Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Nilikuwa nacheki interview ya Nancy alofanyiwa na Zamaradi, alishauri kuwa kama haujaolewa epuka sana mwanaume mwenye mtoto tayari. Nilimuelewa sanaaaaa.
Jamani me sikuiona hiyo interview, itabidi niiangalie. Nimekumbuka kuna members walisema ikitokea umeolewa na single faza; basi angalau awe na m(w)atoto wa kiume, akiwa wa kike jiandae vizuri zaidi.

Na mke akisema kuhusu mali tunasema ooh mbinafsi sijui anawaza tu mali kuliko utu. Sasa mtu ukope ili mjenge afu nyumba uje uambiwe haikuhusu wewe na mwanao, aseeeeeeeeeeeeee
 
Kupigwa mswaki kwenye ndoa kunauma Sana. Imagine unasubiri mechi kwa hamu halafu mwenzio anakataa dah hakuna mateso makali kama hayo. Huyo jamaa angekuwa anapasha hata kimoja kwa siku angekupunguzia machungu sana. Pole Masaidada ugwadu ugonjwa mbaya sana.
 
Ndiyo maana nasema hii kesi atafute watu wazima wanao jua hili suala atleast A-X if not Z.

Wataweza kumshauri kwa umakini saana. Wanaume tunabadilika kwa mambo mengi ambayo mwanamke hawezi kuyatarajia.

Hasa.
-Mali kama ulivyosema.
Suala la mali hata mimi laweza nibadilisha [emoji817]% kama mwanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani me sikuiona hiyo interview, itabidi niiangalie. Nimekumbuka kuna members walisema ikitokea umeolewa na single faza; basi angalau awe na m(w)atoto wa kiume, akiwa wa kike jiandae vizuri zaidi.

Na mke akisema kuhusu mali tunasema ooh mbinafsi sijui anawaza tu mali kuliko utu. Sasa mtu ukope ili mjenge afu nyumba uje uambiwe haikuhusu wewe na mwanao, aseeeeeeeeeeeeee
Shida kubwa hapa ni ubinafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heri ya Mwaka Mpya...Kwanza nianze kukupa pole kwa yanayokusibu katika ndoa yako na maisha Kiujumla,Napenda utambue kuwa wewe si wa kwanza kupitia hali hiyo hivyo jipe moyo kuwa yatapita na baadae itakuwa historia.

Naanza na Suala zima la jinsi ya kukabiliana na mume wako:Mume wako kwa lugha nyepesi na ya kueleweka ni mtu mwenye Gubu na mfuasi halisi wa mfumo dume.Kwa kuzingatia hayo watu wa aina hii ni wa Kuwapuuza na kutohifadhi maneno yao wasemayo maana mwisho wa siku utaishia kujiumiza na kujipa magonjwa ya Moyo.
Kuhusu uhalali wa umiliki wa Nyumba.

Japo hujatupa maelezo ya kina ila kwa haraka mkiwa kwenye ndoa mali yeyote inayochumwa hubakia kuwa ya Familia,hivyo relax hana mamlaka hayo kisheria ya kumuachia nyumba mtoto wa nje ya ndoa na akaacha familia yake ikitaabika(Angalizo neno langu si sheria ukizubaa na kumsikiliza kila anachokisema itakula kwako)

Usiogope na uwe na imani lakini pia nakushauri utafute marafiki wa kukupa faraja,Kumbuka Sala maana Mungu wetu wa mbinguni ndiye msaada pekee..naomba usiwe mnyonge nalo litapita na hata mapito ya kiuchumi unayopitia ni ya kitambo yana mwisho Pia

Usipuuze kutafuta washauri ila wasiwe vijana bali wazee wenye busara watakaokupa ushauri utakaokujenga.

Maisha ni yako yajenge,Maisha ni mafupi yafurahie.

Mnazareth!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole dada....niulize kwanza ndio yule nliyekutana mianzini zanzibar wakati upo internship?....by the way ukitaka kyachana naye kwa huo mzigo haki unayo kwrnye swala la kugawana mali...

