Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunawahi harusi kesho yake. Tukatoka Mwanza saa 12 jioni ili tuingie Dar saa 2 au 3 asubuhi.

Kwenye gari kila mtu alilala, tukabaki mi na dereva tu tunapiga story.

Tukafika maeneo ya tabora nadhani igunga sijui mida ya saa 5 usiku, kitu kimewaka moto.

Hamadi kuna lorry kama mita 50 limezima kati ya barabara na halijaweka alama yeyote. Uzoefu wa dereva ulituokoa lasivyo tusingekuwa duniani leo.

Tulivyofika manyoni mida ya saa 7 hivi tukaamua kulala tu. Hatukuona sababu ya kuwahi tena mjini.

Safari za usiku zinahitaji chombo na dereva imara.
Hata dereva imara pia maana kuna kusababishiwa majanga unafanyaje?usiku kuna so many reckless drivers na malori yanapaki hovyo sana
 
Usiku ni risk sana, niliwah safiri mara moja niliapa sirudii tena huo ujinga, ni bora hata nitumie siku mbili njiani!
Mkuu safari za usiku nimefanya Sana Ila hatari ya kufa IPO nje nje Sana, ndugu zangu wengi wameshauri Sana kuhusu safari za usiku
 
Sasa mbona Uzi wako una 'promote' watu wasafiri usiku na sio mchana ?
Kipindi napost huu Uzi nilikuwa nasafiri usiku Tu ila ndugu zangu wamenihusia Sana kutofanya safari za usiku kutokana na macho yangu kusumbua
 
Kwa uzoefu wangu wa kurndesha gari usiku na mchana, mjini na safarini, nitofautiane na mtoa mada. Kama ni safari, usiku kuna risks nyingi sana, la kwanza na kubwa ni uoni hafifu. Ajali nyingi husababishwa na hili. Hasa kwa madereva wasio na uzoefu, epuka kuendesha usiku.
 
Naogopa sana safari ndefu, Nina kistalet mwaka wa nne sass sijawah kwenda hata km200, December hii labda nijaribu!
Starlet ni chuma cha pua,labda iwe ni mbovu tu
 
Back
Top Bottom