Ushauri wenu: Baba anataka kuuza mali, hataki kunigawia mimi mwanae

Ushauri wenu: Baba anataka kuuza mali, hataki kunigawia mimi mwanae

Bora auze tuu hiyo nyumba ndio inakupa kiburi cha kutotaka kutafuta kazi.
Tena namsifu sana baba yako kashaona mbali huenda mnataka kumuua au nyie kwa nyie mtakuja uana huko mbeleni.
 
Usishindane na mzee wako, hizo mali ni zake na yeye ndiye mwenye maamuzi.

Na mpaka ifikie hatua hiyo kukorofishana na mzee wako ukizingatia na umri wako inaonekana kuna mambo ambayo yalisababisha ambayo hujayaweka wazi.

Kiufupi TAFUTA MAISHA YAKO, WEWE NI MWANAUME, JILIPUE UANZE KUISHI MAISHA YAKO.

Ila usisahu bado ni wazazi wako na wakikuhitaji kwa namna yoyote itikia na uendelee kuwasikiliza bila kinyongo.

Sijawahi kufikiria mali za urithi hata siku moja na hili huwa nawaambia wazazi wangu kila wakianza kuzungumza maswala ya mali zao na utaratibu wa kuzitoa, nilishawaambia tokea awali hizo ardhi na mengine wapewe wadogo zangu mimi wasinifikirie kabisa.

Kujenga nitajenga kwenye ardhi niliyonunua kwa jasho langu. Pia huu utaratibu wa wazazi kulipia vijana wao mahari, nilishakataa kabisa, mahari nitalipa mwenyewe.

Nimeona mengi hasa katika migogoro ya kijamii kuhusu mali kipindi nipo mdogo nikaonaga solution ni moja tu, KUTAFUTA ZANGU MWENYEWE.

Mkuu fanya maamuzi, achana na mawazo ya mali za mzee wako, tafuta zako, na ukizipata utapata heshima ya kweli maana hakuna wa kuziongelea.

KUFA KIUME!!!

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
yaani kama una degree halafu una mentality ya kijinga namna hii kutegemea mali za wazazi wako ni bora hata mimi mwenye mswaki wa HKL lakini napambana kuitafutia vyangu
 
Ukisikia boya ndio hili. Sidhani hata Kama hili bwege Lina girlfriend.
At 39 bado unajificha kwenye sketi ya mama yako huku ukishabikia CCM? Eti chama chako, CCM wezi wa Kura ndio chama chako?
Jiunge na CHADEMA halafu njoo pm tukusaidie
 
Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu ya kazi, naombeni ushauri wenu maana nimeshikwa na gadhabu sana tangu siku ya jana.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 39, na kwetu tumezaliwa watatu tu mimi nikiwa wa kwanza, elimu yangu ni degree 1, baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikawa tu nyumbani kusikilizia mishe kama itatokea, kulitokea kutokuelewana na mzee wangu (hii nilishaielezea humu humu, baba hakutaka kabisa nimuambie mambo ya kujiunga na chama changu cha mapinduzi), akanitimua nyumbani, nikaenda kuishi kwa rafiki yangu huku maisha yakiwa magumu kweli kweli sijapata kushuhudia

Basi siku ya juzi nilimpigia simu mama kumuambia sijala nina siku ya 2, mama yangu alilia sana, nikamuomba aniombee msamaha kwa baba ili niweze kurudi kuishi kpale kwetu ila la kushangaza mama alipomuambia baba, mzee alikataa kabisa kuniona, ikabidi niende home jana kwa kulazimisha nimefika getini nikagonga alikuja mlinzi kunifungulia, alipo niona ni mimi akasema baba amesema asione uso wangu kwenye ile nyumba, nikamuambia nimerudi na hapa ni kwetu, kumbe muda huo baba anaangalia dirishani, alipo niona akatoka nje akiwa na nyundo, akaniambia nimeshakuwa mtu mzima asione kabisa pale, niliumia sana ndugu zangu, nikaona kama baba yangu amefikia kuwa na roho ya kinyama na kikatili wakati mimi pale ni kwetu, kukatokea mabishano makali sana siku ya jana.

