Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Sawa,,lakini kwanini yeye alihisi vumba unalo??..
Unajua pale kibaruan nafasi yangu ya kazi ilikua inanifanya mm ndio naonekana kama mmiliki as i was the main man front kupambana na hiv vimiradi vya hapa na pale (juz nili comment kwenye uzi wa "ulishawah tapeliwa na mtu wa karib yako" ).
Sasa nadhan na yy akapitiwa humo na mm nikapita naye
 
Nimecheka kwa sauti hakika! Walikomaje??
 
Basi huu uzi utakavyowasimanga wadada huu!!!
Sio kuwasimanga ndio uhalisia huo... Nakumbuka nilienda duka moja la dawa kubwa tu kuulizia dawa flani hivi.. nikafika nikamsalimia anaitikia kama hataki. Nikamuulizia jina la dawa akanitajia na bei ilochagamka kwa kweli, Kwa jinsi nilivokuwa nimevaa ni kawaida tu basi alidhani sitoweza kununua akashangaa tu nafungua mkoba nampa hela yake na ghafla akaanza kunichangamkia na mie nikampuuza tu

Sent from my Redmi 8 using JamiiForums mobile app
 
Naona simulizi nyingi za magari,wadada,hotel ,ATM nk chukueni hii ya kijijini!
Mwishoni mwa miaka ya 90' nikiwa mwanafunzi Udsm,nilienda likizo!
Nyumbani tunapakana na Taasisi moja ya Elimu ya Kati!
Jioni moja niliwatoa ng'ombe wakulima,wapate majani embeni mwa bara2 ili kesho wawe fit shambani!
Nilikuwa nilienda nyumbani navaa kinyumbani,jinsi iliyochoka kidogo,makata mbuga,mgolole wa kimasai ,fimbo ,kisu kitefu kiunoni, nkachukua Radio enzi nzile Rising Kama mkulima ( aisee RIP baba)
Basi wakapita wanachuo wakasikia nasikiliza kipindi Cha Mjadala Dw Saa 12 Jioni enzi Immune Kher na Othman Miraj mjadala ilikuwa Miaka Kumi baada ya Anguko la Ujamaa Afrika ipo Wapi!
Jamaa kuona Mara Ile wakaona huyu Mlugaluga hata haelewi kinachoadiliw!
Wakaanza kubwabwaja kwa Kingereza kibovu kuwa.. zisi poor,peasant is just deceiving himself listening to International radio,ili wapate muda wa kunisema walisogea wakiniambia nisiingize ng'ombe eneo la Chuo nikawajibu kuwa naijua mipaka!
Siku mbili baadaye kulikuwa na debate pale Chuoni kuhusu ,Demokrasia ya kiliberali na Mustakabali wa Nchi zilizokuwa za Kijamaa...kwa kuzingatia Azimio la Arusha! ...Walikuwa na Mwalimu mwenye upeo mkubwa Sana!
Basi yule Mwalimu kwa kutambua Moto wangu yangu Primary,Sekondary alinialika niwe mchokoza mada!
Nilienda nimevaa makatambuka vilevile na mojawapo ya yule aliyekuwa ananizidoa na ng"ombe wangu kumbe Ni Kiongozi wa Wanachuo na alikuwa Hightable!
Kimsingi walijuta kunifahamu!
 
Mm miaka hii nimeanzisha michezo ya kizungu. Nikiwa na mihadi na mtu nionane nae namuelekeza aje sehemu ya kulia chakula hotel kubwa kubwa nikifika kule naagiza kisosi kidogo cha mboga za majani au kikombe cha maziwa na yai moja la kuchemsha hapo najua hata 10K haifiki. Mda huo chai inachemka nachukua sim naanza kuchambua timu za kubet huku namsubiri best yangu aje. Basi wahudumu wanajuaga huyu jamaa mnyamwezi au kaishi sana mbele, kumbe nawaangalia wazungu Instagram alafu naigiza.
 
