Ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima: Ukivuliwa nguo, ukabaki utupu! Ustaarabu ni kuchutama!


Mkuu Pascal: Nani kavuliwa nguo hasa? Rais kashindwa kabisa kupangua hoja! Na ameleta maswali mengi mno. Tukubali Serikali imekuwa na kama wiki mbili ngumu hivi karibuni, na yote ni kauli za Rais.

Angekaa kimya kwa hili Rais na kuonyesha amempuuza Gwajima mengi yasingezungumzwa. Hebu angalia swala la wanaharakati kutoka Kenya, hili lilikuwa sana sana la Mkurugenzi wa Uhamiaji, mbona nchi hii imerudisha watu wengi makwao! Kuna kuwapa masaa 12 au 48, na kuna kuwarudishia mipakani, na pia kuwapeleka Mahakamani. Lakini kuwarudisha kwa kuwapiga, na halafu Rais anatoka kwenye Kadamnasi bila aibu na kulizungumzia, hii inafikirisha sana Mkuu, inaonekana kuongoza nchi kwa kufuata utawala wa Sheria ni ngumu mno! Na ugonjwa huu unaanzia ofisi kuu ya nchi!

Kwa kifupi ni Serikali ndio inabidi ichutame!
 
Gwajima hana makosa.
Yeye amesema tu watu wanatekwa na yeye anaona huruma sana.
Lakini yote inategemea atasema nini atakapohubiri Kanisani.
Gwajima ,kwa maoni yangu, ni kama Mchungaji Mtikila, a lot of zeal to help people but little ability.
 
Ndio yule mtu alikuwa anatoa tahadhari kwa Gwajima jana.
Anasema huyu Gwajima ni shupavu sana anapoponga uovu,watu wanamsifia.
Gwajima anawafufua wafu.
Lakini Gwajima has no Doctrine.
Wananchi wa kawaida wanahitaji Doctrine so that they may be able to stay on the correct side of the Prison Bars .
 
Afadhali ya hii kidogo umeificha japo bado umeendelea kumuita mwenyekiti wa chama Chako kichaa,
Kuwa makini pasko kumbuka wasiojulikana wapo!
 
Nasemaje , ipo mambo huku .....

Japonica mimi binafsi namjua gwajima kama mpinzani na nilishangaa alipochukua fomu CCM.

So hangeweza kunasa na biti LA CCM.
CCM hata kama Kuna makosa yapo wanachama hutakiwa kuonyana na kushauriana kwenye Vikao vya ndani.
 
Wewe ni mtu mzma, acha ujinga na uchawa
 
Uzuri alisharudi kutoa ufafanuzi kwamba "Silaha ya mjinga ni kujipendekeza" sababu hana anachojua kwahio hujipendekeza kwa watu flani flani ili kuficha udhaifu huo.

Kujipendekeza==UCHAWA
 
Usishindane na Serikali.
Serikali ni dude kubwa, keep my words.
Hakuna anayeshindana na serikali, tumia akili japo kwa 1% tu.

Mbunge kazi yake ni ku raise concerns on behalf of raia na kuihoji serikali imefanya nini ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa bila raia kunung'unika.

Hio ndio sole purpose ya wabunge wote 200+ waliojazana pale mjengoni ila cha ajabu wabunge almost 90% wametugeuka raia na kuanza kutetea maslahi ya serikali kupitia falsafa ya uchawa.

Wako wabunge wasiozidi watatu ambao wanaweza kutoa hoja dhidi ya serikali the rest ni stupid raving bonkers. Watu walioahirisha kufikiri kwa usahihi ilimradi tu wapate ujiko serikalini.
 
Mayalla mbona unazingua sana aisee.
Yaani kati ya Gwajima na Serikali nani kavuliwa nguo???
Halafu mbona mnataka nchi iende kikondoo hii: hata Wagriki na Wa-roma founders wa Demokrasia walikua wanakaa kwenye mabaraza, wanabishana na kujibishana - ndo raha ya demokrasia.
Mnataka waTz waishije aisee, wote tujae Dodoma na nguo za kijani tuseme Ndio Mama??
 
Uoga huzaa dhambi......
Gwaji lazima apewe maua yake. Kama nchi nzima mkikataa kuchutama, haki na usawa utapatikana. Kwenye mapambano lazima mmoja mmoja halafu sauti zitatoka tu. Gwajima awaunge Chadema Ili sauti yake iweze kusikika
 
[emoji57][emoji57][emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…