Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 9,626
- 6,731
Alikosea sana Lillian, ilibidi amshitaki polisi tu ili akaliwe uroda gerezani na wajanja wenzake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio rahisi kiasi hicho, aibu yake na depression itakumaliza. Huyo Lillian hakuwa na choice zaidi ya kulala na jamaa.
Lakini najiuliza, mwanaume uliyekamilika, unafanya hivyo ili upate nini hasa?
Akiripoti polisi kumbuka hubby to be atazipata taarifa na ndoa itaota mabawa. Hizi tricks mkuu hawa bullies huwawezi hata ufanyeje.
Mkuu kuna wengine wana ji resi.. Ukituma vocha unashangaa wasap imechangamka.Mm hata mapenzi yakoleajeeeee, picha ya pamojaaa sipigiiiiii ng'oooooooooo
Itakuwa hakutaka yeyote ajueangetoa taarifa polisi halaf ndo angempanga kusex
Anajua kuwa sio bikra, lakini kujua kuwa kuna picha za utupu za mke wako mitandaoni ni fedheha kubwa sana.Kwamba mwanaume hajui mkewe hajamkuta bikra [emoji28][emoji28]
Jmn basi ni akili tu mbaya ya mtu.......Mkuu kuna wengine wana ji resi.. Ukituma vocha unashangaa wasap imechangamka.
Ushauri mzuri ila bado hajachelewa sababu bado jamaa anaweza akaendelea kuzitumia kwa manufaa yakeAngeenda police ile siku tu amepokea picha!
Mungu atuepushe sisi na vizazi vyetuMm hata mapenzi yakoleajeeeee, picha ya pamojaaa sipigiiiiii ng'oooooooooo
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏Mwanaume timamu hawezi fanya alichofanyiwa Lily..enwei tuwe makini
Pole kwa rafikio
Muache Zinaa musubiri waume na wengine wasubiri wake kwani dhambi ya zinaa haijawahi muacha mtu SalamaHello wanajamvi,
Natumai mko poa kabisa na mnaendelea vema na weekend!! Kwa wale mashabiki wote [simba na yanga] nawatakia ushindi lakini sipendi yoyote afungwe for the sake ya furaha ya marafiki na jamaa zangu waliogawanyika katika kambi hizo mbili na wote nawapenda.
Back to the topic;
Leo nimesimuliwa story kutoka kwa rafiki yetu moja ambayo imeniuma sana, kama jamii nikahisi nina jukumu la kuwaelimisha na wengine huenda wakajifunza. Hata kama hatajifunza hata moja angalau nimefikisha kama mwanajamii.
Nina rafiki zangu wawili ambao tunapendana sana na urafiki wetu umedumu toka O LEVEL mpaka sasa regardless kuwa A level tulisoma shule TOFAUTI lakini Chuo tukakutana different courses...
Moja ya Rafiki zangu [naomba kumuita LILIAN siyo jina lake halisi] alikuwa na boyfriend wake ambaye kulingana na maelezo take walipendana sana. Uhusiano wao ulianza akiwa advance na ukadumu kwa kipindi chote tulipokuwa Chuo ingawa walisoma chuo TOFAUTI.
Baada ya kumaliza chuo mahusiano yao yaliyumba na hatimaye yalivunjika na kila moja akaendelea na maisha yake...
Baada ya muda kupita LILIAN akapata mchumba, mahari yakatolewa na taratibu za ndoa zikaendelea...
Kumbe kipindi chote haya yanafanyika aliyekuwa Boyfriend wake Tumuite Innocent alikuwa anafuatilia na kumbe hakuwahi kuwa happy kumwona aliyekuwa girlfriend wake anaolewa...
Wakati mambo yakiwa ukingoni kufunga ndoa Innocent akamtafuta LILIAN na kumwomba wakutane waongee... unfortunately Lilian akakataa na kumweleza yaliyopita baina yao yamepita hivyo kila mmoja anapaswa kuendelea na maisha yake...
