PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,786
- 35,916
Imekuwa desturi na mazoea kwa madereva wengi wanaoendesha magari yao binafsi kufanya safari zao ndefu muda wa mchana ingawa ni jambo jema ila kwa mtazamo wangu mimi naona ni shida na usumbufu mwingi njiani.
Naongea hivyo kwasababu ndani ya mwezi Machi nilifanya safari ndefu ya kwenda Mwanza na gari yangu. Nakumbuka nilianza safari usiku saa 7 kutoka Dar ili kuepusha usumbufu kwenye kipande cha Dar-Moro (kwa wazoefu wa kipande hiki watakubaliana na mimi). Muda wa mchana nilipata shida na usumbufu na traffic pamoja mabus na fujo zao mpaka naingia Mwanza usiku saa 3.
Mpaka nimeamua kuandika ushauri huu ni kwa madereva wenzangu ni ushuhuda niliouona kwa macho yangu wiki hii.
Jumamosi iliyopita nimefanya safari tena nyingine ya kwenda Mwanza kwa kupanda bus hakika vituko vya madereva wa bus ni noma, hawa jamaa wanatumia barabara watakavyo,wanaovertake watakavyo tena sehemu yeyote ile ilimradi amekupita, yaani zile speed za miaka ile zimerudi tena na traffic hawana la kusema kwasababu jamaa alipigwa tochi mara 5 na bado hakupigwa cheti mpaka tunafika Mwanza.
Dereva wa bus alikuwa anaovertake mpaka malori matano hasa pale akiona mbele yake inakuja gari ndogo yaani utake usitake utasimama tu mpaka amalize kuovertake kumbe jamaa wanatudharau sana mpaka wanatuita wamama wa nyumbani (msemo huu alikuwa anautumia dereva wa bus akiwa anafanya fujo zake).
Nimeshuhudia kwenye vibao vya speed 50 magari madogo wanakatwa na traffic huku bus letu linapita tu tena na mwendo mdundo bila shida tena likiwa speed 102 hata ile alarm ya speed hakuna.
Nawashauri madereva wenzangu tembeeni usiku kuepusha majanga mchana haya mambo ya mchana tuwaachiwe wenye njia yao madereva wa mabus kwasabb kama kuna watu wanaenyoj barabaran ni watu wa mabus tu...Wale wenzangu na mm tusione tabu kuendesha usiku