizano kati ya wabunge kwa wabunge na wabunge na spika. Sijui unapata picha gani.


Hawa ni wabunge wetu tuliowachagua kwa kura zetu kwa kuwaamini kuwa watakuwa ni watetezi wetu sisi wananchi katika masuala mbali mbali yanayotukabili.


Tuliwachagua kwa kuridhishwa na upeo wao wa mambo, umakini wao, utu na zaidi hekima na busara zao. Hawa ndio watunga sheria na kanuni ambao Katiba imewapa mamlaka hiyo. Kwa haya wayafanyayo tuna kila sababu ya kuhoji uwezo wao wa kufikiri na kujitambua.


Lengo ni kuchambua maudhui ya majibizano haya kati ya Katibu wa Bunge na wabunge ambayo yanaendelea sasa.


Kama ambavyo vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Dk. Kashilila. Mwanzoni mwa sakata hili Dk. Kashilila alisema kuwa tatizo kubwa la wabunge wa sasa ni ugeni na umbumbu wa kujua kanuni. Kwani wengi wao ndio wanaingia bungeni kwa mara ya kwanza.


Kauli hii ilijibiwa vikali na wabunge hawa wapya vijana. Baadhi ya wabunge vijana wamemtaka hata kuomba radhi kwa kauli yake hii.


Wengine wamejitanabaisha kuwa ni weledi wa sheria hata kufikia hatua ya kujitamba kuwa wanazijua sheria kuliko hata Spika. Malumbano ni makali.


Katika hatua hiyo ya jibu nikujibu (Malumbano) kati ya Dk. Kashilila ametoa kauli nyingine kali zaidi. Safari hii si kwa wabunge wageni tu bali kwa wabunge walio wengi ikijumuishwa wabunge wakongwe.


Anasema na kuwashutumu wabunge walio wengi kuwa tatizo lao wamekuwa wakiuza sura tu bungeni badala ya kutimiza wajibu wao kama wawakilishi wa wananchi.

Wajibu wa kuisimamia Serikali na kuwasilisha kero za wananchi na kuzifuatilia mpaka katika hatua ya utekelezaji.

Anakwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wabunge wengi ni wavivu wa kusoma na kudurusu nyaraka hali inayowafanya kushindwa kuibua hoja nzito enye maslahi kwa umma.


Ni kwa muda mrefu wapiga kura wa Tanzania wamekuwa wakilalamikia uwakilishi usiokidhi viwango wa wabunge ndani ya vikao vya Bunge. Wananchi katika majimbo tofauti wamekuwa wakilalamika kuwa kero zao sugu hazitatuliwi na Serikali na wala hawoni jitihada za wabunge wao kuziwasilisha serikalini kupitia Bunge.


Wapiga kura wanajiuliza nini wabunge wao wanafanya wakiwa ndani ya vikao vya Bunge? Maswali haya hutokana na ukimya mkubwa wa wabunge wengi ndani ya vikao vya Bunge. Wapo wabunge ambao unaweza kudhani kuwa hawapo. Kazi yao kubwa ni kupiga kofi na kuitikia ‘ndiyo’ na kisha kuwahi posho.


Yapo masuala mengi amabayo wananchi wamekuwa wakiyahoji. Suala la kutungwa kwa baadhi ya sheria ambazo ndani ya vipindi vifupi tu huonekana kuwa zimepitwa na wakati ni jambo jingine. Zipo sheria ambazo ni za ajabu kabisa ambazo zimetungwa na Bunge.


Kumbe sasa Dk. Kashilila ametufumbua macho na masikio. Tumefahamu sasa tatizo linalowakabili wabunge wengi ambalo linawasababishia ugoigoi wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.


Tatizo ni wabunge wetu hawa huwa ni wavivu wa kudurusu nyaraka na kuzisoma, kuzielewa na kujenga hoja.


Ukiwa mfuatiliaji wa vikao vya Bunge unaweza kubaini majina yanayojirudia rudia ya wabunge ambao huchangia mijadala mbali mbali bungeni. Katika Bunge la Tisa suala hili lilijidhihirisha wazi wazi. Kwani kuna majina ya baadhi tu ya wabunge ndiyo yaliyokuwa yakisiskika kila siku.


