Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Mayalla ni Njaa. Ni vyema uchapishe gazeti. Karma ilishaondoka na jiwe.

Eti Mdee! Yeye mwenyewe alishajimaliza. Labda nikuulize "Chadema ndio walimtoa yule dada kule gerezani"?
 
Please, Zitto hakufukuzwa Bali alijifukuzisha baada ya kwenda mahakamani na akabwagwa.
Mkuu Mchumi econonist , haya mambo ya zamani kuna wengi hawayajui
  1. Jee wajua kuwa Zitto alitimiliwa na CCM ya Chadema ndipo akakimbilia mahakamani?
  2. Jee CC ya Chadema ina uwezo kumfukuza NKM?.
  3. Kumbe katiba ya Chadema ina kipengele cha mtu akienda mahakamani akashindwa ndio anakuwa amejifukuzisha. Jee wajua kipengele hicho ni kinyume cha katiba ya Tanzania?
  4. Jee wajua Zitto alishindwa kwa kitu kinachoitwa legal technicalities na sio points of law, ni ukweli usiofichika CC ya Chadema haina mamkaka ya kumfukuza NKM!. Do you know what ilikuja kuwa happened kwa watesi wa Zitto?.
  5. Sasa hiyo karma ya Zitto alifanya hayo, sasa hamuogopi karma ya hao 19, itakuwa ni kiasi gani?.
P
 
Mkuu Pascal, mimi kwa kweli sijui nani amejikwaa wapi na kuangukia wapi. Lakini kuwa mwangalifu na maneno ya Kiingereza kwa sababu yanakuharibia.
Sio sawa kusema guilty conscious! Inapaswa kuwa guilty conscience.
Kuna tofauti kati ya consciousness na conscience!
 
Ungeanza na makandokando ya chama tawala ..kana kwamba wote ni wapya hawakuwapo Utawala wa JPM ... HAO NDIO WAMEANGUKA VIBAYA WAMEANGUKA PUA ...WANAHANGAIKA KUPUKUTA NGUO WAKATI WANA MAJERAHA YA KUTIBU.... " Read between lines " - natumia kamsemo kako
 
Amepewa mzigo wa kutosha na Halima
 
Zanzibar karibu wamuue babu wa miaka 83 na yupo kimya kama vile haoini, huyu ni Pascal Njaa
 
Paskali, bandiko lako limenikumbusha enzi za sahani za santuri, zile sahani zilikuwa zinatengenezwa kwa kutumia nta, sasa ikipata mkwaruzo kidogo basi sindano ya gramafoni itashindwa kuvuka mkwaruzo hivyo wimbo utajirudiarudia hapohapo mpaka kichwa cha santuri ukishitue kidogo ili kivuke mkwaruzo, sasa kichwa cha gramafoni(HIS MASTER'S VOICE) ni, ni Paskali Ma, ma, Mayalaaaa.
I wish someone could overhaul your brain and have something new from your head.
Paskali wewe alishasema rekoding'i iliyofanyika Mwanza inauthibitisho kuwa Mbowe ni gaidi, sasa ni ushauri gani unataka kuipa Chadema! Kwani ukiiacha Chadema na kuanguka kwake wewe utapungukiwa nini? Kwani mkwamo wa Tanzania unatokana na Chadema? Waache hao magaidi na ugaidi wao unaouamini.
I like your likes.
 
Paskali nakumbuka niliwahi kukusoma mahala ukidai umri wako umekwenda hutaki tena kusumbuana na watu, naamini uko kwenye practical ya hiyo kauli.

Hivi Kitila Mkumbo ambaye unasema hawezi kupitishwa popote na CCM kugombea 2025, bado unamuita ni "think tank" kwa wengine?!

Niliposema Kitila ni mjuaji, labda kosa langu sikumalizia sentensi, Kitila ni mjuaji wa muharibifu, kama angekuwa na maarifa ya maana angetengeneza namna nzuri ya kundi lao kuingia kwenye uongozi wa Chadema, lakini badala yake aliandaa mapinduzi haramu.

Kuhusu kufukuzwa wale wanawake na Chadema, sioni uhuni wowote, wewe unataka kulazimisha kuchanganya kati ya Katiba ya nchi, na Katiba ya Chadema, kina Mdee wamefukuzwa kihalali kwa Katiba ya Chadema ambayo msajili aliipitisha.

Katiba ya nchi pia huwezi kuitumia kuwakingia kifua kina Mdee kwasababu ndio inayotaka mbunge sharti awe anatokana na chama cha siasa bungeni, hapa mwenyewe unakiuka Katiba ya nchi kwa kuendelea kuwatetea hao wanawake.

Naamini kama ungeandika haya unayotuwekea sisi huku kwenye mtihani wako wa "constitutional law" usingepata hilo "banda".

Pia unasema Chadema imeumizwa na "karma" baada ya kuwaonea wale madiwani na Zitto. Pasco unaficha madhila wanayofanyiwa Chadema kwenye chaguzi zetu ili kuifichia aibu CCM yako, halafu unageuza hayo madhila [ wizi wa kura etc] kuwa ndio "Karma" kwa mtazamo wako, wacha usanii.

Hata yule unayesema Karma ilimuumiza vibaya, nae hakuumizwa na Karma kwa sababu alifuata wajibu wake, bali aliumizwa na kiongozi aliyekuwepo aliyekuwa na tabia za kidikteta. Zitto kujipeleka mahakamani alijua fika ambacho kingempata, na ndicho kilimpata.

Vinginevyo, kama hiyo ndio Karma, basi hata hiyo "Karma" yenyewe haitendi haki, nayo ni kama CCM na mambo yake tu, mimi siiamini.

Mwisho kuhusu taratibu unazodai hazifuati sheria zinazotumiwa na Chadema kuwafukuza wanachama wake wasaliti, hapa napo unaleta ujanja tu.

Hao jamaa hufukuzwa baada ya kufuatwa taratibu zote za kichama, na ndio maana hata wakienda mahakamani hushindwa kesi, lakini wewe Paskali unataka kujiweka juu ya KK ya Chadema, Baraza Kuu la Chadema, na mahakama zetu, kwamba wewe ndie unajua zaidi ya hao wote!

Naanza kuona nawe utakuwa na ule ujuaji wa kina Kitila na Zitto, ujuaji wa uharibifu.
 
Paskali sijui kala maharage ya wapi huyu mtu, yaani anajitoa ufahamu to the maximum
 
Paskali sijui kala maharage ya wapi huyu mtu, yaani anajitoa ufahamu to the maximum
 
Huyu hajielewi, anazungumza kana kwamba kuna chochote CDM wangeweza au wanaweza kufanya C19 watoke mjengoni.
 
Hakuna Karma,

Mambo ya kuamini KARMA ni ujinga.
 
Hakuna Karma,

Mambo ya kuamini KARMA ni ujinga.
Mkuu Yoda , naheshimu mawazo yako, kwa vile mambo ya karma ni mambo ya imani, siwezi kulazimisha ninachoamini mimi na wengine waamini, hivyo naheshimu msimamo wako kutoamini karma ila nakuomba isiitukane karma kuwa ni ujinga!.

Hata Waislamu wasioamini Utatu Mtakatifu wa Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu hawaruhusiwa kutuambia ni ujinga, au kusema Yesu sii Mungu, au Sisi Wakristu tunao amini katika Yesu na sio kwa Mtume, haturuhusiwi kubeza imani za wengine, usiamini kwenye karma ila karma sio ujinga na hata kama huamini kuwa karma ipo, ukifanya jambo baya linalo stahili hukumu ya karma, karma itakutandika tuu uwe una amini au huamini na hizo bakora za karma unaweza kuziita jina lolote, ajali, majanga, bahati mbaya, mikosi, laana, radhi, etc ila karma ipo and it's for real!.
P
 
Inasikitisha sana kwa mwandishi nguli na msomi wa sheria kuwa chawa wa Halima. Watu wanaroga vibaya jamani duh!!!!
 

Attachments

  • images (32).jpeg
    30 KB · Views: 5
Paskali sijui kala maharage ya wapi huyu mtu, yaani anajitoa ufahamu to the maximum
Kwahiyo waliompiga lisu risasi karma yao tayari au bado?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…