Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Huyo katibu mkuu nae atakuwa siyo mstaarabu tu. Kusalimia watu kwake ni shida? Ni mmoja wa wale waliolewa madaraka.
 
hapana mkuu ,wakati mwingine wakuu zetu katika kazi huwa wanataka kujua kitu flani kupitia njia tofauti tofauti..mf
Mwaka 2013 huko kwetu ( ) kuna kiongozi mkubwa sana wa taifa hili alikuja sehemu kama mwananchi wa kawaida huku akiwa amevaa shuka za kimasai na kofia zile za pama..baadae sana baada ya kuondoka ndio ikajulikana kama ni boss wa taifa kaingia hapa.
Huyo katibu mkuu nae atakuwa siyo mstaarabu tu. Kusalimia watu kwake ni shida? Ni mmoja wa wale waliolewa madaraka.
 
Jamani Mimi Nina mwili mdogo halafu ni mfupi dharau ninazopitia duniani hapa huwa naishia kucheka.siku moja naenda kazini niko kituoni daladala inakuja ile naanza kuingia konda akanisukuma akasema kwa sauti sipakii mwanafunzi.nikambembeleza akanipakia nikatoa 200 na miaka yangu 30
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hahahahah pole mkuu nenepa kidogo
 

Mimi kuna 'Wajeda' Wawili hivi nakumbuka Siku moja nilikumbana nao 'Kichochoroni' wakiwa 'wamemkwida' Dada Mmoja hivi wa 'Kitaani' huku wakiwa 'Wanampiga' na Yule Dada akiwa 'anawatukana' Matusi makubwa makubwa tu. Na huyu Dada nakumbuka amekuwa 'akinipuuza' mno tu pengine kutokana na 'Ukapuku / Umasikini' wangu ( kama tuwajuavyo Dada zetu wa Dot Com Generation walivyo )

Baada ya Yule Dada kuanza 'Kuwatukana' wale 'Wajeda' nao sasa wakaamua kuanza kumpa 'Mateso' yao makali ya 'Kijeda' nikaanza Kumsikia Yule akianza 'Kujamba' bila utaratibu 'Maalum' na 'Kutapika' ndipo nami kwa 'Ujasiri' wangu mkubwa 'niliobarikiwa' nao na Mwenyezi Mungu 'Kiustaarabu' kabisa nikawaomba wale 'Wajeda' wasiendelee 'Kumuadhibu' ambapo kwa 'Kuhiheshimu' kweli wakaacha na nikaanza Kuwasomesha.

Sijui nina 'Hirizi' gani ya Asili ambayo hata kama nikikutana na Watu wenye 'Hasira' Kali nikianza 'Kuwaimbisha' tu upesi wanaanza 'Kulegea' kisha tunakuwa 'Marafiki' na Maisha yanasonga mbele. Nilipomaliza tu Kuwaimbisha wale 'Wajeda' nikasikia wanamuambia Yule Dada kuwa ana bahati Mimi nimewaonyesha 'Uungwana' japo ni Raia Mwema tu ila walichokuwa wamepanga Kumfanyia aliyekuwa akijua ni Shetani Lucifa tu pekee.

Cha 'Kushangaza' sasa baada ya Kumalizana tu pale na wale 'Wajeda' na Yule Dada ambaye mara nyingi alikuwa 'akinipuuza' alianza Zoezi la Kutafuta ninapoishi mpaka namba yangu ya Simu na alipofanikiwa akaniambia kwa aina ya 'Ujasiri' ule na 'Kumuokoa' Kwangu kule Siku yoyote ile nikiihitaji 'Mbunye' yake niseme ila nikamwambia ya kwamba huwa simsaidii Mtu kwa Malipo bali ni Utu wangu tu na kama ni 'Umasikini' nimeshauzoea.

Tuacheni 'Kupuuziana' na 'Kudharauliana' tafadhali kwani huwezi jua ni nani 'atakusaidia' au 'kukuokoa' hapa duniani na wengine wameshabarikiwa.
 
Hahahahah nimecheka kweli

Ila wanawake huwa wadhaifu sana na first appearance wanaleta madharau San

Hata Mimi ushawahi nitokea sana

Baadae huwa wanakuja kuwa washkaji[emoji1787]
 
Hahahahah nimecheka kweli

Ila wanawake huwa wadhaifu sana na first appearance wanaleta madharau San

Hata Mimi ushawahi nitokea sana

Baadae huwa wanakuja kuwa washkaji[emoji1787]
Heheh kwako ilikuaje mkuu?
 
