Njiwadume
Senior Member
- Jun 13, 2020
- 139
- 343
Nakumbuka miaka 3 iliopita nilikuwa naend hom KANDA MAALUM. Huwa sina utamaduni wa kula njian sasa nilipofika Mwanza nikasema ngoja nipashe mchango wa tumbo nikachukua mchemsho wa sato na baadae kidogo nikachuku mishikaki..baada ya dakika kama 30 gari ikatembea...daaaaahh kufika magu tumbo likaanza kupiga miluzi nikasema ngoja nilikaushie..safari ikaendelea huku tumbo nalo linazidi tulipofika bunda eneo moja linaitwa DDH .gari ikawa inashusha watu nikashuka namimi nikamwambia konda naenda chooni na sitaki gari iniache kumbe konda kanisoma akanipa moyo tu isijari tutakukuta kwa mbele panaitwa nyasura.bahati nzuri mazungumzo yetu na konda kuna bodaboda waliokuja kupokea watu walinisikia bas wakasema choo ipo karibu nikapanda bodaboda nikaenda chooni na gari ikatimka..baada ya kutoka ndo nikajua kuwa hapa gari imeniacha..ikabidi bodaboda aanze kazi ya kuifukuzia gari...tulipata baada ya kama dakika 20.kufika ndani ya gari nikaona gari imejaa abiria hata sijui walipandia wapi..ikabidi konda anitafutie siti nyingine..kwakweli tumbo likivuruga huwa linapoteza ladha ya safari nzima