Viti maalumu ni nafasi ambazo ziliwekwa kwa mantiki ya kuziba mapengo ktk mfumo dume ili kuleta uwiano na uwakilishi sawa katika jamii. Kwa bahati mbaya sana nafasi hizo zimetumika vibaya kwa malengo potofu! Viti maalum imekuwa mzigo kwa sababu wengi wao hawakutumia vizuri nafasi hizo na ndio waliosababisha manung'uniko. Kwa kuwa imekuwa dili nafasi hizo zimeongezwa bila sababu za msingi. Kuna wakati viti maalum vilikuwa vikitolewa kitaifa, baadaye kimkoa, haikuwa mbaya kwa kila mkoa kuwa na mwakilishi mmoja wa viti maalum, lkn sasa kila mkoa wawakilishi 2 au zaidi! hapohapo kuna wawakilishi wa jumuiya kama vijana, wafanyakazi, NGOs, elimu ya juuetc! hapo ndipo ufisadi wa viti maalum unapojitokeza! Wanaochukuliwa hawana hata hizo NGOs, ni mjuano na uzandiki!
Nafasi hizo zingetumika vizuri zilikuwa zinaleta maana nzuri, but not now!