Ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima: Ukivuliwa nguo, ukabaki utupu! Ustaarabu ni kuchutama!

Mkuu kwanza pole na maswahibu yale uliyopitia kulingana na mahojiano yako, ila kwamasikitiko sana with all due respect mkuu unaonekana huja recover bado honest kabisa,sasa hapo aliepaswa kuchutama ni nani? Hebu tueleze kidadavuzi kosa la Gwajima ni lipi? Tunakubaliana kabisa Gwaji ni mmoja wa watu wa hovyo tulionao lakini haiondoi ukweli kua alischokisema sio kitu cha hovyo hata kidogo ni mtetea maslahi pekee ndio atapingana na Gwaji, Je mlitaka atoe mfano wa nani juu ya kupotea? Mbona viongozi wakigusiwa kuhusu kupotea watu wanatoa mifano ile watu walioenda kwa waganga huko hatusikii mkitoa milio hawawagusi walengwa husika? Au wewe binafsi unafurahishwa na mambo haya mkuu unaona sawa na unaona wewe uko salama kwakua ni mwanasisiemu? Mkuu huo ndio uzalendo manaohubiri kwa Taifa letu? Vifo nakupotea kwa watu wanaowakosoa mnaona ni sahihi kwaajili ya maslahi yenu? Taifa mnadhani mna haki miliki yakufanya lolote? Mwisho wa siku sote njia yetu ni moja na Mungu hadhihakiwi
Mika 6:8
*"Bwana amekuambia ni nini kizuri, na anachotaka kwako ni hiki: kutenda haki, kupenda fadhili, na kutembea kwa unyofu na Mungu wako.
Qur’an 49:9
"Ikiwa makundi mawili ya Waumini yanapigana, basi yapatanishi kati yao. Ikiwa kundi moja linadhulumu lingine, basi mpiganeni na lile linalodhulumu."

. Hadith ya Nabii (S.A.W)
"Mwenye kuyakumbatia miongoni mwenu uovu, anapaswa kuubadilisha kwa mkono wake (kiungu); kama hana uwezo, basi kwa lugha yake; na kama hana uwezo, basi kwa moyo wake – na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi."*
(Sahih Muslim – inasisitiza wajibu wa kila mtu kupinga uovu kwa njia anayoweza.

Efeso 5:11
"Wala msiushirikiane katika matendo ya giza yasiyo na matunda; bali, msiwaadhibu."
(Wakristu wanatakiwa kukataa na kukemea mambo ya uovu.)

Sasa Mkuu kama dini zote zinakataa uovu nyie ni nani hadi muone anaepinga Uovu amefanya makosa? Muda utaongea na kila mtu atalipia uovu wake mbele za Mungu.
 
huo mfano wa kichaa kuchukua nguo ulishapitwa na wakati, akichukua nguo si nachukua simu napiga naletewa nguo zingine?? alafu naendelea kuogelea tuu kama kawaida.??

unmashauri gwajima asijibu wakati tayari wamemkata jina lake jimbo la kawe??

ushauri wako wa ovyo sana
 
Wewe jamaa njaa itakuua
 

Hivi una maana gani....

Na kauli yoyote inayotolewa na yeyote kwa qgenda ya kukemea utekaji huku ikiamsha hisia za chuuki, taharuki na vurugu ndani ya jamii yetu haikubaliki zaidi.

Una maana gani hasa....."Kuteka watu watu kumeamsha chuki tayari" Sio kumeamshwa na kuukemea Mama D HATA AKILI ZA KUFIKIRI TU ZINAANZA KUWASHINDA!
 
PASCAL tumekuelewa wakubwa wenzio pole sana kwa awa ambao awajakuelewa ujumbe wako au nasaa yako kwandugu yako Gwajima !
 

Kinachosikitisha zaidi kwa Mayala, kasoma na sheria pia! Hata kama tuna ratiba kiraka, bado inatambua haki za raia! Safari ya Watanzania ni ndefu na ngumu mno!
 
