USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Ndiyo maana hawakumbuki kuwa wanafunzi wanakaa chini na wananchi wanapata shida
 
Ni ukweli mtupu... Viti + Vitambi+ posho=.....Uzembe + usingizi
komba-auchapa-3.jpg
 
Ni ukweli mtupu... Viti + Vitambi+ posho=.....Uzembe + usingizi
komba-auchapa-3.jpg
Komba alijitetea kwa kusema alizama kwenye maombi kuliombea bunge teh teh teh....
Habel Chidawali,Dodoma
MBUNGE wa Mbinga Magharibi John Komba (CCM) ametoa kali ya mwaka ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kusema kuwa katika moja ya vikao vya Bunge aliamua kuzama kwenye maombi ya kuliombea bunge ili liwe na upako.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki baada ya gazeti hili kwenye ukurasa wake wa mbele, toleo la Alhamisi kutoa picha yake akiwa ameegemea kiti huku akiwa amefunga macho na kuandamana na maelezo kwamba alikuwa akifuatilia kwa makini kikao cha mkutano wa pili wa Bunge.

Lakini Komba aliwaeleza wabunge kwamba gazeti hili lilimuonyesha akiwa kama amelala, lakini ukweli ni kwamba alikuwa anazungumza na Mungu akimtaka alishushie Bunge baraka ili mijadala iwe yenye busara kwa taifa.

“Ingawa jana gazeti moja lilionyesha picha yangu kama nimelala, lakini mheshimiwa spika pale sikulala hata kidogo, isipokuwa nilikuwa katika maombi mazito ya kuliombea bunge pamoja na wabunge wa upinzani.

"Si unaona hata leo kiongozi wa upinzani bungeni ametoa maneno matamu” alisema Komba na kusababisha ukumbi mzima wa bunge ulipuke kwa kicheko.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni Novemba 18 mwaka jana wakati akizindua bunge hili la kumi.

Kamba alishawishi wabunge waamini kuwa sala alizokuwa anafanya ndio zilizowezesha hata viongozi wa upinzani waliotoke nje kususia hotuba ya rais, wamsifie na kueleza wako tayari kushirikiana na chama chake.

Kabla ya Komba hajapewa nafasi ya kuchangia hotuba hiyo, kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alimpongeza Rais Kikwete na kusema kuwa Chadema kiko tayari kufanya kazi na CCM pamoja na kuwapa ushauri viongozi wa serikali pindi wanapokwama katika masuala mbalimbali.

“Nampongeza Rais Kikwete kwamba amekuwa msikivu na hasa katika kuridhia suala la mabadiliko ya katiba kwa kuwa kumekuwepo na mapitio mengi yaliyoonyesha kuwa kumekuwepo na marekebisho mengi.

"Lakini yanaonyesha bado kuna nyufa katika katiba nampongeza sana rais katikia jambo hili” alisema Mbowe.

Kauli ya mbowe iliwafurahisha wabunge wa CCM na kuhamasika kumshangilia kwa kugonga meza kama ilivyo kawaida yao katika kuonyesha furaha au kuunga mkono jambo.

Shangwe hizo zilitokana na ukweli kwamba walifurahia kiongozi huyo wa upinzani ambaye alikiongoza chama chake katika kushika msimamo kuwa hawamtambui Rais Kikwete, sasa wamebadili nia.

Komba alielezea kitendo hicho cha Mbowe kuwa kinaashiria Mungu ameshusha neema zake bungeni na kujenga umoja katika eneo hilo ambalo wabunge wapo kwenye mfarakano.

Kutokana na hali hiyo akasema inathibitisha kuwa hakua amelala kama watu wanavyoweza kutafsiri picha hiyo bali alikuwa kwenye maombi.

“Nasisitiza tena kuwa maombi yale yalikuwa ni makubwa na mazito ambayo yalihitaji utulivu na mtu mwenye upako kweli na ndiyo maana na mimi nilitulia kikamilifu na Mungu ameonyesha jibu lake, tena kwa wakati wake," alisema na kuongeza:

"Kwa hiyo mheshimiwa spika hiyo ndiyo hali halisi na kwamba sikuwa katika usingizi sasa naomba kuendelea.”

Wabunge wengi, waliiona picha hiyo na walihamasika kununua kwa wingi kopi za gazeti hili na wengi walikuwa wakiijadili na bila shaka ndiko kulikozua hisia tofauti ya namna mbunge huyo alivyokuwa akifuatilia kikao cha Bunge.

Katika kuchangia hotuba ya Rais Kikwete, Komba alijikita zaidi katika kutetea maslahi ya wavuvi.

Alisema kuwa wavuvi katika maeneo mengi hapa nchini wamekuwa wakionewa kwa kuchomea nyavu zao bila hata ya sababu za msingi.

Mbunge huyo alisema hata wanaoendesha harakati hizo wakidai wanapambana na wavuvi haramu, hawana uelewa wa kutosha kuhusu jambo hilo.

Komba alimtaka Waziri anayehusika na mambo ya vitoweo kuangalia uwezekano wa kuwapa elimu watumishi walio chini yake na kukomesha tabia hiyo.

Alisema maofisa wa uvuvi wanapaswa kufahamu kuwa kuna samaki ambao hata wakikaa zaidi ya mika 3 ua 4 hawawezi kukua hivyo wanahitaji kuvuliwa kwa kutumia nyavu ndogo.

