Uchaguzi 2020 Ushauri wangu kwa vijana na wazee wetu, tuchagueni upinzani tuone watafanya nini

Kuchagua upinzani ni wajibu was Kila mpenda maendeleo,CCM imekuwa madarakani toka nchi inapata Uhuru na bado hamna kilichobadilika katika maisha ya watanzania, Hadi leo hi zaidi ya miaka 60 ya Uhuru kiongozi anatuahidi atatujengea barabara,shule na vituo vya afya na hata aibu hawana
 
Nchi sio sehemu ya MAJARIBIO ... narudia TAIFA sio mahali pakujaribia ...Wakajaribu kwenye umeneja wa ma club ya usiku
 
Hao upinzani na ccm hawana tofauti yeyote ni basi tu kuwa ccm ndio imekamata dola.
 
 
Wapinzani hawa hawa wasio eleweka wanataka nini? Sumu haijaribiwi kwa kulamba
 
Ndugu yangu Pazia 3 umeandika kwa hisia sana, naziona hisia zako katikati ya maandishi yako. Huo ni ushauri, na siku zote ushauri unaweza kupokelewa au kukataliwa. Binafsi ninaukataa ushauri wako na pia kuwashawishi watanzania wenzangu nao waukatae ushauri wako.

Mkuu Pazia 3, sumu haionjwi. Yaani kweli unatushauri watanzania "tubeti" mustakabali wa maisha yetu kwa miaka mitano ijayo?. Kumbuka tunaye Rais Magufuli ambaye tayari tumeshaona aliyoyafanya na mipango yake. Akija mtu wa Upinzani atakuwa na vipaumbele vyake vingine. Subirini kwanza mzee akamilishe aliyoyaahidi.

Mjomba Pazia 3, nyota njema huonekana asubuhi. Hao wanaoomba dhamana kwa watanzania kuongoza nchi yetu, walitakiwa waoneshe kwa vitendo jinsi wanavyoongoza vyama vyao kwa demokrasia, weledi na ustaarabu. Wabunge na madiwani wao wawe mfano bora huko majimboni. Kwasasa wameonesha kushindwa kutimiza hilo, kuwapa nchi ni kujiumiza.

Amani Msumari
Tanga
 
Mkuu Mtumishi Wetu, kuhusu maendeleo ya vitu vs maendeleo ya watu, naungana na wewe.

Na utawala hata uwe mzuri vipi, ukikaa muda mrefu sana, unakuwa monotonous unachukua, hivyo kuna need ya kufanya mabadiliko ili kubadili mboga.

Tatizo kwa Tanzania ya sasa ni kweli chama changu CCM kime overstayed lakini tatizo ni utampa nani kuibadili CCM?. It's very unfortunately hakuna mbadala wa CCM, unless useme tuijaribu tuu Chadema au ACT, liwalo na liwe!. Who would dare take such a risk?.

Better a devil you know, than a devil you don't know!.

Chadema ipi ya kuipa nchi au ACT ipi ya kuipa nchi?.
P
 
Daaaah Mayalla KWELI naona umejipambanua kuwa ss ww Ni mpiga zumari..........................
 
Mhh jmn ndo unawinda uteuzi kwa spidi namna hii🤒🤒
 
Kuichagua ccm ni kuridhika na umsikini ulionao
 
Tafuta kitabu kiitwacho" Dictators mind" kimeeleza kila kitu.
Ukiikosa sifa utotoni utaitaka ukubwani
 
Kwa maneno haya nimegundua kuwa watanzania hawajui umuhimu wa upinzani na wataendelea kutawaliwa na ccm mpaka watakapofunguka akili zao. Wasomi wa Tanzania bado sana fikra zao.
Chadema tangu kianzishwe kina zaidi ya miaka 20 lakini hawajajenga ofisi ya makao makuu ya chama licha ya kupata ruzuku ya bilioni tatu kila mwaka! Hao ndio unataka tuwape nchi waongoze. Kama wameshindwa kujenga ofisi ya makao makuu ya chama tena kwa faida yao wataweza kweli kukuletea wewe maendeleo?
 

Bandiko lako lina mantiki sana sema tatizo tulilonalo na upinzani ni kwamba wamedhamiria sana kuingia Ikulu kiasi kwamba wanasahau kitu ambacho ni cha muhimu zaidi kuliko wao kuwa Ikulu. Mtazamo wangu katika kuhakikisha Upinzani (ACT Wazalendo CHADEMA nccrmageuzihq et al) unakishinda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulitakiwa uanzie chini kuja juu.

Hakuna kitu kinakera na kuumiza kama kusikia Wabunge wa CCM wakigonga meza kupitisha sheria na kanuni kandamizi kutokana na wingi wao Bungeni. Hakuna kitu kinaumiza kama kushuhudia kwamba muhtasari wa uendeshaji nchi unaamuliwa kutokana na wingi wa Wabunge wa Chama fulani badala ya kufikiria Wananchi, ambao ndio maamuzi ya wachache walio wengi yanawaathiri moja kwa moja.

Mpaka siku tutakapoamua kuanzia chini, Upinzani utaendelea kubaki kuwa ni 'pacemakers' katika kila chaguzi Tanzania.
 
Nchi sio sehemu ya MAJARIBIO ... narudia TAIFA sio mahali pakujaribia ...Wakajaribu kwenye umeneja wa ma club ya usiku
Ni kweli na kama wanataka kufanya majaribio basi waanze kujenga kwanza ofisi ya makao makuu ya chama chao, haiwezekani chama kina zaidi ya miaka 20 tangu kianzishwe lakini hakina jengo lake licha ya kupokea ruzuku ya bilioni tatu kila mwaka!
 
Mayalla unashauri tusijaribu kuionja sumu!
 
Chama gani unachohisi kinaweza kuwa mbadala w CCM? Hawa ambao mnadai wananuliwa? Km wanaweza kuuza utu wao tukiwapa nchi si ndio tutauzwa sisi pamoja na wao?
 
Huwa naumia sana kuona MTU mwerevu anaposhadadia upumbavu kwajili ya tumbo lake..hicho ulichokitoa ni upumbavu wa kiwango cha stiglerz
 
Uliko bado uko kwenye kibovu cha baba yako kamuulize shangazi yako atakuambia
Acha matusi haya hayatamsaidia Lisu kushinda!

Je kuna mtu alienda ccm kuchukua forom akanyimwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…