Ilikua Switzerland chief.
 
Na mm nikiwa o level huku NECTA ikiwa ina approach nilikuwaa nakimbiza hesabu alikuja jamaa mmoja sasa ni afsa wa jeshi ku reset pale school. Aliomba vpanga wa school ile ila alioneshwa mm nikiwa na kaumbo kadogo jamaa aliongea zarau kwamba huyu hana sifa hata ya kufanya necta...kilichofata alishangaa kila mwenye swali analeta kwangu..huyu jamaa baadae alikuja kuwa rafik mkubwa sanaa had leo na tumekuwa kama ndugu kabsa..na huwa ananipa deal za maisha hadi leo...NEVER UNDERESTIMATE PEOPLE
 
Kuna jamaa ni dalali wa vifaa vya electronic...!!hua anapita saana nnakofanyia biashara...!!sasa kumbe akikaa na madem anakejeli biashara yangu kuwa haina faida...!!napoteza mda tu

Wale madem kwenye story wakanambia...nkampotezea....!!

Siku moja nlihitaji kubadilisha flat ili ya geto ije ofisini...!!nkampa dili aipeleke kisha aje na ile ya zaman nnapofanyia biashara

Alikutana na mazaga geto ambayo ht kwake haana...!!aliporudi akakaa kmya ila akaenda kutubu kwa madem alowatangazia
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Umezingua sana ,kiini cha story ndiyo umekiacha pending, hebu weka sawa hapo ulipotambulishwa kwa staff kuwa ndiyo manager mpya ungemalizia tu yaliotokea
Kaacha kiini,inabidi jamaaa arudi aelezee vizuri kilichojiri
 
😂😂😂
 
Kuna siku mteja wangu kanipa oda ndefu kidogo nikamwambia namtuma kijana wangu alete na bodaboda jamaa akasema sawa nitaacha maagizo kwa mlinzi. Baadae nikaamua ngoja niende mwenyewe ili nionane nae mteja mkubwa. Nikafika getini mlinzi akanipeleka hadi ofisini kwa jamaa. Nikamsalimia akaitikia akaniwahi 'boss wako mgumu sana kwenye bei lazima atakuwa Mchagga ila namkubali sana amenyooka hana konakona' dah nilibaki nacheka sikumwambia kama ndio mimi akanikabidhi malipo nikaondoka.
Huyu mteja hatujaeahi kuonana hadi leo ni mwendo wa simu tu.
 
Aiseee,na wote wakapata adabu
 
walivyojichekesha ukarespond vipi?
Wale house mates walivogundua sikujali nilienda nao poa tu walijua huwa sijali mambo madogo na kuna jamaa mmoja nilimchukuaga kama sales officer maana nafasi hizo nilikua naajiri mwenyewe 1 year contract renewable na hakuniangusha akawa anafanya vizuri tu mpaka akagrow kuwa relationship officer
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] alikuwa hajibu salamu zako au..?
 
mimi nipo tofauti naheshimu kila mtu
 
Kuna dem niliwah kudate nae alikuwa na shangaz yake mchaga...!!

Shangaz alikuwa ananidharau mno kisa mumewe anafanya kaz maliasili n ukijumlisha sina kazi wa mishe(magu kabana)

Alipandikiza dharau mpk kwa dem....nae akaanza dharau kwa kigezo kuwa haoni kama nna future inayoeleweka

Tulipotezana kama miaka mi2...!!siku yule shangaz alokuja ofisin hakuamini....!!na yule dem nae akaja na hakuamin

Mpaka sasa yule shangaz kafungua biashara kama yangu....na ushauri wa biashara anafuata kwangu
 
mzee inaonekana wewe bishoo sana
 
mimi mwenyewe sinaga mambo ya kusalimiana na watu nisiowajua hata wasiponsalimia poa tu ila sasa watu watakuona una dharau kumbe ni vile tu hupendi shobo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…