Kayika majitu matchplay,ni hili jamaa.
Unazeeka vibaya mzee baba.
Gwajima sio level yako.
Bibi yako na serikali yake mbovu ndo wachutame.

Uchawa utakuuwa mbweha wewe.
Gwajima
 
Mwanaume ameumbwa Kupambana Kuchutama Hioo Kaumbiwa Mwanamke, Na Kwenye Maisha Simamia Haki Ilipo, AHADI ALIZOWAPA HIZO ELA ZA KUTEKELEZA ANATOA SEREKALINI?
 
Nilipokuwa mdogo miaka ya 90 kuna vichaa nilikuwa nakutana nao wenye umri kati ya miaka 30 hivi, nikajiuliza je huwa hawazeeki?
Kumbe na vichaa nao wanazeeka
 
Ninge shauri achutame tu,unapo dili na watu wenye 'machinery ' za kuua na sio rational thinker busara ni kukaa kimya.
 
Wewe jamaa ni mnafiq sana. Ile kutolewa kejeli na Samia ndiyo kuvuliwa nguo? Mimi naona Gwajima ndiye ameivua nguo taasisi ya Urais kwa kusema ukweli ambao wote wenye akili wanaujua lakini hakuwepo mwenye ujasiri wa kuusema hadharani. Aliyetakiwa kuchutuma ni Rais,angekaa kimya na kuzifanyia kazi changamoto alizotaja Gwajima.
 
Gwajima hajavuliwa nguo, aliyevuliwa nguo ni Serikali dhalimu ya ccm ilyojaa vitendo haramu vya kishetani, Polisiccm kwa kutumwa na Bishungwa wakambaka binti wa Uganda na kuwapiga wakenya, matokeo yake wakenya wakaingia kwenye mitandao ya Serikali ya ccm na kuwavua nguo zote kuanika siri zao kuhamisha pesa zao nyingi, huku vijana wa kenya wakimtukana matusi mama yako mayala, na siri za IGP kumiliki mabilioni kuanikwa, na kama siyo ibirisi mashetani wa huko ccm kumshauri mama kufanya uonevu maovu manyanyaso kwa chadema haya yasingekuwepo leo, Nchi ingekuwa na Amani pasipo utekaji wenu na akina Abas Tarimba Msukuma na chawaccm kwa msaada wa Polisiccm
 
Niko njiani naenda Kanisani kwake, leo naenda kumchochea poti wangu tuliamshe DUDE hawawezi kutuzodoa kwenye mikutano yao halafu sisi tunyamaze! Ila ng'wanangwa na wewe umezidi kujikomba wewe ndiye ulisemwa na poti wangu kwamba mnajipendekeza kwa sababu hamna uwezo wa kujitegemea! Amevuliwa nguo au yeye ndiye kawavua nguo? Na mimi nakwambia kama wakiwa wawili kwenye ulingo wa siasa haki ya nani kura yangu nampa Gwajima! Yule maza ni takataka!
 

Mama D: Hivi ungekaa kimya kwa hili ungedhurika Mama.....?
 
Sawa . Tupe majibu sasa anaewateka watanzania wenzetu na kuwapoteza ni nani? Na je kwanini serikali ipo kimya na imeshindwa kushughulikia huu mzimu wa utekaji? Hoja ya Bishop Gwajima ipo hapa hayo mengine tutayatafutia muda tuyajadili.
Watekaji ni msukuma, Abas Tarimba pascal mayala, Amos makada, chawaccm na Polisiccm
 
Kaka wewe sio paschal mayala yule nae kujua tokea zama jamboforum umekuaje siku hizi?ushauri wako ni mzuri ila naona kama umechelewa.
 
Gwajima karusha jiwe kwenye kichaka cha ibirisi ndipo mashetani wote wamejitokeza sasa kila mtanzania kawabaini watesi watekaji waonevu wote chawaccm
 

Kavuliwa nguo au yeye ndiye kamvua mtu.....!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…