Uchaguzi 2020 Ushauri wangu kwa vijana na wazee wetu, tuchagueni upinzani tuone watafanya nini

Kuna Mambo yanaumiza Sana hasa unapoona kijana au mzee akipinga wazi wazi upinzani usishinde uchaguzi. Ni haki yao, lakini hebu fikiria, ukiondoa utawala wa awamu ya kwanza na wa pili, CCM imetuongoza kwa awamu tatu tangu kuanza kwa vyama vingi vya siasa, tumeona madhaifu yao, tumeona mazuri yao, basi tuwapeni na Wapinzani wafanye yao, tutalinganisha baada ya miaka 5 watakayoongoza.

Hatuwajaribishi maana hawaingii kubadili kila kitu, watakuta polisi ipo, mahakama, jeshi, Bunge, shule, vyuo, nk, maana yake wanaposema watafanya tofauti haimaanishi wataanza mwanzo Bali wataboresha baada ya miaka 5 tutawapima.

Kwakuwa CCM ina nguvu na pesa nyingi, baada ya miaka 5 mtatumia kila njia kurudi madarakani endapo upinzani utashindwa kutimiza yale waliyoyaahidi.

Ewe kijana, baba, Mama tuuchagueni upinzani. Kubaki na CCM au kuchagua upinzani haimaanishi tutagawana hela mifukoni, tutafanya kazi Kama siku zote.

Tuungane, tusiwadharau upinzani maana hatujawahi kuwapa nchi tukayaona mazuri na madhaifu yao.

#MakeTanzania great again
Kuchagua upinzani ni wajibu was Kila mpenda maendeleo,CCM imekuwa madarakani toka nchi inapata Uhuru na bado hamna kilichobadilika katika maisha ya watanzania, Hadi leo hi zaidi ya miaka 60 ya Uhuru kiongozi anatuahidi atatujengea barabara,shule na vituo vya afya na hata aibu hawana
 
Nchi sio sehemu ya MAJARIBIO ... narudia TAIFA sio mahali pakujaribia ...Wakajaribu kwenye umeneja wa ma club ya usiku
 
Hao upinzani na ccm hawana tofauti yeyote ni basi tu kuwa ccm ndio imekamata dola.
 
kwani upinzani wenyewe wakuungana ni vyama vingapi si vyama viwili tu CHADEMA na Act Act imejikita Zanzibar,Kusini na kigoma CHADEMA imejikita Tanzania bara upinzani uchaguzi uliyo pita ukipata Kura milioni sita na nusu au saba ukichanganya wapinzani wote CCM milioni Nane watu wapya milioni Saba wameandikishwa, jumla ya wapiga Kura wote no milioni 28 Sasa hapo kikubwa ni upinzani au CCM ni Nani atakuwa na ushawishi wakuongeza wapiga Kura wapya wale waliojiandikisha Safari hii na wale ambao hawakujitokeza uchaguzi uliopita.

Ukitaka kujua Upinzani ni Wabnafsi kupita ccm waambie waungane.
Kila mtu anataka kuwahi ALE
Kwanini hata kama unakubalika usi sacrifize kumpa mwenzako?
Nyerere alijiuzuru na kumuachia Kawawa lkn hawa hawakubali.

Halafu hatuwezi kufanyia majaribio mambo muhimu . Kunyoa tu hatujaribishi saluni itakuwa nchi.
Waonyeshe kupitia shughuli zao za kila siku hata Ruzuku tu hawezi kujenga choo cha shule ?
 
Wapinzani hawa hawa wasio eleweka wanataka nini? Sumu haijaribiwi kwa kulamba
 
Kuna Mambo yanaumiza Sana hasa unapoona kijana au mzee akipinga wazi wazi upinzani usishinde uchaguzi. Ni haki yao, lakini hebu fikiria, ukiondoa utawala wa awamu ya kwanza na wa pili, CCM imetuongoza kwa awamu tatu tangu kuanza kwa vyama vingi vya siasa, tumeona madhaifu yao, tumeona mazuri yao, basi tuwapeni na Wapinzani wafanye yao, tutalinganisha baada ya miaka 5 watakayoongoza.

Hatuwajaribishi maana hawaingii kubadili kila kitu, watakuta polisi ipo, mahakama, jeshi, Bunge, shule, vyuo, nk, maana yake wanaposema watafanya tofauti haimaanishi wataanza mwanzo Bali wataboresha baada ya miaka 5 tutawapima.

Kwakuwa CCM ina nguvu na pesa nyingi, baada ya miaka 5 mtatumia kila njia kurudi madarakani endapo upinzani utashindwa kutimiza yale waliyoyaahidi.

