Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

Hata dereva imara pia maana kuna kusababishiwa majanga unafanyaje?usiku kuna so many reckless drivers na malori yanapaki hovyo sana
 
Usiku ni risk sana, niliwah safiri mara moja niliapa sirudii tena huo ujinga, ni bora hata nitumie siku mbili njiani!
Mkuu safari za usiku nimefanya Sana Ila hatari ya kufa IPO nje nje Sana, ndugu zangu wengi wameshauri Sana kuhusu safari za usiku
 
Sasa mbona Uzi wako una 'promote' watu wasafiri usiku na sio mchana ?
Kipindi napost huu Uzi nilikuwa nasafiri usiku Tu ila ndugu zangu wamenihusia Sana kutofanya safari za usiku kutokana na macho yangu kusumbua
 
Kwa uzoefu wangu wa kurndesha gari usiku na mchana, mjini na safarini, nitofautiane na mtoa mada. Kama ni safari, usiku kuna risks nyingi sana, la kwanza na kubwa ni uoni hafifu. Ajali nyingi husababishwa na hili. Hasa kwa madereva wasio na uzoefu, epuka kuendesha usiku.
 
Naogopa sana safari ndefu, Nina kistalet mwaka wa nne sass sijawah kwenda hata km200, December hii labda nijaribu!
Starlet ni chuma cha pua,labda iwe ni mbovu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…