Kuna ilivyo na inavyopaswa kuwa. ARGUMENT YAKO NI SAHIHI ILA:
Fei ameona fursa. Club yake inampa mshahara wa m4, amebakiza muda mfupi, kuna club inamtaka. Hapo kuna fursa ya kupata fedha iwapo atasainiwa akiwa huru. Ts business nothing personal.
Umeona mancity inachofanya kwa Halaand? Madrid imeonyesha nia tu City wamekimbilia kupandisha mshahara na kumuonyesha mchezaji kuwa tunakuthamini. Viongozi wa Yanga walikuwa na nafasi ya kuboresha maslahi ya Fei angalau yafanane na jina lake. Hii hupunguza njaa zisizo na msingi. A DOG IS LOYAL TO THE ONE WHO FEEDS IT.
Badala yake Yanga walitaka kupiga fedha ndefu kupitia Fei. Mshahara kidogo, Mkataba upo mwisho halafu wamuuze m500 na inawezekana bila Fei kupata chochote. Fei kaona bora achukukue hiyo fursa hata kama itamgharimu kusubiri hadi 2024.
Ni kama tu dalali aliyekutafutia mteja wa nyumba yako halafu yeye atake kuchukua fedha mara mbili ya unachopata wewe sababu amemshawishi mnunuzi. Unaweza jikuta unasema siuzi tena tuache tu.
Mpira ni burudani kwa mashabiki na maslahi kwa wachezaji.
View attachment 2566696