Ushauri wenu Wakuu, Wahadhiri wanaoomba rushwa ya ngono wamemfikia mtoto wangu

Muwekeeni mtego, upange vizuri muhakikishe anakamatwa live, anarekodiwa na kuwa exposed kwenye 'mahakama' ya umma via social media platforms likishachemka huko ndiyo lipelekwe mahakamani.
Nina binti ambaye yuko chuo so I understand what you're going through.
 
Kumbe umesoma saut 😂😂😂
 
Kwa nini wizara ya Elimu inashindwa kutuma wakaguzi wa serikali katika usahishaji wa vyuo?
 
Stories za aina hii nazo ni za kuzisikiliza with an open mind. Sijawahi kusikia story kama hii kutoka kwa msichana mwenye uwezo mkubwa darasani.
Kwahiyo wenye uwezo mdogo lecturers wanaruhusiwa kuwashawishi kingono ili wawafaulishe?
NB: Yapo pia malalamiko ya wanafunzi kufelishwa kwa makusudi huku uwezo wao kimasomo si mdogo.
 
Nendeni takukuru wamuwekee huyo msnngee mtego. Visa kama hivi takukuru wanapenda sana maana wanakaa sana ofisini bika kazi.
Tatizo hawa lecturers wanapenda sana mademu wakati mishahara midogo pesa hawana
Hakika kiongozi
 
Kwahiyo wenye uwezo mdogo lecturers wanaruhusiwa kuwashawishi kingono ili wawafaulishe?
NB: Yapo pia malalamiko ya wanafunzi kufelishwa kwa makusudi huku uwezo wao kimasomo si mdogo.
Sina maana hiyo. Ninamaanisha kwamba ukisikia story kama hiyo kutoka kwa mwanafunzi mwenye uwezo mdogo (especially baada ya kuwa ameshafeli somo tayari) kuna two possibilities: (1) inaweza kuwa story ya kweli na (2) inaweza kuwa story ya kutunga ili kufunika udhaifu wake!

So, don’t take everything at face value. You’ll be at risk of being dragged into an unworthy war!
 
Mie nimepita chuo, na visanga vya hivyo nimeshuhudia. Mie nilipitia kisanga kwa lecturer ila hakunitaka kimapenzi, ni alikua na chuki binafsi juu yangu, na aliniambia somo langu hutafaulu na hutafeli pia, kwa sababu uwezo wako uko juu, niliishia kupata alama ambayo hata sikutarajia.

Bas tyuuh.
 
Mwaka jana wife aliniambia binti wanayemlea familia nzima (ni yatima) anatakwa kimapenzi. Binti kidato cha pili, ila hii familia wana asili ya mashape na maumbo makubwa so unaweza ukahisi ni mkubwa.

Binti akamuambia mama mdogo mwingine, stori ikazunguka mpaka ikamfikia wife. Wakawa wanaogopa kuchukua hatua kwakua mtoto anaweza jikuta ananyanyaswa, kwahiyo wakamshauri binti avumilie.

Shule ikiwa inafungwa yule mwalimu akamuambia binti aondoke na gari linalowafuata wanafunzi wote ila ashuke center ili amkute hapo. Ikabidi afuatwe shule ili kuzuia hili swala.

Hii ishu ikanifikia mimi. Nikauliza jina la shule na jina la mwalimu nikatajiwa. Nikaomba namba za mwalimu wakagoma kunipa. Nikacheki na Afisa Elimu Sekondari wa eneo hilo akanipa namba ya mkuu wa hiyo shule, mkuu wa shule akanipa namba ya mwalimu.

Nikajitambulisha kwa mwalimu, nikamuelezea channel iliyonipa namba yake. Nikamuelezea ishu ambazo nimezisikia, nikamuambia siamini kama anafanya hivyo ila kama anafanya aache.

Nikamuahidi kwamba ikatokea anamuambia binti nimepiga simu au akamnyanyasa baada ya hiyo siku mimi nitamuibukia huko huko.

Yule binti akarudi baada ya leave, akatoa feedback mwalimu hamletei yale mambo na wala hamnyanyasi. Huyu ni binti ambaye siyo damu yangu, naimagine ikitokea kwa binti ambaye ni damu yangu nitakvyoenda kumkata mtu ngumi za kutosha.
 
Ni kweli unachokisema lakini sio mtoto wangu wa kwanza kulalamika ni wanafunzi wa kike wa huyo mwalimu wengi wamepitia hayo masaibu na anajinasibu kuwa anatafta wake akiwa darasani
Vyuo havina channels za kuripoti hizi issues? Kama kuna ushahidi wa texts, emails,classmates , marafiki etc na kama kuna wanafunzi wengine wamepitia hiyo, then mna strong case ya kukomesha hiyo tabia once and for all, msiachie hayo mambo ya kipumbavu
 
Tafuta takukuru chapu
 
Safi sana🔥🔥
 
Hongera kwa malezi mazuri ambayo yamefanya binti awe open kwako/ulikopata taarifa.

Ila naamini binti angekuwa amemuelewa lecturer isingefika kwako kuwa anapata sexual harassment.
I believe kuna some sort of flexibility mzazi anatakiwa kuwa nayo ili mtoto aweze kuqa free kumueleza mambo kama hayo. Hongera kwa hilo.

Suluhisho kwa lecturer mnaweza mkamchoma kwa takukuru au ukamtisha kwa namna inayofaa ili asidhuru na wengine. Ila suluhisho la kudumu ni kumjenga mtoto awe strong zaidi ya hapo kwa kuweza kupambana na aituations kama hizo mwenyewe ili hata usipokuwepo aweze kuzihandle mwenyewe. Kwa Afrika huku sexual harassments zipo za aina nyingi na sehemu mbali mbali kutokana na nafasi ya mwanamke kwenye jamii yetu.

My 2 cents✌️
 
Ushauri wa kwanza, ni kuangalia maendeleo ya Mtoto Kwanza , katika masomo yote na Hilo alilipata supu. Je Kwa ujumla anafanya vizuri au ndio spana mkononi.
Pili baada ya kufanya la hapo juu, ni kumpa mbinu ya kumwesha kushinda huo mtihani, bila kutumika.
Tatu kama kweli Mtoto anajiweza, ndio kuomba review Kwa Mwalimu tofauti.
Nne kuwa siliana na Chama cha wanafunzi kuona njia za kukabiliana na wa hadhiri WA namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…