Ushauri wenu Wakuu, Wahadhiri wanaoomba rushwa ya ngono wamemfikia mtoto wangu

Hii ya ku-appeal mkuu sina hata hamu nayo. Walimu wa department husika Huwa wanalindana ni ngumu kuchomoa hilo lilikuwa wazo langu la kwanza.
Mtoto semester ya mwaka Jana alisupp somo Moja tu. Na mwaka huu hii semester ni Moja tu na yote ni ya huyo mwalimu.
Vyuo vyetu hivi unakuta Kuna mwalimu semester ya kwanza anawafundisha somo Moja na semester nyingine kingine hii ni kawaida sana hasa vyuo vyetu hivi.
Ushaidi wa kumtia hatiani ndio tunautafta.
 
Mbona unapoteza muda wako na mhadhili fukara kama huyo.
Pesa ipo waziwazi, tena ndefu sana kila unapotazama muundo wa utawala wa Samia Suluhu Hassan.

Sahau maswala ya "uchawa"; hayo hayalipi tena siku hizi baada ya Samia kufanikiwa kunyakua uongozi kwa mabavu. Tazama vizuri humo ndani utapata sehemu ambayo itakupatia pesa haramu kama unayoililia wewe hapa.

Ni swala la kujuwa tu ni wapi pa kujipenyeza ili unufaike.
 
Kama hayajakukuta unaweza ukadhani masikhara, mdogo wangu mpaka alihama chuo na akapoteza mwaka mzima sababu ya walimu kama hawa.

Nachukia sana haya mambo ya rushwa ya ngono!
 
Stories za aina hii nazo ni za kuzisikiliza with an open mind. Sijawahi kusikia story kama hii kutoka kwa msichana mwenye uwezo mkubwa darasani.
Mimi ninayo ya mdogo wangu, top of class UDOM, mwalimu alimbully kwamba atamfelisha na alimtorture mentally mpaka akahama chuo na kupoteza a whole year. Amemaliza degree yake ya kwanza miaka kadhaa iliyopita top of her class na moja kwa moja akapata scholarship ya postgraduate nje ya nchi.

Kuna upumbavu mkubwa sana binti akiwa hajirahisishi kwa walimu huko vyuoni!
 
Huyu mtoto wangu amepitia hii changamoto mwaka Jana mpaka mtoto akatoa pesa bila sisi kujua,

Bahati mbaya tena mwaka huu mwalimu alikuwa anawafundisha pia amempa supp na ameahidi hachomoi mpaka ampe mapenzi, na inasadikika ameungua wakuu msaada wenu
Jina la Lecturer, chuo, faculty namba yake ya simu tumtumie Waziri Gwajima
 
Mkuu nakuelewa sana chuoni ukiwa na urafiki na wadada hata ue unaweza kupewa
 
Amrekodi na kumshitaki kwa ushahidi wa kumrekodi akiomba rushwa.

Amshitaki mitandaoni mpaka TAKUKURU.

Bila ya hivyo atampitia yeye na wengine wengi tu.
 
Muache ujuaji kwa kila jambo, hivi mnadhani Chuo mmeenda pekee?, hakuna asiyejua haya mambo yapo vyuo vyote hapa nchini, mpaka hivyo top 5 vina huu upuuzi.
Wewe umejifungia ndani ya gunia, wakati mimi nikikueleza hali inavyopaswa kuwa kwenye taasisi yoyote ya huduma kama hiyo..

Unashindwa kujuwa tatizo linatoka wapi; utaweza vipi kutoa ushauri wa ufumbuzi.

Hizo top 5 unazozungumzia wewe, sijui unazipa u'top' tokana na nini; kutoa digrii za heshima hata kwa watu vihiyo?

Tatizo siyo hayo mavyuo na wahadhili wake; ni uozo ulionea katika kila sehemu ya taifa hili.

Samia mtu mwovu ataanzia wapi kuwa kielelezo cha mambo mazuri yatakayofanyika kwenye hivyo vyuo.

Unalalamikia mhadhiri, halafu unashindwa kumlalamikia anayewezesha hali hiyo kuwa mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…