Ushauri: Walimu wote waanze na mishahara sawa, mwalimu wa science kuanza na mshahara mkubwa ni dharau kwa walimu wengine

Ushauri: Walimu wote waanze na mishahara sawa, mwalimu wa science kuanza na mshahara mkubwa ni dharau kwa walimu wengine

Leo tena nimekuja kulalamika,
Hivi mwaka 2019 serikali iliona nini?
Ilijisikiaje au kwakuwa head alikuwa mwalimu wa science akaona awabebe wenzake?

Najua lengo ni kuwatia motisha walimu wa science,
Sawa.
Lakini je ili iweje? Kwa faida ipi?
Shule ni zile zile,
Wanafunzi wale wale,

Tena wakifika form three walimu wa science wanajichagulia watoto wao wa kuwafundisha,
Unakuta shule wanafunzi 300 wanasoma historia
Wanafunzi 60 wanasoma science
Hapo mwalimu mwenye mzigo mkubwa ni yupi? Kama sio huyu mwenye watoto 300!

Badala ya kujifanya kuongeza pesa kwa walimu wa science,
Serikali iajiri walimu wengi wa science na sanaa ili kuweka ikama sawa,
Na kutoa mzigo mkubwa wa vipindi kwa walimu waliopo,
Halafu iongeze mishahara na kuweka mazingira mazuri ikiwemo nyumba za kisasa kwa walimu,

Walimu acheni kujiwekea matabaka ninyi kwa ninyi,
Hakuna mwalimu bora kuliko mwingine
Itikadi za mwendazake ziachwe kama zilivyo
Supply and demand i guess? Bidhaa zinapokuwa nyingi sokoni thamani inashuka na bei inashuka pia ila zile chache na zinazopatikana kwa shida nadhani thamani inaongezeka .
 
Tofauti ya mwalimu wa sayansi na sanaa huwa ni pale wanapoajiriwa na tofauti haizidi 50k ila baadae wakipanda cheo mshahara huwa unalingana. Nyongeza hiyo nafikiri ni motisha ya kuwa na vipindi vingi na kuandaa zana za kujiuma na kifundishia
Inatakiwa waongeze walau iwe na utofauti wa 200K.Tbh,sayansi na arts ni mbingu na ardhi..Ila kikubwa ni maboresho yafanyike kwa pande zote ili kusaidia kufanya kazi kwa moyo mkunjufu.
 
Back
Top Bottom