Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

Unafikiri ndio itaku save hio mbinu na wao wanajua ni uongo tu! Wanajuwa wazi unadanganya na hapo ndipo atapoanza kukusumbulia!
Imenisaidia mara kadhaa. Ni kiasi cha kuwa serious tu; pia ikitegemeana na muonekano wako na usafiri unaotumia. Wengine tuna sura za kikauzu, ukisema kitu unaaminika mara moja.
 
Ila mbona ata mchana ukifata vibao vyao vizuri hawasumbui
 
Ujue kusumbuliwa Kuna kuja pale ukiwa na baby warker lazima traffic wakusumbue lakini kana una drive gari la ukweli ma traffic hawakusimamish hovyo hovyo safiria Ford Ranger , Vx V8, BMW x6, Land cruiser ,etc usumbufu kwa matrafic kusimamishwa unapungua .Tafuteni hela mmiliki gari za ukweli muone Kama mtasumbuka njian.
 
Ila mbona ata mchana ukifata vibao vyao vizuri hawasumbui
Ukiwa na gari ndogo umbali wa dar to Dodoma waweza simamishwa hata mara 20 kukaguliwa lakini Kama una gari la maana kusimamishwa hupungua Sana , safiria land cruiser hard top uone Kama utasimamishwa sasa ukisafiria spacio and hizo baby warker utasimamishwa kukaguliwa hadi utakoma[emoji23][emoji23]
 
Tatizo la usiku kuna possibility ya mambo ya kutegeana mawe na kuachiana ngeu na vilema vya mapanga
 
Dereva anaye sinzia usiku barabarani huyo ni mtu tu na mambo yake na si dereva wa taaluma kama mimi hapa,usiku ndiyo sichoki na ninakata kilometer za kutosha
 
Nzuri sana, naamini kwema pande zako Watu8

Ndo maana usiku sipendi kusafiri. Imagine jamaa angegonga huyo tembo. Usiku kuna Mengine mkuu.
 
Hahahah mnyama akikatiza humuoni au πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna ile ghafla bin vu, mkuu. Na hii sitasahau kudrive (sikuwa dereva) toka Maputo to Durban, kuna sehemu na vibao vya tahadhari vimewekwa kuwa wanyama kama ng’ombe wanakatiza. Kuna mmoja alitusababishia kizaa zaa, giza halafu mvua. Sitosahau lile tukio.
 
Mvua kali usiku haifai unaendesha speed 60 tu maximum mpaka pawe clear
 
Kutembea usiku kuna raha yake ila barabara ya Mwanza shinyanga ni mbaya aisee. Kwanza ina matuta kurupushi, pili matuta yake ni yale tuta mrusho. Tuta kama gogo. Safari ya Dom Mwanza unaweza tumia masaa sita mwanza hadi shinyanga ila ukatumia hata manne kutoka shinyanga kwenda Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…