Kutokana na ukweli usiofichika ndani ya nchi ya Tanzania kwamba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni miongoni mwa Chama Kikubwa cha Siasa na pia ndio Chama kilichoshika madaraka mpaka sasa na ambacho kinatabiriwa kwa asilimia kubwa kuendelea kushika madaraka na kuunda Serikali kwa mara nyingine tena katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 utakao jumuisha chaguzi za Urais, Ubunge na Madiwani.
Ombi langu kwa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mh Rais John Pombe Joseph Magufuli ambae mara kwa mara ameonesha waziwazi bila ya kificho kuchukizwa na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa, kwamba watuletee wagombea Ubunge ambao hawana harufu ya rushwa wala uchafu wowote kwa maana Wagombea hawa wakishinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ndio hao hao baada ya kushinda Ubunge watakao chaguliwa eidha kuwa Mawaziri ndani ya Serikali au watakao husika katika kutunga sheria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imezoeleka ya kwamba, Siasa za Afrika mara kwa mara zinahusisha matendo ya rushwa na wagombea wa hizo nafasi mara nyingi hawachaguliwi kutokana na Sifa zao, elimu zao au yapi watakayo watendea wananchi wao, bali rushwa ya pesa na nyinginezo (rushwa iwe ya wazi wazi au ya Siri) ndio utumika kuwa kigezo cha mwisho cha uamuzi na kuchagua ni nani atakae shinda. Ndio kinachoendelea mpaka sasa na mkifuatilia Wagombea wote kwa undani basi utakuta wagombea karibia wote walijihusisha kutoa rushwa eidha kwa Siri au kwa Uwazi kwenda kwa Viongozi, wajumbe na wapiga kura kwenye majimbo mbalimbali.
Inawezekana katika sehemu mbalimbali ya majimbo ndani ya Tanzania ya kwamba eidha rushwa imetumika au inatumika , pia wagombea wengine wengi uenda walianza kampeni mapema, na wengine inasemekana mpaka walikamatwa siku moja kabla ya uchaguzi wa jana na kuwekwa ndani kwa kutoa rushwa na kushawishi wajumbe wapiga kura, hawa wote hawafai kuwepo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki katika kutunga Sheria au kuwa Mawaziri watarajiwa.
Mfano mzuri wa baadhi ya maeneo yanayosemekana yalinuka rushwa ya waziwazi kabisa ni kama Kibamba - DSM, Bukoba Mjini - Mkoani Kagera, Kinondoni - DSM, Msalala - Shinyanga, Bunda - Mara, Bukene - Tabora, Kigamboni - DSM, Nzega - Tabora, n.k haya ni maeneo machache katika mengi yaliyohusishwa na changamoto hizi za rushwa ambapo baadhi ya Wagombea walioshindwa mpaka wale washindi wa Kura za maoni kuanzia nafasi ya kwanza mpaka nafasi ya tano au zaidi katika orodha ya washindi wa baadhi ya majimbo, wengi wao inasadikika wametumia au walitumia rushwa kushawishi wajumbe kwa namna moja au nyingine waweze kuwapigia kura kabla na baada ya chaguzi zinazoendelea.
Kwa majibu na ukweli Zaidi kuhusu majimbo hayo tajwa hapo juu na majimbo mengine mengi Zaidi, Vijana Wazalendo wapo waulizeni na watoe taarifa kamili ya kweli ya mienendo ya kila mgombea kabla na baada ya chaguzi za jana na zinazoendelea mpaka sasa katika kila majimbo na mtapata picha na ukweli ninao jaribu kuwashauri.
Mwisho, Ombi hili pia liende kwa vyama vya Siasa vya Upinzani kutuletea wagombea walio wasafi kwa maana Tanzania ya kweli na yenye nguvu duniani ni ile Tanzania ambayo itapata Viongozi wenye dhamira ya kweli na Uchungu katika kuwatetea Wananchi wa Tanzania na Taifa la Tanzania BILA YA KUTUMIA RUSHWA
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
ANGALIZO
Mimi SIO Mwanachama wa Chama chochote cha Siasa na Kazi yangu siku zote ni kushauri kwa manufaa ya Taifa la Tanzania na Wananchi wake, Pia natambua ya kwamba Ushauri au Ombi siku zote SIO lazima lifuatwe na linaweza kuachwa ila kama kweli Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Vyama vingine vya Siasa nchini Tanzania mna dhamira ya kweli katika kuwaletea Watanzania Viongozi bora kwa maslahi ya Taifa la Tanzania na Watanzania na pia kuisambaratisha rushwa basi mnaweza kuwa Wazalendo wa dhati kabisa kwa kuwakata na kuwaondoa wale wote waliotoa rushwa, kuvunja kanuni au kuvunja sheria ata kama walishinda kura za Maoni au waliofatia katika ushindi bila ya kuangalia ni nani ameshinda au ni nani ambaye aliyefuatia katika orodha ya washindi 1 mpaka 10 au zaidi ya hapo.