Ewe kijana, baba, Mama tuuchagueni upinzani. Kubaki na CCM au kuchagua upinzani haimaanishi tutagawana hela mifukoni, tutafanya kazi Kama siku zote.

Tuungane, tusiwadharau upinzani maana hatujawahi kuwapa nchi tukayaona mazuri na madhaifu yao.

#MakeTanzania great again
Ndugu yangu Pazia 3 umeandika kwa hisia sana, naziona hisia zako katikati ya maandishi yako. Huo ni ushauri, na siku zote ushauri unaweza kupokelewa au kukataliwa. Binafsi ninaukataa ushauri wako na pia kuwashawishi watanzania wenzangu nao waukatae ushauri wako.

Mkuu Pazia 3, sumu haionjwi. Yaani kweli unatushauri watanzania "tubeti" mustakabali wa maisha yetu kwa miaka mitano ijayo?. Kumbuka tunaye Rais Magufuli ambaye tayari tumeshaona aliyoyafanya na mipango yake. Akija mtu wa Upinzani atakuwa na vipaumbele vyake vingine. Subirini kwanza mzee akamilishe aliyoyaahidi.

Mjomba Pazia 3, nyota njema huonekana asubuhi. Hao wanaoomba dhamana kwa watanzania kuongoza nchi yetu, walitakiwa waoneshe kwa vitendo jinsi wanavyoongoza vyama vyao kwa demokrasia, weledi na ustaarabu. Wabunge na madiwani wao wawe mfano bora huko majimboni. Kwasasa wameonesha kushindwa kutimiza hilo, kuwapa nchi ni kujiumiza.

Amani Msumari
Tanga
 
Mzee wa kitimoto tunachosema ni maendeleo ya watu sio vitu!!
Ethiopia wana mabwawa makubwatuu, wana reli za kisasa, madege ya kumwaga Afrika nzima hakuna, lakini watu wanakimbia kila siku ni UDICTEITA!!
People turned slaves in there own country!!
Fikiria North Korea, China Moscow etc??
Fikiria WaTz kama ulivyokuwa zamani.
Mkuu Mtumishi Wetu, kuhusu maendeleo ya vitu vs maendeleo ya watu, naungana na wewe.

Na utawala hata uwe mzuri vipi, ukikaa muda mrefu sana, unakuwa monotonous unachukua, hivyo kuna need ya kufanya mabadiliko ili kubadili mboga.

Tatizo kwa Tanzania ya sasa ni kweli chama changu CCM kime overstayed lakini tatizo ni utampa nani kuibadili CCM?. It's very unfortunately hakuna mbadala wa CCM, unless useme tuijaribu tuu Chadema au ACT, liwalo na liwe!. Who would dare take such a risk?.

Better a devil you know, than a devil you don't know!.

Chadema ipi ya kuipa nchi au ACT ipi ya kuipa nchi?.
P
 
Mkuu Pazia 3, kwanza asante kwa bandiko hili. Kiukweli bandiko lako ni la ushauri kwa Watanzania, tufanye majararibio ya kuwajaribisha wapinzani kwa kuwapa Ikulu yetu ili tuone watafanyaje!.

Yaani when you have two options, moja umeona deliveries ya mazuri ya alichofanya, na yanaonekanika, halafu mwingine hana lolote la kuonekanika, lakini ana ahadi tuu, hivyo unatushauri tuache kumchagua aliye deliver, mazuri ya kuonekanika na badala yake tumjaribishe mwenye ahadi ili kuona atafanya nini?!. Huku sio kuchezea shilingi chooni?.

Yaani unawashauri watu waache mbachao, kwa msala upitao?. Mimi nawashauri watu humu, katu, usikubali kamwe, bura yako njema, kuibadili kwa rehani!.
P
Daaaah Mayalla KWELI naona umejipambanua kuwa ss ww Ni mpiga zumari..........................
 
Mkuu Pazia 3, kwanza asante kwa bandiko hili. Kiukweli bandiko lako ni la ushauri kwa Watanzania, tufanye majararibio ya kuwajaribisha wapinzani kwa kuwapa Ikulu yetu ili tuone watafanyaje!.

Yaani when you have two options, moja umeona deliveries ya mazuri ya alichofanya, na yanaonekanika, halafu mwingine hana lolote la kuonekanika, lakini ana ahadi tuu, hivyo unatushauri tuache kumchagua aliye deliver, mazuri ya kuonekanika na badala yake tumjaribishe mwenye ahadi ili kuona atafanya nini?!. Huku sio kuchezea shilingi chooni?.