Kumbe sasa katibu wa Bunge anabainisha tatizo kubwa, lla wabunge wetu walio wengi ni uvivu wa kusoma kunakowanyima uelewa wa mijadala na kanuni.


Ukweli ni kwamba Watanzania tulio wengi ni wavivu wa kusoma. Si wabunge pekee. Katika kundi hili la wavivu wa kusoma wote tumo. Hivi karibuni nilihidhuria semina.


Katika semina hiyo iliyokuwa ikihusu masuala ya ujasiriamali na masoko watoa mada walitupatia machapisho mengi siku ya kwanza.

Kesho yake wakawa wakituuliza maswali yaliyotokana na machapisho waliotupatia.


Wengi wetu hatukuwa na majibu ya maswali yale. Hivyo ilidhihirika wazi kuwa hatukusoma machapisho tuliopatia.

Lakini kwa mbunge kuwa mvivu wa kusoma sheria kanuni na miswada ni angamizo kwa taifa. Kwani kwa kutofahamu kwa ukamilifu sheria na kanuni ndio kunakopelekea wabunge wengi kuwa mabubu au kuchangia kwa ubabaishaji. Ndiko kunakosababisha kutungwa kwa sheria kandamizi.


Kashilila amenena. Lakini pamoja na kusema kwake ukweli ni budi tukajiuliza kama kauli zake hazitasababisha hadhi ya Bunge na wabunge kushuka?


Hazitasababisha wananchi kuwa na mtazamo mbaya kwa wawakilishi wao? Je, ni kitu gani kimewasukuma kukimbilia bungeni ikiwa hawana dhamira ya dhati ya uwakilishi wa kweli? Kama ni kutetea maslahi ya wananchi je, watayateteaje ikiwa hawazisomi na kuzijua sheria na kanuni za Bunge?


Nionavyo wabunge wengi wamekimbilia bungeni kwa ajili ya kufuata maslahi tu. Wengi hawana dhamira ya kweli ya kuwawakilisha wananchi masikini wa taifa hili.


Tujuilize ni kweli mbunge mwenye uchungu na uwakilishi wa maendeleo ya wnanchi wake ana sababu gain ya kutozisoma kanuni za Bunge? Hicho kitabu cha kanuni za Bunge kina ukubwa gani hata kuwafanya wabunge wengi kuona udhia kukisoma?

Ni miezi sita sasa ya uhai wa Bunge hili la 10. Ni ajabu kwa mbunge kutozijua kanuni ndani ya kipindi cha miezi sita bungeni. Hapa kuna tatizo la maadili na la kiutendaji ambalo linawakabili wabunge wetu walio wengi. Ni vema sasa wakabadilika.

Watanzania sidhani kama watapenda kuona na kusikia malumbano haya baina ya wabunge na Katibu wa Bunge yanaendela kwani kuendeleza malumbano haya ni kushusha heshima ya Bunge na imani ya wananchi kwa chombo hiki muhimu cha uwakilishi.


Hoja nyingine nzito ya Dk. Kashilila, ametamka dhana ya uwakilishi wa wabunge wa viti maalumu. Kwa mtazamo wake wabunge hawa ni mzigo mzito kwa walipa kodi.

Ndiyo. Hata mimi pamoja na Watanzania wengi hili tumeliona.

Hapa ninaweza kutolea mfano mdogo.

Jimbo la Kilombero katika Bunge hili la 10 lina wabunge wanne wanaoliwakilisha. Yaani wabunge watatu wa viti maalumu na mbunge mmoja ni wa kuchaguliwa.

Hakuna cha maana wanachokifanya wabunge hawa licha ya wingi wao. Kilombero haijabadilika wala hakuna dalili za mabadiliko. Si mbunge wa kuchaguliwa wala wa viti maalumu wanaowakilisha matatizo ya wananchi bungeni. Kikao kilichopita wananchi wa Kilombero walishuhudia ububu wa wabunge wote wanne wanaoliwakilisha Jimbo la Kilombero.


Sasa hapa unaweza kujiuliza kwani wingi wa wabunge ni maendeleo?


