USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

hizo nafasi ni lazima ziendelee kuwapo bungeni kwa mtazamo wa chama cha magamba, hayo ni mapoozeo ya waheshimiwa sana wa magamba wawapo mjengoni.
<br />
<br />

Duh, we Khakha we! Sijui S. Simba anachungulia humu?
 
Balozi kasema vyema sana...viti maalumu ni kuzidi kumkandamiza mwanamke...tatizo hawawezi kukubali...wa kwanza kupinga ni walio madarakani...
 
hizo nafasi ni lazima ziendelee kuwapo bungeni kwa mtazamo wa chama cha magamba, hayo ni mapoozeo ya waheshimiwa sana wa magamba wawapo mjengoni.
ulikuwa na haja gani ya kuquote kwani ungetoa mchango tu isingetosha? Mnaudhi sana watu mnaoquote thread ndeefu. Mnatusumbua wenye mobile
 
Wanawake wa Kitanzania wanasubiria fadhila za mwanaume, halafu wanajiita wapambanaji wa haki za wanawake!!.
 
Kauli kama hii iliwahi kutolewa na Ananelea Nkya wa Tamwa mwaka jana, alishambuliwa sijapatya kuona. Hizo nafasi zomeshawaziba macho hawa waliozipata kiasi kuwa hawataki kabisa kusikia habari za kuzifuta... wameshaona kuwa ni haki yao kumbe zinawadhalilishwa na kuwatweza
 
Tunayasema haya Tangu zamani na hadi sasa ila afadhali amesema mtu wa nje pengine wataamka kutoka katika usingizi mzito. Viti maalum ni vya kufutwa na mzigo kwa sisi walipa kodi hatuvitaki. Kama wanataka kuwawezesha akina mama wawasaidie waweze kushinda kwenye majimbo watapata kujifunza na kuacha kuwa conflict interest zinazopelekea watu kuamini wanatumika kwa ajili ya sababu maalum. Viti maalum havifai na vinatugharimu gharama zisizo na msingi.
 
Jamani hizo si nafasi zamaawara zao? Magamba hawatakubali
 
Unajua hizi nafasi za viti maalumu zilianzishwa kwa nia nzuri nayo ni kuongezea uwakilishi bungeni makundi muhimu za jamii yetu ambazo zina uwakilishi pungufu kama wanawake, walemavu, vyama vya wafanyakazi nk. Tatizo ni kwamba viongozi wame abuse ni nzuri ya viti hivyo mpaka vime poteza maana kwa sababu havi tumiki kuongezea uwakilishi makundi muhimu ya jamii yetu bali kulipa fadhila mbali mbali. Kwa hali ya sasa no bora tu vifutwe.
 
wakatae viti maalum?? huyu balozi anacheza nini.. wakikataa dhahabu na ushungi kule bungeni atavaa nani?? steve wassira??

Wanajitahidi kutingisha masaburi wakati wa kampeni ili wapatiwe nafasi hizi!!. Mimi mke wangu akipewa hii nafasi, najua tayar kesha megwa na ntamwambia aende tu akaisha na huyo aliyemmega mimi basi!!!
 
wakatae viti maalum?? huyu balozi anacheza nini.. wakikataa dhahabu na ushungi kule bungeni atavaa nani?? steve wassira??
ha haaaa haaa...............nao wakubwa hawatakubali coz si unajua wengi wao hadi wapate hyo viti maalum wanakua ni chakula ya flani
 
Watasema Balozi anahubiri Umwagaji Damu! Ukweli kwa Magamba ni Kosa kubwa hadi unalaumiwa...
 
Wengi wanapenda Upendeleo, unadhani mtu kama Sophia Simba ataukataa huo ubunge wa bure? Miaka yoote ameishi Dar lakini bado ana inferiority kuwa hata weza kusimama jukwaani na kuomba kura kwa wananchi wa Dar; ni lazima apate upendeleo toka kwa wakubwa.

Anangalia anavyoiendesha UWT au alivyomwekea mkwara Justine Mhagama jina lake kukatwa wakati wa kugombea Uspika.

Wanawake wengi Ndani ya CCM ni hivyo wanaishi wa Mapendeleo; hawatasema hapana
 
Kuna umuhimu katika mchakato wa katiba mpya kujadili kama wananchi wanahitaji uwepo wa viti maalum au laa,kwangu binafsi naona imefika wakat sasa wanawake wanaweza kusimama wenyewe na kugombania nafai mbali mbali hvyo hamna haja ya kuwepo kwa viti maaluum na badala yake hizo pesa wanazolipwa hao wabunge wa viti maalum zingepelekwa kwenye sekta ya ilimu kwa kuongeza mishahara ya walimu.ni jamii ilioelimika tu ndo itakayoona umuhimu wa mwanamke na sio kwa kuwapa nafasi ya upendeleo kama hyo ya viti maalum
 
Mimi mwenyewe sioni umuhimu wa viti maalumu hebu tupige hesabu ndogo tuseme kuna wabunge wa viti maalumu 100'mshahara wao+posho+malupulupu tuseme milioni 5 per month'
so kwa mwezi mmoja milioni 500 tsh kwa mwaka bilion 6 tsh'kwa miaka mitano 30 bilioni tsh'kuna ile sheria wakimaliza ubunge kila mp anapewa 50 milion tsh kwa total ya wote bilion 5 tsh tukiweka na mambo mengne unakuta inafika hata bilioni 40 tsh.
Hz ela zingetupeleka mbali sana'
 
Back
Top Bottom