Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni ukweli mtupu... Viti + Vitambi+ posho=.....Uzembe + usingizi
![]()
Komba alijitetea kwa kusema alizama kwenye maombi kuliombea bunge teh teh teh....Ni ukweli mtupu... Viti + Vitambi+ posho=.....Uzembe + usingizi
![]()
Habel Chidawali,Dodoma
MBUNGE wa Mbinga Magharibi John Komba (CCM) ametoa kali ya mwaka ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kusema kuwa katika moja ya vikao vya Bunge aliamua kuzama kwenye maombi ya kuliombea bunge ili liwe na upako.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki baada ya gazeti hili kwenye ukurasa wake wa mbele, toleo la Alhamisi kutoa picha yake akiwa ameegemea kiti huku akiwa amefunga macho na kuandamana na maelezo kwamba alikuwa akifuatilia kwa makini kikao cha mkutano wa pili wa Bunge.
Lakini Komba aliwaeleza wabunge kwamba gazeti hili lilimuonyesha akiwa kama amelala, lakini ukweli ni kwamba alikuwa anazungumza na Mungu akimtaka alishushie Bunge baraka ili mijadala iwe yenye busara kwa taifa.
Ingawa jana gazeti moja lilionyesha picha yangu kama nimelala, lakini mheshimiwa spika pale sikulala hata kidogo, isipokuwa nilikuwa katika maombi mazito ya kuliombea bunge pamoja na wabunge wa upinzani.
"Si unaona hata leo kiongozi wa upinzani bungeni ametoa maneno matamu alisema Komba na kusababisha ukumbi mzima wa bunge ulipuke kwa kicheko.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni Novemba 18 mwaka jana wakati akizindua bunge hili la kumi.
Kamba alishawishi wabunge waamini kuwa sala alizokuwa anafanya ndio zilizowezesha hata viongozi wa upinzani waliotoke nje kususia hotuba ya rais, wamsifie na kueleza wako tayari kushirikiana na chama chake.
Kabla ya Komba hajapewa nafasi ya kuchangia hotuba hiyo, kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alimpongeza Rais Kikwete na kusema kuwa Chadema kiko tayari kufanya kazi na CCM pamoja na kuwapa ushauri viongozi wa serikali pindi wanapokwama katika masuala mbalimbali.
Nampongeza Rais Kikwete kwamba amekuwa msikivu na hasa katika kuridhia suala la mabadiliko ya katiba kwa kuwa kumekuwepo na mapitio mengi yaliyoonyesha kuwa kumekuwepo na marekebisho mengi.
"Lakini yanaonyesha bado kuna nyufa katika katiba nampongeza sana rais katikia jambo hili alisema Mbowe.
Kauli ya mbowe iliwafurahisha wabunge wa CCM na kuhamasika kumshangilia kwa kugonga meza kama ilivyo kawaida yao katika kuonyesha furaha au kuunga mkono jambo.
Shangwe hizo zilitokana na ukweli kwamba walifurahia kiongozi huyo wa upinzani ambaye alikiongoza chama chake katika kushika msimamo kuwa hawamtambui Rais Kikwete, sasa wamebadili nia.
Komba alielezea kitendo hicho cha Mbowe kuwa kinaashiria Mungu ameshusha neema zake bungeni na kujenga umoja katika eneo hilo ambalo wabunge wapo kwenye mfarakano.
Kutokana na hali hiyo akasema inathibitisha kuwa hakua amelala kama watu wanavyoweza kutafsiri picha hiyo bali alikuwa kwenye maombi.
Nasisitiza tena kuwa maombi yale yalikuwa ni makubwa na mazito ambayo yalihitaji utulivu na mtu mwenye upako kweli na ndiyo maana na mimi nilitulia kikamilifu na Mungu ameonyesha jibu lake, tena kwa wakati wake," alisema na kuongeza:
"Kwa hiyo mheshimiwa spika hiyo ndiyo hali halisi na kwamba sikuwa katika usingizi sasa naomba kuendelea.
Wabunge wengi, waliiona picha hiyo na walihamasika kununua kwa wingi kopi za gazeti hili na wengi walikuwa wakiijadili na bila shaka ndiko kulikozua hisia tofauti ya namna mbunge huyo alivyokuwa akifuatilia kikao cha Bunge.
Katika kuchangia hotuba ya Rais Kikwete, Komba alijikita zaidi katika kutetea maslahi ya wavuvi.
Alisema kuwa wavuvi katika maeneo mengi hapa nchini wamekuwa wakionewa kwa kuchomea nyavu zao bila hata ya sababu za msingi.
Mbunge huyo alisema hata wanaoendesha harakati hizo wakidai wanapambana na wavuvi haramu, hawana uelewa wa kutosha kuhusu jambo hilo.
Komba alimtaka Waziri anayehusika na mambo ya vitoweo kuangalia uwezekano wa kuwapa elimu watumishi walio chini yake na kukomesha tabia hiyo.
Alisema maofisa wa uvuvi wanapaswa kufahamu kuwa kuna samaki ambao hata wakikaa zaidi ya mika 3 ua 4 hawawezi kukua hivyo wanahitaji kuvuliwa kwa kutumia nyavu ndogo.
Alitolea mfano wa dagaa ambazo alisema kuwa huwa umbo lao ni dogo haziwezi kukua zaidi.
Kutokana na kitendo hicho, akawataka maofisa wa uvuvi wanaoendesha kampeni za kuchoma nyavu hizo ambazo ni kwa ajili ya kuvua dagaa wakachome nyavu hizo zikiwa kwenye viwanda zinakotengenezwa.
Alisema hiyo ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuwaepusha wavuvi na uonevu wanaofanyiwa ambao hasara kwao na familia zao.
Mbunge huyo alizungumza mengi ikiwa ni pamoja na historia ya maisha yake.
Alisema katika kipindi cha masomo yake alishindwa kuendelea baada ya kufeli mtihani lakini akasema kuwa alitumia njia mbalimbali za kujinusuru hadi akafikia elimu ya juu na hivyo akawataka wanafunzi waliofeli mitihani wasikate tama
hivi huyu komb kwao hana kitanda,jamaa jing kweli,hiv wanayachaguaje mazembe kama haya,au kimenengule wawawa ndo iliwavutia.
Kwangu mimi ni mawili.
Matumizi ya rangi za bendera ya taifa kwenye carpet nadhani sio sahihi. Inakuwaje wabunge wanakanyaga bendera ya taifa? wao wapo juu ya sheria? kukosa heshma.
Tatizo lingine ni Interior decor. Sijui ni nani aliyechagua mpangilio wa rangi maana haziendani kabisa. Viti red, carpet - rangi ya bendera ya taifa. Yaani ndani kumekuwa kama x'mas tree! bad taste.
Dr Kashishila lazima ajue kuwa wanawake wanadai usawa na kama ndivyo hivyo wapigane majimboni kupata kuchaguliwa kama kina Kilango na Mdee. Hakuna kuwaachia kwani kwa kufanya hivyo nikuwaona wanawake ni dhaifu.Wafutwe c kupunguzwa hawana faida upupu mtupu
Kwa nchi zetu za africa wanawake bado wanadharaulika,mi naona ni jambo jema tu wanawake kupewa hivi viti maalum,ili na wao watoe mchango kwenye jamii, ila sasa malengo yanatumika vibaya sijui mchumba wa fulani, mama mkwe, marafiki.