RESOLVED HOJA Ushauri wangu: Mabasi ya abiria ya mikoani yaishie Mbezi Magufuli

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
👊
 
Define city centre kwanza, kama ni huku Mjini kkoo, posta etc hayaruhusiwi kuingia Muda wa kawaida ni asubuhi Sana ama usiku, unless ni mabasi ya kimataifa.

Ukipanda Ratco Kariakoo mchana unakutana na Costa ambayo itakupeleka mbezi ukapande basi.

Mabasi ya kimataifa yanayokwenda Mombasa, Nairobi, Kampala etc yanatoka Direct Mjini bila kupitia mbezi, yakifika ubungo wanakata mawasiliano kutafuta Tegeta.

Foleni haitakomeshwa kamwe kwa kulimit magari ya public kama hayo. Basi kama Hilo linabeba watu 40-60 wakimwagika mtaani hao kila MTU akichukua Bolt, bajaji, boda etc wanasababisha foleni kubwa kuliko ukiwakusanya wote kwa pamoja.

Long story short usafiri binafsi ndio husababisha foleni, kila MTU akitumia kifaa chake binafsi foleni ni kubwa, Uchafuzi mazingira mkubwa etc. cha muhimu usafiri wa Umma uboreshwe, mabasi yaongezwe, mwendokasi ziwe nyingi, Daladala ndogo zitolewe ziwekwe kubwa Tu zenye Nafasi, waweke daladala premium if possible Ku encourage watu wasitumie usafiri binafsi.
 
Ipo zaidi ya kilomita 30 Kutoka kati kati ya jiji?

Hii si saw na haikubaliki ikiwa lengo ni kuongeza na kurahisisha huduma.

Kama stand Moja ni dawa, mbona mwanza ina stand mbili?

Issue ni huduma.
 
Magufuli ana deserve recognition, mbona mlishindwa kujenga awamu zilizopita
Unafikiri kukikiwa na ulazima wa kujenga Uwanja wa ndege Chato, Ikulu kubwa Dodoma au stendi ya mwendokasi jangwani kwenye mafuriko ili navyo tulazimishe vitumike kama unavyolazimisha "main" terminal yako ya Magufuli kutumika??
 
Itakuwa ni ajabu sana kama mji ukikosa sheria za Zoning kila mtu anajifanyia anavyotaka , sasahivi stand za ma bus zipo kila kona ya jiji inachukiza sana na ni kero , nimefurahi umesema serikali iboreshe public transport , ila linapokuja suala la sehemu ya kupakia na kushushia abiria iwepo sehemu moja maalum.
 
Unafikiri kukikiwa na ulazima wa kujenga Uwanja wa ndege Chato, Ikulu kubwa Dodoma au stendi ya mwendokasi jangwani kwenye mafuriko ili navyo tulazimishe vitumike kama unavyolazimisha "main" terminal yako ya Magufuli kutumika??
Ni kweli ujenzi wa uwanja wa chato alifanya faulo hilo nakubaliana na wewe , na wale waliojenga parking ya mwendokasi walizingua , ila kwenye ujenzi wa Kituo cha mabasi cha Mbezi , magufuli nampa Big up alikuwa na mawazo mazuri sawa na walivyojenga bandari kavu pale kwala

Ungejua mapato ya serikali yanayopotea kwa Ma bus kushushia abiria nje ya Magufuli terminal ungesikitika , weka pembeni chuki na ushabiki wa kisiasa angalia manuufaa ya nchi
 
Shida kubwa itaanzia ile siku utakuwa miongoni mwa wamiliki wa mabasi ya kusafirisha abiria automatically utapingana na wazo lako
Nchi haiongozwi kwa matakwa ya mtu binafsi nchi inaongozwa kwa sheria , mawazo au matamanio yangu hayana maana kama yanapingana na kuhujumu maendeleo ya nchi
 
Hata Mimi pamoja na wasomi wengine tunataka ziwe hivyo kama zilivyo za airport au sgr,
 
Lakini mkuu si Huwa wanapita magufuli kulipa ushuru hatama wamezaja shekilango, au siku hizi hawapiti ?
 
Mizigo na watoto siyo sababu ya kuweka stendi katikati ya mji.
Wasafiri hujiandaa kwa safari, kujiandaa ni pamoja na kujiwekea nauli ya watoto na mizigo.
Stendi ya Magufuli pembeni kidogo kuna stendi ya daladala zinazofika jijini kote.
Hivyo hoja ya mizigo na watoto haina msingi.
Mbona watu wanatelemka na watoto pamoja na mizigo yao Airport na wanafika salama makwao!!
Hii stendi kabla haijafika hapo ilianzia katikati ya jiji, Kisutu, Mnazi mmoja na mtaa wa Msimbazi Kariakoo.
Kuhamishia stendi ubungo na baadaye Mbezi Nia ilikuwa kuondoa vurugu mjini.
Lakini leo kampuni kama Ratco, Tahmeed, Super Feo nk, wapo katikati ya mji wanasumbuliwa tu.
 
Ungejua mapato ya serikali yanayopotea kwa Ma bus kushushia abiria nje ya Magufuli terminal ungesikitika , weka pembeni chuki na ushabiki wa kisiasa angalia manuufaa ya nchi
Abira wangu wa Mtwara na Lindi 90% wanaishia Temeke na bus langu litaishia hapo hapo Temeke, siji huko stendi kuu Magufuli ili niongezee tu mapato, kama ni ushuru wa bus tutatuma kwa M-pesa.
 
Tozo na kodi zote zikatwe kwenye tiketi na stendi gari inazoingia. Kodi nyingine za mapato wamiliki wa magari wanalipa bila kujali gari inalala wapi.
Mbona inajulikana tozo zote huwa zinakatwa kwenye tiketi ndiyo maana abiria akiwa na tiketi hatakiwa kudawaida kiingilio stand
 
He he , wanafanya miradi ya ujenzi kwa gharama kubwa bila kupanga na kufuuta ramani na mipango miji ya kisasa,

Hata hizi flyovers, robo tatu zimejengwa kwa makosa ,zitakuja kubomolewa
 
Biashara ya mabasi waachien serikal, nyie wengine kimbilieni kwenye kilimo, cotton ginnery, viwanda vya kutengeneza sabuni na vinywaji baridi.. 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…