Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Sasa hapo cha ajabu nini??
Wewe na viporo wanakuita upashe, kuna mwenzio huku kashaniitia mpk ukoo wao wote na nimegoma.!

Kawajaza pesa wale maanko jau lakini wapi, kanisusia mpk ofisi tulioanzisha wote na kila kitu labda nitakubali lakini hamna kitu.!!
Na sitegemei kumrudia hata mbwa apige mswaki..!
 
Baba mkubwa alishaona pale hamna mtu
 
S2 episode 7


Nikawa nazidi kupata mawazo tu maisha yakaendelea na Rachel ila nikawa sina furaha kama zamani hata sex nikawa kuna muda nafanya basi tu, ila huyu binti bana sijui alikua na shida gani kuna siku nakumbuka sijui nilikua nimekunywa nini maana nikaanza tu kua mnywaji, hio siku tulisex muda mrefu sana nakumbuka baada ya kumaliza akaniambia "patrick, katika wanaume wangu wote sijawahi kupata mwanaume ananitia hivi"

Dah imagine unaambiwa hivo na mke wako, nilitamani nimnase hata vibao ila nikasema hapa hakuna mwanamke hapa nianze kuangalia tu namna ya kujichomoa pindi mtoto akizaliwa, kuna siku nikashika simu anayotumia maana nikawa simuamini sana yaani wale mabwana zake maana majina yalinasa kichwani kwangu wengi tu bado alikua anachat nao, wengi wanamlaumu kwanini ameamua kuolewa, na yeye ana wa entertain tu yani anakua kama anataka hataki kuwapa tena utamu, na sms hizo hafuti anaziacha tu imagine, basi bana mi nikakata shauri hapa mwanamke hakuna, na mahari siwezi kutoa tena



Kuna siku mama akanitumia sms "naona mmeenda kuoa huko kimya kimya na baba zako yatayokukuta mmalize wenyewe" basi nikaona haina maana nikaipotezea tu, maisha yakaendelea nashukuru Mungu mama yake Rachel alikua ni mama flani mpole ivi na ana hekima sana, hapo nilikua na uhuru naweza kupata muda nawatembelea, sikua na roho ya kwanini nilimsaidia kila nachoweza hata wadogo zake Rachel walikua wananipenda sana maana niliwapa chochote kila napopata nafasi.....


Siku zikaenda mimba ikazidi kua kubwa ikabidi nipange sehem nyingine nyumba kubwa zaidi ila hapo katikati nilipigwa matukio na Rachel mpaka akili ikakaa sawa,mara arudi saa 5, mara ukute kafunga tu ofisi hata kama ni mchana na haeleweki yupo wapi, kuna siku nilichukia ikabidi nimchane tu kuhusu hao mabwana zake akaanza kusema hayo yalikua maisha ya nyuma, nikamuuliza sasa mbona bado unawasiliana nao ye akadai wao ndo wanamsumbua, huwezi amini ila nikatokea kumchukia tu tukaanza kulala different rooms, hapo ndani kila mtu anarudi anavyotaka mi hapo wala sijali wala nini nachowaza tu baada ya mtoto kuzaliwa niachane nae


Ikapita muda siku akanifata analia mbona sijui namnyanyasa mi nikamchana tu tuwaze mambo ya mtoto we endelea na wanaume wako, akajibu sawa badae akatoka hio siku hakurudi kabisa na kesho yake, nikafanya udadisi nikagundua hayupo kwao wala kwa rafiki yake nikawa nashangaa tu huyu mwanamke ni jini au sasa na tumbo lote hilo yuko wapi..... Hapo kumbuka Mary naongea nae mara moja moja ila sikuwahi kumwambia kama huku nimeyatimba, na mama mkwe tunawasiliana safi tu wala sikuwahi kumlalamikia kama kuna shida


Muda ukaenda mpaka ikafika siku akajifungua nilimpeleka hospitali moja private alivyojifungua salama nikawachukulia mahitaji alikua na mama yake na mdogo wake wa kike mi nikaenda kazini, jioni narudi nakuta marafiki zake wadada wawili na wakaka watatu wamekuja kumsalimia, katika kutambulishana nikaja gundua kati ya wale wakaka wa3 wawili kati yao wamewahi kua na mahusiano nae kumbuka hapo majina ya kwenye zile sms yaligoma kabisa kutoka kichwani, nikashikwa na hasira tu nikauliza wanaruhusiwa lini wakaniambia kesho mi nikaondoka nikawaacha hospitali


Badae mama mkwe akanipigia anauliza mbona nimeondoka nikawaambia nina presentation ofisini kesho nimekuja iandaa, hapo nina hasira najiuliza huyu mtoto ni wangu kweli, nikaenda sehemu nikapiga mtungi badae nikamtumia rachel sms " kati yangu na hao jamaa zako(nikawataja kwa majina wale washkaji wawili ambao nilikua na uhakika washakua nae) nani baba wa mtoto? Maana naona kama siwaelewi vile??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…