SHILINDE,
1: Hii ni MIZIGO isiyo ya lazima. Kwani hawa wanawakilisha JIMBO GANI ikiwa wananchi wote wa jimbo fulani wanamchagua mwakilishi wao kwa kupiga kura?
2: Na je, kama ni mtu anafkiri waende basi kuwakilisha mbona hawaletwi kwa kundi wanalodaiwa kuwakilisha afu kundi hilo liseme kama linamkubali au laaa?
3: Hivi wa nyie mnaopewa izo nafasi bila kutoka jasho mnajiskia je kulipwa mamilioni kutokana na kodi za wavuja jasho nikiwemo mimi, wanaoteseka kwa mishahara ya TGSD?
4: Watu hamna udhaifu wowote wa viungo mnaitwa mnawakilisha "KUNDI MAALUM" what kind of maalum is this? Mbona sioni wanaume wanaowakilisha makundi maalum? Hakuna wanaume wenye wanaohitaji huo uwakilishi maalum?
5: Nafkiri huu umaalum huenda ni KA_MRIJA kalikobuniwa kumkaba zaidi mtu wa chini maana mi SIONI HAJA Ya wao kuwepo hali wabunge walopigiwa kura wapo, hawajashindwa kazi. Ni muda sasa na ni busara UMAALUM UACHWE ili hizo fedha zihudumie wananchi wa wanaowakilishwa na wabunge halali.
6: Afu inabidi tujifunze kwa wenzetu wa Afrika mashariki. Mi naona wenzetu wana mabunge madogo na wana MAENDELEO af wa TZ maskini af MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA yako juu... This is senceless...
Mwisho kwa apa, kama wewe ni MTANZANIA unaeumia kuona nchi yako haisongi mbele miaka nenda rudi, chukua hatua ya kupinga "VITI MAALUM"