Baada ya mabishano ya kama dk tatu sikuamini masikio na maneno ya baba yangu, alisema hivi: "wewe mbwa sikutambui, haujielewi mbwa mkubwa wewe, ndio maana kwenye urithi wangu sijakuweka na mwezi huu wa sita nauza mali zangu nawagawia ndugu zako sehemu ya pesa wakaendeleze maisha yao huko walipo" wakuu hii kauli imeniuma mnoo

Wakuu naombeni ushauri wenu, huyu mzee nataka nikamshtaki mahakamani maana mimi ni mtoto wake mkubwa na tumefanana mnooo. Mimi nilipaswa nikabidhiwa sehemu ya mali, wakuu sipati usingizi kabisa, nahisi kuchanganyikiwa kabisa, huyu mzee nataka akakae hata jela miezi mitatu ili aweze kuona uchungu wa kugawa mali kwa upendeleo

Kuna rafiki yangu alinipa option ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili niweze kumkamata mzee kila nitakachoongea aweze kukubaliana na mimi

Nachukua kwanza maoni yenu wakuu.

Karibuni.
Miaka 39,elimu degree unataka mali gani tena?
 
Baba yako anakupenda na anataka uwajibike ili uanzekujua kutafuta vya kwako so acha kulialia haitokusaidia, tafuta vya kwako ebooo!
 
Pale nyumbani sio kwenu, ni pa baba yako na mke wake ambaye ni wewe. Sehemu ya urithi wake alishakusomesha wewe.
Je, hiyo mali akiuza then aongeze mke alipe na mahali, utaendelea kung'ang'ania hiyo chombo ya mzee?
 
achana nae.
Fanya mambo yako.ila siku ukifanikiwa MSIJUANE.
Kwani wanachelewa hao kuumwa na kuanza kuwatafuta watoto wao wawasaidie
 
mkuu uyu mzee sasaivi nahisi ametawaliwa na roho mbaya sana, nataka nipate na mimi maali siwezi kubali jasho langu lipotee mkuu.
Jasho lako hapo ni lipi wewe kijana?

Yaani mali atafute dingi wewe useme ni jasho lako! Aisee vijana tunakwama wapi!

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Hapana mkuu mimi sina shida yeyote, pale ni kwetu mkuu na nina haki ya kupata mgao sawa sawa
Naamini inaweza kuwa chai ya hii,, lakini kama unafikisha ujumbe kwa mtu umfikie vizuri,,mtu wa namna hii background yake haikujengwa vizuri,, kwa umri huo unakomaa na mzee bado? Wewe utaacha urithi kama uko namna hiyo?? Mshukuru mzee wako amekuvumilia sana na anajitaidi sana kukuonesha kuwa wapaswa kupambana kivyako update za kwako,,
Kazi zipo nyingi mfano saidia fundi ujenzi,,ukonda,,kuendesha bajaj,,pikipiki n.k

Pambana na kutafuta zako achana na za Mzee
 
[emoji16][emoji16][emoji16]Hivi si ndo wewe ulienda kuishi kwa rafiki yako, alafu upo kwa watu ukawa unataka uheshimiwe kama wewe ndo baba mwenye Nyumba? Ukawa unalalamika kuwa mama mwenye Nyumba anamchemshia tu mume wake maji ya kuoga lakin wewe hakuchemshii?
 
Ikiwa haya ndio mawazo ya mwanaume ambaye anatuaminiwa baadae kuja kuiongoza familia ndio maana wanawake wanapigania usawa.....
 
