Uchaguzi 2020 Ushauri wa bure kwa John Mnyika kuhusu mzabuni wa NEC

Uchaguzi 2020 Ushauri wa bure kwa John Mnyika kuhusu mzabuni wa NEC

Hoja yako ni ya kipuuzi.

Ununuzi wa karatasi za kupigia kura siyo sawa na ununuzi wa vifaa vya chama. Unalinganisha visivyolinganishika. Sijui kwa nini watetezi wa Tume, CCM au Serikali, mara nyingi, huonekana au ni watu wenye uelewa mdogo au watu wanaojifanya ni wajinga.

Ununuzi wa karatasi za kupigia kura, unatakiwa kuonesha uwazi kwa wadau wote ili kujenga imani. Na ndivyo inavyofanyika Duniani kote, na ndivyo ilivyokuwa ikifanyika miaka yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ndo unaamka sa hizi watu washaona picha za Dodoma na ikungi ni balaa tupu,mpaka yehodaya akasema hakuna kijiji chenye watu wengi namna hiyo.

Au ndo unatoka kazini kwa wahindi sa hizi.
Hali ilivyo, hata kama anatoka kazini kwa waChina au waAfrica au kwa mtu wa asili yoyote ile, mradi ana kazi...kwani wako wengi sana leo hii hawana kazi kwa muda mrefu sana...
 
Hakuna chama cha hovyo kabisa kama CHADEMA. Wameona maji yamewakaba kooni sasa wanaleta visingizio. Tulieni dawa ikolee, mnarukaruka nini..
Nakubaliana na wewe kabisa. Wakati huu wa lala salama ungetegemea Chama kinachotaka kuchukua dola kingejikita katika kueleza kitawafanyia nini Watanzania pindi wakipewa ridhaa. Lakini kwa sababu hawana sera ndiyo wanashika mabua; watazama tuu majini maana wamesishatoboa mtumbwi wao kwa kusema uongo uliotukuka. Eti maendeleo ya watu hayawezi kuletwa na maendeleo ya vitu!!!! SGR, Umeme, barabara, flyovers, hospitali, n.k. haziwezi kuleta maendeleo ya watu!! SHAME ON YOU. HATUDANGANYIKI. Jiulize huyu Mnyika kwa muda wote alikua kimya; sasa anaibuka na sera ya karatasi!! Tujiulize jee walikuwa na mchezo mchafu na hizo karatasi waliotega na sasa umefeli??? Jambo la kumsifu Mnyika ni moja tuu. Alijitoa kutetea jimbo lake baada ya kuona mwaka huu asingeshinda. Hongera kwa hilo.
 
Umetumwa na Jamana au mahera??? Tuanzie hapo Kwanza, Acha upumbavu!
 
Nguli wa sheria anasema uongo na kufungiwa kampeni?
Huyo ni boya tu,

Hebu leteni mafuriko ya leo tuone ukame wa watu waliokuwa na hamu na mgombea
Nimeingia youtube mida yote sioni kitu nini shida?

Au warusha pivha nao bado wako jela ya NEC?

Tunataka picha hatutaki uinga ujinga, mbona za kanza ya ziwa mlikuwa mnawahisha?

Za huko nyumbani kwake, kwa nini mnachelewa kutoa?
Picha na video zote anazo Yehodaya muulize atakutumia, pombe za kununuliwa zitakupoteza jiangalie Sana bwana mdogo
 
Huyo Kigogo toka aanze kuanika uchafu wenu kuna siku mmewahi kumjibu? zaidi mnahangaika tu kumtafuta yeye binafsi, jibuni kila anachokielekeza kwenu msihangaike na mtu.
Hakuna anayehangaika na huyo taahira. Watanzania wanachapa kazi na maendeleo yanaonekana. Hata yule pimbi aliyepata ajali juzi anashukuru kwa miundo mbinu imara na sasa yuko kitandani. Yale yote aliyopanga yamekwenda na maji na ndio kwanza kunapambazuka.
 
Makini sana kiongozi, hawa CHADEMA kiufupi wamepwaya sana. Ni hopeless kabisa, samahani kwa hii lughasina namna. Wanadandia hoja hovyo.

Kifo cha nyani miti yote huteleza
Hii ndiyo picha ya watu wenye damu ya kijani na waliokunywa maji ya kijani.
 
Ethiopia kuna kilakitu ila kila leo raia wanakimbia nchi yao hujiulizi shida ipo wapi, hiyo cm na bundle viwe zinakusaidia kusoma baadhi ya vitu mtandaoni na sio kuisifia tu ccm, na hayo mavitu yanajengwa huku kodi vikiwa kubwa balaa saizi kusafirisha tu mazao kutoka mkoa mmoja hadi mwingine ni shughuli haswa
 
Nimefuatilia Press ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. John John Mnyika, akiitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusisha vyama vya siasa juu ya manunuzi ya vifaa vyote vya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Mnyika anakiri kwamba Tume imeitisha zabuni ya manunuzi ya vifaa vya Uchaguzi zikiwemo Karatasi za kupiga Kura. Kwa Taarifa hiyo inathibitisha NEC imefuata taratibu za manunuzi ya Umma kisheria, Na kwa maana nyingine Mzabuni aliye shinda tenda ndiye aliyepewa kazi. Lakini Mnyika ameonesha wasiwasi juu ya Mzabuni wa Manunuzi ya karatasi tu za kupigia Kura (ballot papers) kuwa "kwa vyanzo vyao CHADEMA" Kampuni inayochapisha Karatasi iko Dar es salaam.

Kwa maoni yangu naona Bw. Mnyika anasahau kwamba kabla hajaifanyia uchunguzi NEC kupitia "vyanzo vyao" , yeye kama Kiongozi na mtendaji Mkuu wa Chama alitakiwa kufika NEC na apate Taarifa kuhusu manunuzi ya Vifaa mbali mbali yalivyofanywa kama kuna haja hiyo na (kwa basis ile ile) kwamba ni Manunuzi ya UMMA na kwa namna yoyote Taarifa zake zipo NEC sio kwenye "Vyanzo vyao"

Ikiwa Kampuni imeshinda zabuni na kupewa tenda ubaya uko wapi kiasi cha kutiliwa shaka na Mtu Mkubwa kama yeye?, Karatasi za kura zina maajabu gani yanayoweza kutiliwa shaka?, Ni nini umaalum wa kuona Afrika kusini wanaweza kuwa na sifa za ziada kuliko Jamana (Kama kweli Jamana ndio wametengeneza hizo ballot papers?)

Kama Chadema ambayo ni Taasisi, haijawahi kuingiliwa katika maamuzi ya manunuzi ya Vifaa vyake vya kazi na Taasisi nyingine yoyote, Je, Ni sawa kuishurutisha NEC kufuata matakwa ya CHADEMA?

Bw. Mnyika haoni kwamba kufanya hivyo ni kuingilia Uhuru wa Tume kama ambavyo anaaminisha Umma kwamba Tume hii haipo huru?, Unasisitizaje mabadiliko kama wewe hutaki kuwa Mfano?

USHAURI
Katika kutafuta Mafanikio kisiasa na hata kushika Dola ni vyema CHADEMA kikajikita zaidi kuonesha ubora wa sera zake kwa wananchi hasa katika siku hizi zilizobaki kuliko kila wakati kutafuta Migogoro na Migongano isiyo ya lazima na kuweka kila "kinachohisiwa hakipo sawa" mitandaoni au kwenye vyombo vya habari bila ya kufuata utaratibu wa kisheria ili kujiridhisha na jambo fulani na ikibidi kama haliko sawa kulizuia.
Makaratasi ya uchaguzi sio sawa a na yale yanayochapishwa na makampuni yaliopewa tenda ya kuchapisha vitabu au kalenda za makampuni
 
Hawa jamaa tumewashitukia! Haiingii akilini umpe tenda mtu wa Africa kusini ili hali kuna watanzania wanaweza! Juzi tu walidai sekta binafsi inakufa kisa haipewi tenda na serikali, leo mtanzania kupewa wanalalamika tena! Nadhani chandimu wanatumia matope kuwaza si akili ninazozijua mimi!
 
Wewe ni mshauri wa CHADEMA?
Umepanick brother. Pole.
 
mnyika ni kiongozi wa hovyo sana
mwaka 2015 alikua anailazimisha tume iwape nywila za mitandao ya tume
mwaka huu anakuja na kiroja cha kutaka tume ieleze mzabuni ni nani
karatasi ya kura hata ikichapwa Namtumbo,haibadili maamuzi yangu ya kumchagua Tundu lissu,anachofanya mnyika ni kuwavuruga wapiga kura wake na kuwakatisha tamaa tu
Eti utamchagua TL? Ubarikiwe.
 
Unasema karatasi zinamaajabu gani?
Jua yakuwa kunaweza kuwa na chemical zinawekwa kwenye kisanduku cha lisu ukimuwekea tick inafutika after 2 hours ,hiyo technology unajua?
Umelishwa uwongo. Hizo ni hadithi za kufikirika
Kwa kura ngapi atakazopata mpaka aibiwe?
Watz ni wale wale wataendelea kuchagua viongozi sio kundi la matapeli
 
Back
Top Bottom