Yaani unawashauri watu waache mbachao, kwa msala upitao?. Mimi nawashauri watu humu, katu, usikubali kamwe, bura yako njema, kuibadili kwa rehani!.
P
Mhh jmn ndo unawinda uteuzi kwa spidi namna hii🤒🤒
 
Kuna Mambo yanaumiza Sana hasa unapoona kijana au mzee akipinga wazi wazi upinzani usishinde uchaguzi. Ni haki yao, lakini hebu fikiria, ukiondoa utawala wa awamu ya kwanza na wa pili, CCM imetuongoza kwa awamu tatu tangu kuanza kwa vyama vingi vya siasa, tumeona madhaifu yao, tumeona mazuri yao, basi tuwapeni na Wapinzani wafanye yao, tutalinganisha baada ya miaka 5 watakayoongoza.

Hatuwajaribishi maana hawaingii kubadili kila kitu, watakuta polisi ipo, mahakama, jeshi, Bunge, shule, vyuo, nk, maana yake wanaposema watafanya tofauti haimaanishi wataanza mwanzo Bali wataboresha baada ya miaka 5 tutawapima.

Kwakuwa CCM ina nguvu na pesa nyingi, baada ya miaka 5 mtatumia kila njia kurudi madarakani endapo upinzani utashindwa kutimiza yale waliyoyaahidi.

Ewe kijana, baba, Mama tuuchagueni upinzani. Kubaki na CCM au kuchagua upinzani haimaanishi tutagawana hela mifukoni, tutafanya kazi Kama siku zote.

Tuungane, tusiwadharau upinzani maana hatujawahi kuwapa nchi tukayaona mazuri na madhaifu yao.

#MakeTanzania great again
Kuichagua ccm ni kuridhika na umsikini ulionao
 
Hivi mbona watawala watangulizi hawakupenda kusifiwa hivi. Kwa nini utawala huu unataka na kung'ang'ania sana kusifiwa. Hivi hii ni nini sasa! Kuna nini? Yaani ushamba uliooneshwa juzi wa kuita wasanii na kutumia fedha zote hizo wakati mama zetu huku mavijijini hawana dawa na wanajifunika mashuka ambayo ni vitambaa walivyopewa na CCM ni ushamba kweli kweli.
Tafuta kitabu kiitwacho" Dictators mind" kimeeleza kila kitu.
Ukiikosa sifa utotoni utaitaka ukubwani
 
Kwa maneno haya nimegundua kuwa watanzania hawajui umuhimu wa upinzani na wataendelea kutawaliwa na ccm mpaka watakapofunguka akili zao. Wasomi wa Tanzania bado sana fikra zao.
Chadema tangu kianzishwe kina zaidi ya miaka 20 lakini hawajajenga ofisi ya makao makuu ya chama licha ya kupata ruzuku ya bilioni tatu kila mwaka! Hao ndio unataka tuwape nchi waongoze. Kama wameshindwa kujenga ofisi ya makao makuu ya chama tena kwa faida yao wataweza kweli kukuletea wewe maendeleo?
 
Kuna Mambo yanaumiza Sana hasa unapoona kijana au mzee akipinga wazi wazi upinzani usishinde uchaguzi. Ni haki yao, lakini hebu fikiria, ukiondoa utawala wa awamu ya kwanza na wa pili, CCM imetuongoza kwa awamu tatu tangu kuanza kwa vyama vingi vya siasa, tumeona madhaifu yao, tumeona mazuri yao, basi tuwapeni na Wapinzani wafanye yao, tutalinganisha baada ya miaka 5 watakayoongoza.

Hatuwajaribishi maana hawaingii kubadili kila kitu, watakuta polisi ipo, mahakama, jeshi, Bunge, shule, vyuo, nk, maana yake wanaposema watafanya tofauti haimaanishi wataanza mwanzo Bali wataboresha baada ya miaka 5 tutawapima.

Kwakuwa CCM ina nguvu na pesa nyingi, baada ya miaka 5 mtatumia kila njia kurudi madarakani endapo upinzani utashindwa kutimiza yale waliyoyaahidi.

Ewe kijana, baba, Mama tuuchagueni upinzani. Kubaki na CCM au kuchagua upinzani haimaanishi tutagawana hela mifukoni, tutafanya kazi Kama siku zote.

Tuungane, tusiwadharau upinzani maana hatujawahi kuwapa nchi tukayaona mazuri na madhaifu yao.

