Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

😂😂😂😂😂
We kaka upo dark ages au?
Umenichekesha mnooo. Sasa mtu kama wewe hatuwezi kulingana kwasababu nimekuzidi kwa kila kitu.
Na kama unataka kuniaminisha kuwa uanamke ni udhaifu, kanye ulale.
Eti mtu mzima una kuja hapa na hoja za vikojoleo 😂😂😂😂
 
Kuna footballer mmoja maarufu Sana aliwahi kucheza timu ya aseno(jina limenitoka) nadhani timu yake ya taifa ni Sweden.

Huyu jamaa, Kuna stories nilipata kusimuliwa Kuna siku alienda mgahawani huko kwao, Sasa alivyofika wahudumu hawakumtambua wakawa wanamchukulia poa. Kile kitendo kilimkera Sana, kwa hasira akaamua kuununua ule mgahawa fastaaa
 
Huwezi kumzidi mtu kwa kila kitu, tambua hilo
 
ishanitokea zaidi ya mara moja nahisi ni sababu ya mwili mdogo na wembamba pia sio mtu wa kuvunja kabati navaa kawida sana, ndevu hakuna na ki baby face japo nimekula chumvi.

Kuna siku ilikua fiesta wasanii na team ya clouds ilikua imefikia hoteli ambayo na mimi nilikuepo kuhudhuria sherehe ya ufunguzu wa kampuni fulani ya bima ambayo ni wateja wangu nawapa huduma fulani. Nilitoka mida ya saa 3 usiku kabla event kuisha, wakati nashuka chini naenda Launge kuongea na simu nawakuta ma chekibobu wa clouds akina Bdozen, Mchomvu na wengine wengi tu watoto wa mjini pale launge. nikawasalimia na kukaa ila hawakujibu na waliniona kama sio type yao.

Lahaula, kabla sijamaliza kuongea na simu naona binti kanirukia kwa nyuma na bonge la hug na mabusu ya shavuni na kulalamika nimemtupa simtafuti tena. Wale machekibobu wakashtuka macho yakawatoka, wakamuuliza yule dada vipi upo sawa akawajibu "am very happy nahisi hata show leo nitaperform vizuri". Kwa ufupi yule dada ni katika hawa wasanii wa kike wanaosumbua mjini kwa sasa na nyimbo zao na siku ile ndio alikua kati ya wasanii wa kutegemewa katika show. Kanakumbuka mchango wangu tangia kadogo kananifata kuniimbia akapela, nakakosoa na kumpa ushauri sasa am happy kanaishi ndoto yake.
 
Kuwa smart ni kama kipawa mkuu si kila mtu anazaliwa nacho. Kuna mwingine hana kitu lakini mara zote kapendeza.
Mwingine ana pesa & etc lakini kupendeza hajui. Yaani design ya wale wagumu wasiojali kuhusu yao.
Nina jamaa yangu toka shule yeye akipata tu sent anawaza akanunue nguo, saa etc. Muda huo me nikipata sent nawaza nikawanunulie pumba kuku wangu😂
 
Hii mambo iliwah nitokea nimetoka chuo na piga kaz na fundi mtaani.
Tuko na fundi mtaan tunapiga kaz kwenye nyumba ya mshua mmoja hv wa mambo ya ujenzi.
Asubuhi hiyo nagonga nyundo sana juu ya dari, fundi mkuu yuko chini na mama mwenye nyumba wanaongea kwa kilugha huku mimi nasikia baadhi ya maongezi yao kuwa "mwangalie fundi wako huko juu asije akaniunguzia nyumba yangu" na fundi akamjibu "haina shida ntaenda kuangalia",
Nilijisikia vibaya kwani kaz ninaijua vizur tu, pia fundi ananikubali kwenye kaz zenye utata lkn huyu mama alinidhalau sana na umbo langu dogo.
Kazi iliisha tukatimua na fundi wangu na ujira wetu mkononi, fundi mkuu alinieleza tulipo toka kuwa yule mama hakuamini kabsa kwenye kazi nikamjibu nilisikia alichoongea nikiwa juu.
Jion sasa yule mama alimwakia fundi kuwa kijana wako kaharibu kule juu anataka kumwunguzia nyumba yake, fundi mkuu akamwahidi kesho atakuja kurekebisha mwenye mama wa watu akapoa. Fundi alinipigia na kunijulisha hiyo inshu na tukakubaliana kwenda kesho.
Siku iliyofuata asb kama kawaida tukakutana fundi, ila fundi siku hiyo mtoto wake alikuwa mgonja hivyo alikuwa anafanya maandalizi ya kumpeleka hospital mtoto wake na hivyo mm kwenda eneo la tukio ila fundi aliniambia nimpe matumaini kuwa atakuja si muda kukangua kazi.
Nimefika site mama wa watu ananiangalia hovyohovyo tu, fundi yuko wapi? Yuko njian atakuja.
Nikaingia mzigoni sasa wala hata sikupanda juu ya dari yaani ni palepale kwenye main switch mchezo ukaisha , namwambia angalia vitu vyako vinafanya kazi? Akajibu ndio. Nikajua imemkaba hiyo na dhalau zke akidhani palipoharibika ni juu ya dari nipokuwa nagongagonga.
Nikawa zangu pale nje namsubili fundi aje maana hatukuwa na mawasiliano ya simu mpaka alipofika akamweleza nn kutokufika kwa wakat kwa kilugha, hao tukaendelea na shughuli zetu.
Nikamwacha anashangaa tu màana na fundi hakuangaika kukagua !
 