Jamaa ilikuwa ndio zake anaibuka ghafla tu nyie hamjui

Halafu baadae ndio mnashtuka

Huya wa Sasa Hana hizo guts
 
Wanaume mnaolalamika wanawake wanawadharau, sasa, kama umevaa na kukaa hovyo unategemea nini?
Mbona hamshobokei wanawake walio hovyo kama ni kweli hamtilii maanani outward appearance? Mjitafakari
Kingine, inaonekana tunashida kubwa kwenye maadili yetu. Kwanini tunaambizana ya kuwa tunatakiwa tuheshimu watu wote kwasababu anaweza kuwa na kazi nzuri au unaweza kupata shida akakusaidia nk? Kwanini tusifundishane kuheshimiana kwa upendo kutoka moyoni kuliko kutishana? Hi ndio sababu tunakua wanafiki na chini kwa chini tunachukiana.
Mimi binafsi uwe muokota machupa jalalani au meneja wa wapi, nita watreat sawa bila kujali chochote. Ndio maana kwa watu wenye position kubwa au wanaotegemea special treatment kutoka kwangu wananiona nina dharau, ili hali wale watu wanadharaulika na jamii wananiona sina shida yeyote.
Kuhusu kudharaulika kwasababu ya muonekano wa nje, sijawahi. Sana sana watu wakiniona matarajio yao yanazidi hata uhalisia wangu. Lakini watu wengi, hasa wanaume wananiona nipo shallow kichwani (sexism). Wanahisi siwezi kufanya maamuzi magumu, kuchanganua mambo, kutetea hoja au kuwa na skills kwenye male-dominant fields. Wanahisi nipo kama pambo na nikiwaprove wrong kuna wanaofurahi na kuna wanaonichukia na kunipiga vitu kwa nguvu zao zote.
 
Kuna manager wa hotel fulani kubwa tu. Alitusimulia kuwa siku moja akiwa ndio manager wa zamu akaitwa na muhudumu wa mapokezi shida ikiwa kuna mgeni kachoka choka hivi lakini anahitaji room ya bei mbaya pale hotelini.
Sasa muhudumu wa mapokezi akamwambia mgeni mchovu angoje kidogo akamuonyesha na pa kupumzikia ili amuandalie hiyo room uku ikiwa ni kupata muda ili amwambie manager kuhusu kumpa chumba cha bei mbaya jamaa.
Manager kumuona mgeni alivyo ikabidi aende kuongea nae.mshtuko ukampata baada ya mager kujitambulisha jamaa nae akajitambulisha jina ndipo akajuwa jamaa ni footballer mkubwa tu duniani na jezi aliyovaa juu ni ya timu yake ya taifa.mara moja akapewa room bila hata maswali mengi.
 
nakumbuka kuna kidemu kilikua kinanidharau sana enzi hizo bush, basi nilivyomaliza shule pale kijijini nikaondoka kwenda Dar ikapitwa miaka 4 nikasikia kapewa mimba na aliyempa mimba nimshikaji niliesoma naye na alipewa mimba akiwa bado anasoma, basi kwakuwa jamaa nayeye alikua na ndg Dar ikabidi wakimbilie Dar es salaam kwa ndg wa mshikaji baada ya mwaka mmoja kupita ndipo wakashauriwa waende hospital kwa ajili ya kufanya uzazi wa mpango na hospital ilikua maeneo ninayoishi basi mshikaji ndg yake akamwambia nenda utamkuta rafiki yako uliesoma naye akuelekeze bwana weee

si wakaja mpaka home yule demu hakuamin kama ndiyo mimi aliekuwa ananidharau kule bush basi nikawasindikiza mpaka hospitalini kisha tukarudi nikawapeleka mpaka stendi yule demu nafsi ilimsuta sana mpaka aliamua kunitumia sms akisema kweli nimeamini usimdharau mtu ktk hii Dunia nilikuwa nakuchukulia poa poa kijijini leo unaijua mitaa ya Dar kiasi hiki na umetupeleka mpaka hospitali

aliishia kusema nisamehe, nami sikumjibu maskini.
 
Huyo katibu mkuu nae atakuwa siyo mstaarabu tu. Kusalimia watu kwake ni shida? Ni mmoja wa wale waliolewa madaraka.
Huwezi nilazimisha nikusalimie wakati wa kupokea huduma. Sio lazima kabisa wala haiongezi au kupunguza chochote.
Nikija customer care nahitaji huduma, salamu naweza enda shule ya msingi wakanisalimia watu zaidi ya 1000 na shida yangu isitatuliwe.
 
Huwezi nilazimisha nikusalimie wakati wa kupokea huduma. Sio lazima kabisa wala haiongezi au kupunguza chochote.
Nikija customer care nahitaji huduma, salamu naweza enda shule ya msingi wakanisalimia watu zaidi ya 1000 na shida yangu isitatuliwe.
Hakuna anaekulazimisha kusalimia. Lakini ustaarabu wa mtu uanzia hapo kwenye salaam. Ukisalimia utapoteza nini na utatumia masaa mangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…