#MakeTanzania great again

Bandiko lako lina mantiki sana sema tatizo tulilonalo na upinzani ni kwamba wamedhamiria sana kuingia Ikulu kiasi kwamba wanasahau kitu ambacho ni cha muhimu zaidi kuliko wao kuwa Ikulu. Mtazamo wangu katika kuhakikisha Upinzani (ACT Wazalendo CHADEMA nccrmageuzihq et al) unakishinda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulitakiwa uanzie chini kuja juu.

Hakuna kitu kinakera na kuumiza kama kusikia Wabunge wa CCM wakigonga meza kupitisha sheria na kanuni kandamizi kutokana na wingi wao Bungeni. Hakuna kitu kinaumiza kama kushuhudia kwamba muhtasari wa uendeshaji nchi unaamuliwa kutokana na wingi wa Wabunge wa Chama fulani badala ya kufikiria Wananchi, ambao ndio maamuzi ya wachache walio wengi yanawaathiri moja kwa moja.

Mpaka siku tutakapoamua kuanzia chini, Upinzani utaendelea kubaki kuwa ni 'pacemakers' katika kila chaguzi Tanzania.
 
Nchi sio sehemu ya MAJARIBIO ... narudia TAIFA sio mahali pakujaribia ...Wakajaribu kwenye umeneja wa ma club ya usiku
Ni kweli na kama wanataka kufanya majaribio basi waanze kujenga kwanza ofisi ya makao makuu ya chama chao, haiwezekani chama kina zaidi ya miaka 20 tangu kianzishwe lakini hakina jengo lake licha ya kupokea ruzuku ya bilioni tatu kila mwaka!
 
Mkuu Pazia 3, kwanza asante kwa bandiko hili. Kiukweli bandiko lako ni la ushauri kwa Watanzania, tufanye majararibio ya kuwajaribisha wapinzani kwa kuwapa Ikulu yetu ili tuone watafanyaje!.

Yaani when you have two options, moja umeona deliveries ya mazuri ya alichofanya, na yanaonekanika, halafu mwingine hana lolote la kuonekanika, lakini ana ahadi tuu, hivyo unatushauri tuache kumchagua aliye deliver, mazuri ya kuonekanika na badala yake tumjaribishe mwenye ahadi ili kuona atafanya nini?!. Huku sio kuchezea shilingi chooni?.

Yaani unawashauri watu waache mbachao, kwa msala upitao?. Mimi nawashauri watu humu, katu, usikubali kamwe, bura yako njema, kuibadili kwa rehani!.
P
Mayalla unashauri tusijaribu kuionja sumu!
 
Chama kilichoshindwa kupanga tu miji huku kila siku nchi ikizidi kuharibiwa kwa kujengwa hovyo na kuwa takataka kwa ni I tukirudishe madarakani?

Ukwel ndio huu, CCM haipaswi kabisa kuendelea Kuongoza Tanzania. Tunaitaji chama mbadala chenye sera mbadala chenye maono tofauti kwa mustakabali wa taifa letu.
Chama gani unachohisi kinaweza kuwa mbadala w CCM? Hawa ambao mnadai wananuliwa? Km wanaweza kuuza utu wao tukiwapa nchi si ndio tutauzwa sisi pamoja na wao?
 
Mkuu Pazia 3, kwanza asante kwa bandiko hili. Kiukweli bandiko lako ni la ushauri kwa Watanzania, tufanye majararibio ya kuwajaribisha wapinzani kwa kuwapa Ikulu yetu ili tuone watafanyaje!.

Yaani when you have two options, moja umeona deliveries ya mazuri ya alichofanya, na yanaonekanika, halafu mwingine hana lolote la kuonekanika, lakini ana ahadi tuu, hivyo unatushauri tuache kumchagua aliye deliver, mazuri ya kuonekanika na badala yake tumjaribishe mwenye ahadi ili kuona atafanya nini?!. Huku sio kuchezea shilingi chooni?.

Yaani unawashauri watu waache mbachao, kwa msala upitao?. Mimi nawashauri watu humu, katu, usikubali kamwe, bura yako njema, kuibadili kwa rehani!.
P
Huwa naumia sana kuona MTU mwerevu anaposhadadia upumbavu kwajili ya tumbo lake..hicho ulichokitoa ni upumbavu wa kiwango cha stiglerz
 
Uliko bado uko kwenye kibovu cha baba yako kamuulize shangazi yako atakuambia
Acha matusi haya hayatamsaidia Lisu kushinda!

Je kuna mtu alienda ccm kuchukua forom akanyimwa?
 
Back
Top Bottom