Ukweli utababaki pale pale kuwa wabunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa na hawana kazi.

Nimalize kwa kutoa ushauri kwa wabunge wetu. Kwanza wafahamu kuwa wapo bungeni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya matumbo yao ndugu na jamaa zao.


Hivyo ni vema wakajituma kusoma kwa makini, kuelewa kanuni na kuibua hoja zenye tija kwa manufaa na maendeleo ya wananchi waliowatuma kuwawakilisha. Tutafakari pamoja!


victormakinda@yahoo.com
 
Je hakuna wanasheria wanaoweza kufungua kesi ya kikatiba kupinga viti maalumu?

Ni kweli kabisa huko wamejaa wauza sura tu, hata hawajui wanachokihitaji ndiko huko tumeambiwa viongozi wamejaza wapenzi wao na vimada, sura nyingine hata hujui zinamuwakilisha nani wakina vicky kamata wanaingia huko kwa kigezo kipi pamoja nayote hayo tunayoyasikia mtaani hivi bwana mkubwa hajui kutahayari?

Kuna na wengine wengi tu wengine wamejinunulia na u daktari wa heshima na tangu waingie bungeni hatujasikia wala kuona kitu, cha kuuzi ni pale wazee vikongwe kama wakina Anna Abdallah na Rita Mlaki waliotoka kwenye kuchaguliwa wamechuja bado wameng'ang'ania humo humo kwa kodi yangu mimi wanapewa magari ya anasa na kulipwa mafuta ya kutupa, umeme kwa kodi yangu shit nchi huu pumbavu kabisa wakati watoto wetu wanalala njaa na kuramba mavi usiku na mchana kwa kusomea chini kwenye shule za kata,hukusi kulazimisha mapinduzi kama yale ya egypt na kwingineko?

Haya ndio CCM wanayotaka tuyavumilie hatutaki
 
Inawezekana Kashilila ni mtumishi wa mapacha watatu?
mtanzania yoyote mwenye akili atakubaliana na hoja zote za msingi alizotoa dr kashila sio siri watanzania ni kama hatuna bunge kibaya zaidi wabunge wote wako pale bungeni kwa ajili ya kuwezeshwa na si vinginevyo
 
Nitangulie kwa kumpongeza daktari Kashilila kwa kuwatolea uvivu wabunge wengi mamluki, ambao wanatumia uelewa mdogo wa wapiga kura wao kama ngazi ya kupandia.

Aidha nimpongeza pia kwa ujasiri wake; maana kauli yake kwamba wabunge wa viti maalum, kwa kiwango kikubwa ni mzigo husiokuwa wa lazima inawakilisha hisia za watu wengi.

Pamoja na pongezi hizo natofautiana naye linapokuja suala la sintofahamu zilizotokea pale bungeni; Spika kwa makusudi kabisa alipindisha kanuni inayoongozi uteuzi wa wagombea uenyekiti wa bunge kwa maslahi yake, na hilo lilipohojiwa spika pamoja na wabunge wa CCM walijaribu kutumia wingi wao kupotosha hoja iliyokuwa mezani na ndipo wabunge wa CDM wakapinga kwa nguvu zao zote uburuzwaji huo.

Katika hali hiyo hakuna suala laugeni wala kutofahamu kanuni, bali kinachojitokeza hapa ni kwamba vijana hao pamoja na uchache wao wanazifahamu kanuni za bunge fika kiasi kwamba hawatakubali kuburuzwa.
 
Makupa hongera sana kwa kukubali kuwa mzalendo leo, japo umekubali kishingo upande, huku ukijaribu kuweka wabunge wote kapu moja
ila Hongera sana, kwa mwezi mmoja toka kujiunga naanza kuona mabadiliko,
JF ni jukwaa zuri sana, baada ya miezi miwili hoyo kazi yako utaacha na kuanza kuongea uhuru kama mtanzania
anyway hongera sana, MAKUPA

mtanzania yoyote mwenye akili atakubaliana na hoja zote za msingi alizotoa dr kashila sio siri watanzania ni kama hatuna bunge kibaya zaidi wabunge wote wako pale bungeni kwa ajili ya kuwezeshwa na si vinginevyo
 
Hata speaker hatambui uwezo wa viti maalumu alidhani wote pale bungeni wameingia na kura zetu wananchi, kumbe kuna wakina RWAKATARE na VIKI KAMATAwaliozomea na kupiga kelele za kichama chama ni wale hao maalumu
 
matokeo mengine ya matumizi makubwa kwenye utawala na siasa hi hayo hapo chini

The Citizen Reporter
Dar es Salaam. The International Monetary Fund (IMF) is concerned about Tanzania's increasing borrowing for recurrent spending. Presenting a report titled Regional Economic Outlook: Sub-Saharan Africa yesterday in Dar es Salaam, IMF senior resident representative John Wakeman-Linn urged the government to immediately review its fiscal policy to curb high debt levels taking into consideration the fact that food and fuel prices are rising and are likely to harm the economy.

"For the last five years, Tanzania has increasingly borrowed to finance recurrent expenditure while tax revenues have stagnated," he said. "Without a change in the fiscal policy, debt levels will rise rapidly." The government budget for 2010/2011 was Sh11.1 trillion. Of the amount Sh6 trillion was to be raised from domestic revenue and the rest from domestic loans and external grants and credit.

However, the IMF noted that it would be judicious for the government to hire more teachers, health care and agricultural workers.Economists and financial gurus are worried that increased government borrowing from commercial banks will have a "crowding out effect", meaning a reduction in private consumption or investment that occurs because of a rise in government spending.

This is the case because more government borrowing to finance its spending would increase interest rates, leading to a reduction in private investment. "I think there is a need for the government to tighten the expenditure discipline, and one way could be to re-introduce cash budgets. Otherwise, the increasing borrowing is really threatening the economy," Infotech chief executive officer Ali Mufuruki told The Citizen.

Meanwhile the IMF has lowered Tanzania's economic growth forecast by one per cent this year to six per cent due to rising food and fuel prices and problems of power generation, caused by delayed rains.

The IMF forecast growth in 2011 and 2012 to be 7.2 and 7.5 per cent respectively. But Mr Wakeman-Linn said yesterday that the continued power shortage and other global phenomena like high oil and food prices had prompted the fund to revise its economic forecast for Tanzania. "We anticipate a fall in activity early this year thus the growth is projected to be six per cent. However, solid growth prospects are projected for the years ahead if the recommended fiscal adjustments are made. "

He said the government might need to quickly seek immediate solutions to curb the increasing rising food and fuel prices, which are clearly having an impact on poverty, inflation, and would have an impact on GDP.

In its latest monetary policy statement, the Bank of Tanzania reported that it would cushion the economy from effects of higher crude oil prices and chronic energy shortages. It targeted the economy to grow at 7.1 per cent this year.

"The Bank of Tanzania will... take additional measures to curb the effects of the above cost-push factors on domestic prices, and ensure that the growth of monetary aggregates remains within targets for the year ending June 2011," noted the statement.

East Africa's second biggest economy grew by seven per cent in 2010, due to strong performance in agriculture, construction, manufacturing, transport, communications, fishing and real estate. However, analysts have warned that the economy faces some downside risks driven by the recent rises in global oil prices, high domestic electricity tariffs and power outages.

Although the situation has not reached alarming levels, they say urgent measures should be taken to check the situation.Such steps should include reducing oil taxes and coming up with a lasting solution to power problems.
The state-run Tanzania Electric Supply Company raised tariffs by 18.5 per cent in January, two months after it introduced power cuts, mainly because drought caused water levels to fall abysmally low at hydropower stations
 
Thursday, May 5, 2011
Na Victor Makinda, Dar es Salaam

“Futa kauli!”
“We vipi waambiwa huna masikio!”
“Jamani hatuko klabu tuko bungeni!”
“Out!out katuburuza huyo!!”
SPIKA: “Jamani naomba utulivu!!”
“Hatoki mtu nje!!”
“Tutatoka wote….!!!”
“Tufunge mlango tupigane!!…!!”
“Naona mnafanya mnada badala ya kuendelea na Bunge”
“Msitumie wingi wenu kutuburuza!!”
SPIKA: “Watu mmechaguliwa na kura za wananchi kwanini mnafanya mambo ya kitoto hivi hamjui kuwa tunaonwa na wananchi?”

Hao ndio viongozi wetu!
 
mkuu kwa ili tumpe pongezi kafanya uzalendo siko kuwa kama akina mkullo, wanaulivyo mambo ya ukweli wanajibu hizo ni story za mitaa hali kweli watu hawajalipwa.

Inawezekana Kashilila ni mtumishi wa mapacha watatu?
 
Dk. Kashilila aliwaponda wabunge wa viti maalumu akisema kundi hilo ni mzigo kwa taifa kwa kuwa hawana kazi wanayoifanya zaidi ya kukidhi maslahi ya kisiasa.

Dk. Kashilila alisema ni Tanzania pekee ndiyo yenye wabunge wa aina hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine zinazofuata mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola (Commonwealth).


Mtendaji huyo wa Bunge alihoji sababu za kuwepo kwa kundi hilo la wabunge, wakati wabunge wa majimbo wapo. Wabunge 102 kati ya wabunge 350 waliopo bungeni hivi sasa ni wabunge wa viti maalumu.


“Wabunge wa majimbo wapo 239, ndiyo kusema kwamba katika eneo lote la Tanzania hakuna eneo lisilokuwa na uwakilishi bungeni. Ukisema kila mbunge wa jimbo aende jimboni kwake, utakuta nchi yote ipo covered (ina wabunge).

“Sasa unajiuliza kama hivyo ndivyo hawa wabunge wa viti maalumu wa kazi gani
? Wanafanya kazi ipi special (maalumu) ambayo haifanywi na mbunge wa jimbo?” alihoji.

Alipoulizwa iwapo hoja yake hiyo inalenga kushauri wabunge wa viti maalumu wafutwe
, Dk Kashilila alisema: “ Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaiga affirmative policy ya Uingereza.

“Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.

“Kwa kufanya hivyo tutajikuta tumewaondoa hawa wabunge wa viti maalumu ambao kimsingi mimi sioni kazi wanayofanya na badala yake tutakuwa na wanawake bungeni, lakini wanaotokana na majimbo,” alisema.


Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge walitoa maoni tofauti kuhusiana na kauli hiyo, huku baadhi yao wakiipinga wazi wazi kauli hiyo.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) alimshangaa Dk. Kashilila kwa kutoa mashambulizi makali dhidi ya wabunge wa viti maalumu, huku akisema wabunge hao ni watu wenye mchango mkubwa kwa jamii.


“Hayo ni maoni yake, lakini kusema wabunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa mimi nadhani siyo sahihi. Wabunge wa viti maalumu wana mchango mkubwa kwa jamii na hata hao walioweka mfumo huu walijua wabunge wa viti maalumu wana mchango.

“Tunafanya shughuli nyingi za kijamii, tumekuwa tukisaidiana na wabunge wa majimbo katika mambo mbalimbali. Pale ambapo wabunge wa majimbo hawatimizi sisi tumekuwa tukiziba mapengo. Kwa hiyo si kweli kusema wabunge wa viti maalumu hawana kazi ya kufanya,” alisema



Maoni yangu:
tunapoteza zaidi ya bilioni 50 kwa miaka mitano kughalimia hawa wabunge wasio na tija kwa taifa wala kwa hao wanawake wanao wawakilisha nadhani tukifuata mfumo wa kiingereza kwa sababu tunafuta huo itakuwa makini zaidi, au kama vipi tuwe na utaratibu ambao wabunge wanatoka kajimboni tu na uwakilishi na ushawishi wao utaoneka wazi wazi, hizo pesa tunaweza kuzitumia kuleta maendeleo makubwa sana, na hawa wakuu wa mikoa na wilaya watolewe pia hakuna kitu cha maana wanachofanya.

SOURCE: MTANZANIA (
Wabunge kikaongoni)
Pia kungekuwa na utaratibu mwengine wa uwakilishi wa Wabunge kutoka Zanzibar.
 
Back
Top Bottom