Alitolea mfano wa dagaa ambazo alisema kuwa huwa umbo lao ni dogo haziwezi kukua zaidi.

Kutokana na kitendo hicho, akawataka maofisa wa uvuvi wanaoendesha kampeni za kuchoma nyavu hizo ambazo ni kwa ajili ya kuvua dagaa wakachome nyavu hizo zikiwa kwenye viwanda zinakotengenezwa.

Alisema hiyo ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuwaepusha wavuvi na uonevu wanaofanyiwa ambao hasara kwao na familia zao.

Mbunge huyo alizungumza mengi ikiwa ni pamoja na historia ya maisha yake.

Alisema katika kipindi cha masomo yake alishindwa kuendelea baada ya kufeli mtihani lakini akasema kuwa alitumia njia mbalimbali za kujinusuru hadi akafikia elimu ya juu na hivyo akawataka wanafunzi waliofeli mitihani wasikate tama
 
Kila mmoja Ana kimada wake tatizo letu ni unafiki wanakula kodi yetu viti maalum wanamwakilisha nani wizi mtupu big up wabunge wanawake wenye majimbo viti maalum ni vimada watuambie wanamwkilisha nani ! Ni kupiga makofi tuu basi jamani Huo ndiyo ufisadi. Tutazidi kuwa masikini milele
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hivi huyu komb kwao hana kitanda,jamaa jing kweli,hiv wanayachaguaje mazembe kama haya,au kimenengule wawawa ndo iliwavutia.
 
hivi huyu komb kwao hana kitanda,jamaa jing kweli,hiv wanayachaguaje mazembe kama haya,au kimenengule wawawa ndo iliwavutia.

Wenye matatizo makubwa ni sisi wapiga kura,kwanini tuchague mtu tu,eti kwasababu anajulikana Dar,uwezo wa kutumikia wananchi hatutaki kujua..lazima tuvune mabua kwa kuwalea ngedere..
 
Kwangu mimi ni mawili.
Matumizi ya rangi za bendera ya taifa kwenye carpet nadhani sio sahihi. Inakuwaje wabunge wanakanyaga bendera ya taifa? wao wapo juu ya sheria? kukosa heshma.

Tatizo lingine ni Interior decor. Sijui ni nani aliyechagua mpangilio wa rangi maana haziendani kabisa. Viti red, carpet - rangi ya bendera ya taifa. Yaani ndani kumekuwa kama x'mas tree! bad taste.

Matumizi ya hivi vitu viwili yananiboa mno,hivi ni kweli tunakosa wachanganya rangi wazuri au ndio bora liende na kwenye bendera sehemu isiyotakiwa unaikuta inapohitajika haipo..
 
Wabunge viti maalum ni chanzo cha mogogoro ndani ya vyama vya siasa .
Ukiangalia namna wanavyopatikani utaona upendeleo wa ukabila, ukoo, undigu, na pengine wanawake wanadhalilishwa kwa kulazimika kufanya ngono na wenye mamlaka ya kuteua viti maalum

hii inapelekea wanawake hawa wawe watumwa na kuwa nyumba ndogo za wenye mamlaka
 
ni bora wapigwe chini kule bungeni kwenda kushindana kuvaa vimini na kupinga hoja za msingi kama kinondoni kuna wabunge wa viti maalum watano hata kazi yao cjui ni nn?
 
tuamgalieni nchi zilizo endelea eg. USA, UK, China mabunge yao hayana wabunge wengi kiasi kama hiki hata hao wanaochanguliwa kwa maoni yangu wapunguzwe maana ndani ya wilaya unakuta kunawabunge zaidi ya mmoja wanafanya nini? angalia nchi kama China ni nchi kubwa lakini idadi ya wabunge sio kama yetu nchi yenye zaidi ya watu 1.4billion na sisi tz 4.2 mill hatuna uwiano hatakidogo . huko chini kuna madiwani na wenyeviti wanatosha kuwakilisha 50billion sio mchezo zinaweza fanya kitu cha maana kabisa
 
Hawana cha maana wanachofanya zaidi ya kujaza ukumbi wa bunge tu.
Mara nyingi wametumiwa kama viburudisho vya waheshimiwa tu
Inakera sna kuona jambo hili likiendelea kuhusudiwa na hasa CCM
 
hii pesa unaweza kutumika kuleza maendeleo hapa nchi, hasa kwa kuwawezesha hakina mama kiuchumi kuliko hizi siasa za uongo na kweli
 
Wafutwe c kupunguzwa hawana faida upupu mtupu
Dr Kashishila lazima ajue kuwa wanawake wanadai usawa na kama ndivyo hivyo wapigane majimboni kupata kuchaguliwa kama kina Kilango na Mdee. Hakuna kuwaachia kwani kwa kufanya hivyo nikuwaona wanawake ni dhaifu.
 
Kwa nchi zetu za africa wanawake bado wanadharaulika,mi naona ni jambo jema tu wanawake kupewa hivi viti maalum,ili na wao watoe mchango kwenye jamii, ila sasa malengo yanatumika vibaya sijui mchumba wa fulani, mama mkwe, marafiki.

Mkuu kwa kuwekwa katika viti maalumu hii inaongeza dharau kwa wanawake, kwa nini wasisimame majimboni wakapambana! Mbona akina Makinda, Mdee na wengine wamesimama kupitia majimbo na wameshinda.
 
Back
Top Bottom