Zikapita kama siku mbili hivi akiwa hana hili wala lile my poor friend Lilian akashangaa anapokea meseji WHATSAPP kutoka kwa Innocent ikiwa na maelezo marefu lakini pia ikiwa na picha... Kufungua zile picha akajikuta akijiona Akiwa uchi wa Mnyama kila kitu kikiwa hadharani...
Moja ya masharti ya Innocent ni kuwa ikiwa anataka kuendelea na michakato yake ya harusi peaceful basi amkubalie na aandae mazingira WASEX vinginevyo kila kitu kitaenda public....
After a much panic, contemplation asijue nini cha kufanya na hofu ya kupoteza ampendaye, ndoa na aibu akajikuta akikubali MASIKINI [IMENIUMA SANA]...
Lilian AMESEX TENA BILA HATA KINGA roughly 8 days kabla ya ndoa yake.... asijue USALAMA wa afya yake kwani amekutana na mtu ambaye ameachana Naye miaka kadhaa na hajui hali yake....
Rafiki yangu ameingia kwenye ndoa akiwa na maumivu lakini akiwa hana uhakika kama Kweli Innocent amefuta picha na video zake zote kama walivyokubaliana au kuna siku tena atazitumia dhidi yake...
Anatamani angemiliki silaha au angekuwa na fedha atafute mafia akamalize kazi lakini YOTE hayo Yapo nje ya uwezo wake..
Ndugu zangu NEVER EVER SHARE YOUR NUDE PHOTOS AU VIDEOS KWA GHARAMA YOYOTE... HASA KWA MAHUSIANO HAYA YA NJE AU KABLA YA NDOA...
Huwezi jua ni kwa kiwango gani zitahifadhiwa na kesho kutumika dhidi yako, zikakufanya mtumwa na kukutia wasiwasi na mashaka!!!
Najiuliza siku Mume wake akiijua hii story ni vipi itakuwa ndoa ya rafiki yangu LILIAN!!!
POLE SANA LILIAN, kwa hakika uliifanya siri na hukutamani aijue yoyote lakini hakuna siri ya wawili na nisamehe nimeitoa hapa angalau kuwafunza na kuwanusuru wengine KWANI NINA HAKIKA KAMA UNGEPEWA NAFASI YA KUANZA UPYA USINGEFANYA YOTE ULIYOYAFANYA AWALI.
MUNGU AKUJAALIE NDOA YENYE HERI NA FANAKA, MPENDE SHEMEJI YANGU NA ISHI KWA FURAHA KWA MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA DUNIA YUPO KAMOJA NA WEWE.
Kaka zangu nawashauri ziheshimuni nyoyo za wale waliojitoa kwa ajili yenu
Kwa hakika sii jambo jepesi kihivyo someone to have your nudes.....Uyoo mwanamke naye ni mpumbavu snaa elimu yake imemsaidia nn sasa ata iyoo ndoa naona ni kama kaenda kujichimbia kaburi Tu ishu ndogo kama iyoo ameshindwa kuisolve vp mmewe akitetereka kiuchumi ataweza kuisimamia familia yeye peke yake alishindwa kusuka mpango wowote amuweke uyoo jamaa ndani na kufungua kesi useless kabisa na elimu yake
Huyo alitakiwa amwambie ukweli mumewe kwamba fulan ananimanipulate.
..wafanye mchongo siku anaenda kumla wamkamate akatiwe ndani.
Bora aibu mara moja kuliko aibu mara 2.
Mume mtarajiwa kwan hakua na ex.
Km kweli anampenda angemsamehe sababu yalitokea kbl yake.
Sasa kinachoenda tokea atapata aibu mara 2 ya picha kutofutwa..na kusambazwa
Na kulalwa kbl ya ndoa...tena siku chache.
Mume akijua hili i swear atamuacha.
Hivi kwani hamnaga watu wa kuwashirikisha mambo wawashauri? Ht mmoja unayemwamini dada? Hana.
Sio kila jambo la kusolve peke yako au la kufa nalo rohonii, ndio hawa wanajiuaga.
Kutunza siri kutamcost soon, huyo inno ahajfuta picha.
Ni kosa kiaheria kumtisha mtu..the day kanitumia text ya vitisho naandaa polisi.