Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

kwani huu muungano una faida gani hasa pasco??
 
Huyu Paskali uzee unamjia vibaya.
 
Ushauri wako ni wa bure lakini ni wa hovyo!
 
Kaka Paskali, unataka maoni yako ya kumfukuza Bwana Othman yafanyiwe kazi...!! Lakini unataka maoni ya Othman yamfukuzishe kazi..!! Hutendi haki.
Mkuu Ngali, Ngalikihinja, kwanza naomba kujitanabaisha kuwa mimi ni miongoni mwa watetezi wakuu wa freedom of expression, hivyo ushauri huu usitafasiriwe kuwa ni kuingilia freedom of expression ya OMO, no!.
Kuna baadhi ya nafasi za juu za uongozi kwenye ngazi za maamuzi, kiongozi huwezi kutoa maoni kinzani.

Uongozi wa serikali ni kama ndoa, wana ndoa wanafungwa na kanuni ya a collective responsibility. Hata ikitokea wanandoa wamehitilafiana, watoto hawapaswi kujua, au ikitokea mzee ni hakuna kitu, mama hawezi kutangaza public na kusema no anatoa maoni yake.

Wabunge wa ACT walio ndani ya serikali ya GNU ya Zanzibar, ni wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM yenye lengo la kuimarisha muungano.

Hivyo viongozi wote wa GNU wanabanwa na kanuni ya a collective responsibility kudumisha muungano
Hivi kwanini mtu akitoa maoni yanayokinzana na watawala anatakiwa afanyiwe jambo baya?.
Hapa ukinipa mifano, nitakushukuru. A collective responsibility inataka kama hukubaliani, unanyamaza kimya, na ukiamua kuongea, ondoka kwanza ndani ya serikali ndipo upinge.
Mnataka taifa la NDIYO MZEE? Kwanini hoja zake zisijibiwe kwa hoja zenye nguvu zaidi?
Hapana, tunataka viongozi waadilifu, maadam umekubali kuingia kwenye ndoa, ni lazima utimize masherti ya ndoa ikiwemo kutimiza wajibu wa ndoa.
P.
 
Wewe jamaa ni mchochezi na mgombanishi mkubwa.
 
Jifunze Kenya, Uhuru na Ruto.
 
OMO aambiwe ukweli. Akubali au akatae. Asiwe wa vugu vugu. Halafu Wazanzibar tumewakaribisha wamiliki na ardhi manake wazee wetu waliachia territorial resources zetu ziwe za Muungano. Nini maana ya kuachia sovereignty kwa ajili ya Muungano? Lakini wao hilo hawataki.
Na Je, inawezekana mtu kutoka Babati(mzaliwa) kwenda kuwa Rais wa Zanzibar?
Tamaa itawatumbukiza shimoni.
 
Kuufuta muungano sio kupingana na watawala bali ni Uhaini.
 
Pascal nadhan una hoja ya msingi..Mimi sielewi kwa wanaotaka kuuvunja muungano wanawafikiriaje wazanzibar wanaoishi bara, ambao wameolewa, wanafanya kazi, wanalima, wanafanya biashara kubwakubwa....wanawafikiraje...????hivi wanajua maana ya kutengana..kutengana hakuna mswalie mtume shekh.....watu nahisi wamechoka amani...
 

Usisubiri Mwinyi kumfukuza Othman Masoud,Omo alitaka kujiuzulu wakati wa sakata la wizi wa kura kwa Mbunge wa Konde,,Mwinyi kamkatalia

OMO,hajaongea chochote kibaya,alichoongea ni maoni ya Wazanzibari walio wengi...

Kama kila mtu anaezungumza kile anachokiamini na kukikubali afukuzwe kazi basi Watanganyika pamoja na Wazanzibari watakuwa wanafuata upepo na kukubali kila kitu kinachofanywa na kusemwa na Wanasiasa..

Watanzania tunataka kuondokana katika hali ya kuwa watumwa wa kuwaza na kufikiri,hatutaki kurudi katika zama Hewala bwana..,ndio mzee,..nk..

Tunataka democrasia ya kweli,tunataka uhuru wa kujieleza,wa kuamua,wa kuhoji,wa kifikri nk..

Hatutaki kuishi kwa woga,kwa kujificha,maisha ni mfupi sana,acha tuishi kwa kujiamini,na kuamua tunachotaka

Muungano hauna faida kwa Zanzibar,Muungano unarejesha nyuma Zanzibar,Wazanzibari walio wengi hawaitaki,ukweli ndio huo

Nchi iliyokuwa Empire,yenye lugha yake,dini yake,utamaduni wake,ustarabu wake,uchumi wake,nchi iliyokuwa ikitoa misaada kwa nchi nyegine,hivi sasa haiwezi kuomba misaada mpaka ipewe ruhusa..,wtf
 
Mawakala wa Muungano ndio wanaoifanya Zanzibar iingie kwenye siasa za ovyo, .

Mkwamo wa kisiasa Zanzibar unasababishwa na Muungano,kabla ya Seif Sharif na Amani karume hawajakaa na kukubaliana kuleta muafaka katika siasa za Zanzibar

kamati kibao za kutuliza hali mbaya ya kisiasa Zanzibar ziliundwa,lakini hakuna hata moja iliyoleta matunda..

Utulivu wa kisiasa ulikuja pale Maalim na Karume walivyokaa kivyao bila ya kamati zilizoundwa na Serikali ya Mungano..

Divide and rule ndio njama zinazotumiwa na kamati zinazoundwa na serikali ya Muungano ili kuidumaza ZANZIBAR,wazanzibari wamelijua hilo
 
Wewe Mlugaluga unajuaje maoni ya wazanzibari? Je kama hayo maoni ya OMO pia ni maoni ya baadhi ya wanaCCM wengine wa Zanzibar (Salmin Amour type) wanamtumia yeye kufikisha ujumbe...

Ndani ya CCM sio kwamba wote wanakubali mambo yalivyo, nao wafukuzwe?
 
Pascal Mayalla Saa zengine ujitazame, usijifanye una akili na maarifa makubwa kupita kiasi.

Kuna umwehu kichwani kwako ujitazame na kujihakiki vyema. Unafahamu athari ya kisiasa itakayotokea kwa Othman kufutwa kazi katika uingozi wa Hussein.

WAZANZIBARI WANA AJENDA YAO, CCM HAWANA AJENDA WAPO KIMASLAHI ZAIDI, NA CCM SIO WAZANZIBARI ILA BAADHI YA WZAZANZIBARI WAMO NDANI YA CCM.

USIMPANGIE.
 
Kwani hapo Bara hakuna Wakenya,Waganda,Wanaigeria nk,wanaoishi hapo,walioowa hapo?wanaofanya biashara kubwa kubwa hapo?

Hayo ni mawazo mgando,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…