Kama nakuona vile
 
Mi kuna manzi mmoja katika harakat za kusaka tonge ikatokea tuna mawasiliano na yalikua strictly kikaz zaid cz wao walikua na ma distributor wa products flan hiv za security na mi nikawa moja ya wateja wao.
Sikua namjua kiundani na mawasiliano yetu yalikua nadra sana ile kikaz kaz na mazoea kwa mbaaaali.Status zake watsap na view na yy zangu anaziona.Kwakua napenda muzik basi alikua ananikosha kwa baadh ya vi clip anavyotupia mara moja moja sana navi comment.
Siku moja nikawa sina ishu kabisa job na niko bored na bahat mbaya sana akaweka status ilonivutia basi kama kawaida nika comment (yy zangu huwa ha respond japo hizo mara moja moja sana naziweka) basi aka respond finaly tukaanza kuchat.
Tukachat mara ujinga ukaingia humo ndani na u cant believe siku hiyo hiyo nikamgonga mzigo vizuuri tu kiroho safi.

SASA iko hiv,
Ofcz mm nilimchukulia poa kumbe hayuko hivyo.Anajimilikia ka usafir kake mwenyewe kazur tu (mi zangu daladala so mpaka nampanga akajaa nikajua na yy wa level zangu 😁😁😁). Mida tunakutana ndio nikalijua hilo,nikapiga mzigo na kwa aibu nikamshikisha 40k ila manka yule akazikataa kata kata.Nikaona oohoh leo nimepima vibaya kumbe na yy akanichukulia mambo safi hela ninazo asijue mimi ni bahili kishenzii 😂.
Sikua na mpango na game tena na yy akanitengenezea mazingira next week yake nikagonga tena.Ohoooh sijui alijua na leo nitapanda dau tena!!!!???. WAPII.
kesho yake akapiga mzinga nikachomoa..
Week ijayo yake akani set tena Shi 100 mfukon sina.
Kwa mara nyingine akani text "leo ninw hamu kitimoto, ningepata kilo 1 jion yangu ingeisha freshi." Nikaona isiwe kesi nikamtumia 5000- elfu 5 😊 bila ya kutoleo.AKANIPOTEZEA MAZIMA hata message za kikazi hajibu tenaa..

Baadae saaaana huko akajaga ni text, HUENDANI KABISA NA UNAVYOONEKANA. WW BAHILI SANA.

Kwa kifupi alinichukulia nina hela kumbe njaa tu 😆😆😆😆😆
 
Wakati mwingine unajitoa ufahamu kidogo ili kujua tabia za watu wako..
 
Katibu MKUU nae kilaza sana huyo
 
Wanawake walosoma na watumishi wana changamoto sana,wengi wao huachika baada ya kuolewa ndani ya miaka 10 ya ndoa....
 
Reactions: apk
[emoji23][emoji23][emoji23]Daah,buku tano bila hata ya kutolea
 
Usikute hata ni mnyakyusa
 
Sasa kivumbi uwe na mwili mdogo na mfupi, huaminiki hata kidogo.
 
Sasa kivumbi uwe na mwili mdogo na mfupi, huaminiki hata kidogo.
Mimi siyo mfupi ila mwili mdogo tu hata nikutanena mtu tuliyekutana naye miaka 15 iliyopita ataniambia yani niko vile vile. Nina mtoto wa kike watu uwa wanapata shida kuamini kwamba ni mwanangu japo bado mdogo wanahisi labda mtoto wa ndugu yangu. Hata shuleni walimu wake wasionifahamu uwa wanashangaa waakisikia ananiita baba.
 
Hahahaaa we ni kauzu zaidi ya mkuda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…