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitaka kuchangia kama wewe maana mie ni muhanga wa issue kama hiyo nimemuachia nyumba mwanamke maana kwa sasa mwanamke akienda mahakamani mwanaume huna chako nikaona isiwe tabu kwa sasa naanza upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaunguza nyumba aiseeeeee.
Bora aseme hainihusu mimi ya watoto.
Lakini na mtoto pia kamtoa.
Kwanza si baba mzuri anabagua watoto wake mwenyewe.
masai dada fanya tu mpango uunguze nyumba
Jamani me sikuiona hiyo interview, itabidi niiangalie. Nimekumbuka kuna members walisema ikitokea umeolewa na single faza; basi angalau awe na m(w)atoto wa kiume, akiwa wa kike jiandae vizuri zaidi.

Na mke akisema kuhusu mali tunasema ooh mbinafsi sijui anawaza tu mali kuliko utu. Sasa mtu ukope ili mjenge afu nyumba uje uambiwe haikuhusu wewe na mwanao, aseeeeeeeeeeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani me sikuiona hiyo interview, itabidi niiangalie. Nimekumbuka kuna members walisema ikitokea umeolewa na single faza; basi angalau awe na m(w)atoto wa kiume, akiwa wa kike jiandae vizuri zaidi.

Na mke akisema kuhusu mali tunasema ooh mbinafsi sijui anawaza tu mali kuliko utu. Sasa mtu ukope ili mjenge afu nyumba uje uambiwe haikuhusu wewe na mwanao, aseeeeeeeeeeeeee
Haki haya mambo ni wito dear.
 
Ninaunguza nyumba aiseeeeee.
Bora aseme hainihusu mimi ya watoto.
Lakini na mtoto pia kamtoa.
Kwanza si baba mzuri anabagua watoto wake mwenyewe.
masai dada fanya tu mpango uunguze nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahhahaa ndo kama mbwai na iwe mbwai eeh? Ila hapo pa kumu-ignore hadi na mtoto wake mwenyewe ndo nachoka zaidi. Au kwamba anahisi huyo sio mtoto wake? ingawa mke ashasema wanafanana balaa. Hapa ni kujitafuta tu na kujipanga tena kiuchumi; kwa hizi dalili ni bora ajue kuwa huyo mtoto amejizalia mwenyewe so apambane tu kwa ajili ya mwanae.
 
Nilichojifunza kwa mwaka 2019...Njia sahihi na salama kwa mwanamke kuwa free kisaikolojia,kihisia na kimahusiano ni kuwa na uhuru wa kiuchumi..Inuka,pambana,fufua biashara yako then raha jipe mwenyewe(ila usiache kumtii coz ni mmeo...

Mungu akutie nguvu,ndoa zina changamoto sana yaani usipokuwa tough unaweza ukakimbia mchana kweupee
[emoji122][emoji122]
 
masai dada,

Pole sana dada! Heri ya mwaka mpya 2020
Suala la mumeo kukwambia nyumba ni ya mtoto linatokana na alichosikia either kutoka kwa marafiki zako au ndugu zako, huenda ikawa unaongelea sana hiyo nyumba na huenda ukawa unaongelea kwa mazuri hauna maana mbaya ya kuwa unaifikiria sana hiyo nyumba. Jitahidi uache kuongelea mali kwa mtu yeyote yule.

Kuhusu kukataa kufanya mapenzi after P nionavyo mimi either anakukomoa baada ya Kukereka aliposikia unaongelea sana mali au ana mtu nje. Endelea kumpenda na muandalie kila kitu kama zamani ila usiongelee masuala ya mapenzi kwa muda wa mwezi mzima au zaidi na uwe unapendeza mara kwa mara especially jioni ili awe anahisi unataka kutoka out, hiyo itamfanya asitoke au awe anatoka huku roho ikiwa juu juu kuwa na wewe unaweza kutoka muda wowote na uonyeshe uko happy!

Ongea na ndugu yake anaekuelewa zaidi kuhusu matatizo yake na onyesha kuwa bado unampenda na unaipenda ndoa yako.

Endelea kupenda mtoto wake na uwe unamuulizia maendeleo yake ya shuleni na likizo wasiliana na mama yake mtoto ili aje tena ku clear hicho kiwingu kilichojitokeza kuhusu kutompenda.

Wish all the best! Be patient kama umeolewa na mmasai huwa wako hivyo kuna ndugu yangu anateswa kama wewe na hapewi hata mia!! Jamaa huwa anaenda sokoni mwenyewe.
 
Back
Top Bottom