Hili tatizo kubwa aisee.lakini yote haya mara nyingi yanatokana na malezi mtoto aliyolelewa.
Hivi mfano mimi naona kabisa Mali za urithi hazinihusu,pengine hakuna hata cha kurithi kabisa nitagombana na mzazi kwa lipi Sasa,alivyonilea vya kunilea inatosha sana tena mkuu umesomeshwa mpaka hata hapo ilitakiwa uwe na njia tayari japo kwa ni kweli maisha yamekuwa changamoto sana ila sio kwa kulazimisha Mali za watu ukaroge sijui mahakamani ni upuuzi tu.
 
Nakumbuka uzi wako boss[emoji23]

Hivi bado unapigania urithi..Serious?

Ondoka hapo nenda kapambane upate zako jamii itakuheshimu..Duniani usipokuwa na akili + mali ulizopigania mwenyewe utanyanyaswa sana usiku + mchana

Ni hayo tuu Mr Kikohozi
Nimepitia nyuz za huyu jamaa nilichogundua ni comedian tu Mara ana ml 20 Mara IST una ml 20 unakosa hela ya kula
 
Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu ya kazi, naombeni ushauri wenu maana nimeshikwa na gadhabu sana tangu siku ya jana.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 39, na kwetu tumezaliwa watatu tu mimi nikiwa wa kwanza, elimu yangu ni degree 1, baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikawa tu nyumbani kusikilizia mishe kama itatokea, kulitokea kutokuelewana na mzee wangu (hii nilishaielezea humu humu, baba hakutaka kabisa nimuambie mambo ya kujiunga na chama changu cha mapinduzi), akanitimua nyumbani, nikaenda kuishi kwa rafiki yangu huku maisha yakiwa magumu kweli kweli sijapata kushuhudia

Basi siku ya juzi nilimpigia simu mama kumuambia sijala nina siku ya 2, mama yangu alilia sana, nikamuomba aniombee msamaha kwa baba ili niweze kurudi kuishi kpale kwetu ila la kushangaza mama alipomuambia baba, mzee alikataa kabisa kuniona, ikabidi niende home jana kwa kulazimisha nimefika getini nikagonga alikuja mlinzi kunifungulia, alipo niona ni mimi akasema baba amesema asione uso wangu kwenye ile nyumba, nikamuambia nimerudi na hapa ni kwetu, kumbe muda huo baba anaangalia dirishani, alipo niona akatoka nje akiwa na nyundo, akaniambia nimeshakuwa mtu mzima asione kabisa pale, niliumia sana ndugu zangu, nikaona kama baba yangu amefikia kuwa na roho ya kinyama na kikatili wakati mimi pale ni kwetu, kukatokea mabishano makali sana siku ya jana.

Baada ya mabishano ya kama dk tatu sikuamini masikio na maneno ya baba yangu, alisema hivi: "wewe mbwa sikutambui, haujielewi mbwa mkubwa wewe, ndio maana kwenye urithi wangu sijakuweka na mwezi huu wa sita nauza mali zangu nawagawia ndugu zako sehemu ya pesa wakaendeleze maisha yao huko walipo" wakuu hii kauli imeniuma mnoo

Wakuu naombeni ushauri wenu, huyu mzee nataka nikamshtaki mahakamani maana mimi ni mtoto wake mkubwa na tumefanana mnooo. Mimi nilipaswa nikabidhiwa sehemu ya mali, wakuu sipati usingizi kabisa, nahisi kuchanganyikiwa kabisa, huyu mzee nataka akakae hata jela miezi mitatu ili aweze kuona uchungu wa kugawa mali kwa upendeleo

Kuna rafiki yangu alinipa option ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili niweze kumkamata mzee kila nitakachoongea aweze kukubaliana na mimi

Nachukua kwanza maoni yenu wakuu.

Karibuni.
Aisee....!
Mpaka leo kuna big babies,
Baba yako yuko sahihi, ninyi big babies lazima mukue na kupambana na maisha.
Umri wako inatakiwa uwe na mke na watoto, sasa wataka kuishi kwa baba.
SHAME!
 
Nilipoona tu miaka 39 nkafikiri hiyo 3 imekosewa labda ni 0, nkazoom kumbe ni 3 kweli, nkaishia hapohapo kusoma!

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom