PSL god
JF-Expert Member
- Nov 18, 2023
- 8,435
- 6,476
Mtani na wewe unaburudika na storyAisee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtani na wewe unaburudika na storyAisee
Njoo ukiwa na pajama yako tu nikusimulie vizuri nimesimamisha kusoma huku kuna ndefu nyingineNdefu mno
Aliyesimamisha kusoma anisimulie
Nini sasaAisee
Sasa hapo cha ajabu nini??Episode 11
maisha yakaendelea hapo nishabadili na namba za simu nikarudi kazini ila nikawa mlevi sana, kuna siku mpaka director alikua mmama mmoja hivi alinifukuza ofisini akaniambia we nenda kwanza mpaka kesho, barua za onyo nikawa nakutana nazo karibu kila wiki, Maisha yakaendelea nikaja kuona nikiendelea kufanya kazi dar sitapata amani ya moyo, nikaanza mipango ya kutafuta kazi sehemu nyingine kimya kimya nikaja kupata kazi mwanza ila nilitakiwa nisubiri kama miezi miwili ndo niripoti , sasa kuna siku nimekaa Mary akanipigia sijui hata namba zangu alipewa na nani, akanisihi sana tuonane nikamuambia sawa, basi badae tumeonana yupo smart kweli na kazini alirudishwa pale pale, akawa ananiambia twende ukachukue vitu vyako vilivyobaki, tukaenda home tukaishia kusex tu, mazoea yakaanza taratibu nikaona no this is not right nikamwambia tuache tutarudisha matatizo tu, nikaja kuamugaza naenda mwanza nahama huku, akakubali hivo hivo mpaka siku naondoka tulilala wote asubuhi niliondokea kwake
Mary kwa sasa ameshaolewa na ana mtoto mmoja, hua tunawasiliana sana yaani sana ila hatujawahi kuonana tangia hio siku naenda mwanza yaani hata nikiwa dar tulishakubaliana tusije onana kabisa, kuna siku nipo dar ananiita mikocheni huwez kuamini nilienda ila njiani roho iligoma nikarudi, hata leo hii nimetoka kuongea nae tunashauriana mambo mengi ya kimaisha
samirah ye bado hajaolewa na nina mawasiliano yake hua tunaishia kutaniana hapa na pale tu japokua nae sijawahi kumuona toka ile siku tunaachana akiwa bado chuo, 6 years ago!!!
Mimi sasa, mwanza ndo nikakutana na machizi wenzangu kwenye mapenzi nikapigwa matukio mpaka akili ikakaa sawa, ndo lengo la kuleta huu uzi ila muone kua niliacha wanawake wa aina gani na nikaja kutumbukia na kupigwa matukio na wanawake wa aina ipi, wanakuambia mkataa pema pabaya pamuita, hapa ndo sasa story inaanza rasmi wadau
Baba mkubwa alishaona pale hamna mtuS2 episode 6
Dah nilitafakari sana nikapata mawazo makali sana, nikawaza maisha na Mary kule dar, nikamuwaza Samira, nikawaza nimekuja kuingia kwenye balaa gani tena, uzuri napenda sana kua mtulivu kwenye situation za kupanic mpaka leo ndo niko hivyo, nikawaza sana nikajilaumu nimemtia mimba binti ambae simjui vizuri, mbaya zaidi nishaenda na kujitambulisha kwao, nikawaza sana kuhusu huyu mwanangu tumboni, badae mawazo yanakuja ni wangu kweli au? Yaani nikawa sielewi tu
Nikarudi home usiku kufika napokelewa sina hata furaha, nikampa simu yake akawa kafurahi kweli anasema ngoja nichukue na picha zangu za zamani,mi hapo namchora tu npo zangu kimya, kanipakulia nikamwambia tumbo linauma siwezi kula basi ananibembeleza hapo sina hata hisia wala amani mpaka muda tukaenda kulala, akataka tusex namuambia tu tumbo linasumbua, akaja pitiwa na usingizi, mi hapo siwezi kulala, huwezi kuamini kuanzia hapo nilipatwa na tatizo la kutopata usingizi mpaka leo linanitesa, nikaanza kumuangalia akiwa amelala, ni binti mrembo, nikaanza kuwaza zile sms, natamani hata nimnyonge!! Ila bado nawaza hiki kiumbe tumboni, au nimconvince atoe mimba nimpige chini, ntampa sababu gani, basi tu mawazo hayaishi
Nikatoka nikaenda sebleni nikamimina pombe nikaanza kunywa huko( mpaka leo nina utamaduni huwezi kukosa pombe kwangu hata kama sio za bei lakini lazima niwe na stock ndani)... Mawazo kama yote sielewi cha kufanya, sasa sijui kwanini nikawa namkumbuka sana Mary nikiwa nimelewa, Samira ikawa rahisi kumsahau labda kwa kua hatukua pamoja kwa muda mrefu, nikashika simu nikampigia Mary ikaita weee haikupokelewa, nikaachana nayo, nimekaa sebleni Rachel mara kanifata,
"Mume wangu mbona huku tena usiku na hio pombe na tumbo kulikoni"
Nikamwambia nina kiporo ofisini nataka malizia alafu nakunywa kidogo labda tumbo litakaa sawa, basi akaja pale ananibembeleza na nini hapo nawaza zile sms, nawaza ile clip yaani napata hasira basi tu, badae akarudi kulala nikawaza nikasema ntapata jibu tu hakuna haja ya kupanic
Kesho nikaenda kazini kama kawaida, natoka nikapita pale golini kwake nikampa hi tukawa tunapiga story tu pale, mara mezani nikaona ile simu niliyomrekebeshia nikamuulizia ulipata picha zako za zamani akasema ndio, basi nimekaa pale nikazuga zuga badae nikashika ile simu kuchungulia nakuta sms zote zipo tu kama jana, hajafuta hata kitu, moyoni nikasema huyu binti tofauti na umalaya mbona tena ni kama hamnazo, ni ujinga au kiburi? Yaani ushahidi wote wa ujinga wake anaacha tu na anajua naweza angalia muda wowote..... Nikajisemea moyoni... Karibu uswahilini patrick
Hasira zikapanda pale tena nikaaga nikaondoka zangu, mi huyo mpaka bar nikanywa kidogo nikakumbuka Mary alinichek sikumjibu ikabidi nimpigie, tukapiga story tu pale nikazuga nipo sawa wala hakuna shida yoyote basi badae nikarudi home siku ikaisha
Kumbuka hapo bado nadaiwa laki 3 kwa kina Rachel ambayo sikumalizia, nawaza hapo nipeleke au niachane nayo tu, nikawa najiona mjinga yaani mimi ndo naenda kulipia K ambayo watu washacheza nayo kiasi kile nikasema dah! Si niliacha K za maana dar nikakimbilia huku, acha nikome sasa
Ujinga sasa, badala kipindi cha mwanzo ndo ningeanza kumdadisi Rachel nikajikuta sa ivi ndo naanza kumhoji kuhusu maisha yake, ndo akaniambia baba yao aliwakimbia wakiwa wadogo, na yule mdogo wao wa mwisho ni mtoto wa baba mwingine, anadai baada ya kumaliza la saba hakuendelea na shule, na alipofikisha miaka 16 ndo akahamia kwa yule rafiki yake mwenye mgahawa akaanza kujitegemea, sasa nikawa namuuliza unajitegemea kwa kazi gani sasa akawa anajiuma uma akilini hapo najiambia patrick acha ujinga kwani majibu huna
Mama mkwe nae hapo alishakua free ananipigia simu tu tunawasiliana kama kawaida na nyumbani akawa anakuja freely tu, nikapanga siku nikaenda kumalizia ile laki 3 lakini safari hii nilienda na baba mkubwa(hakuwepo awamu ya kwanza).... Tukafika tukamkuta mama mkwe,Rachel na mzee mmoja safari hii hapakua na maongezi sana tukalipa ile pesa tukala pale maongezi kidogo tukaondoka
Tukapita mahali nikawa nimekaa na baba mkubwa mara from nowhere ananiambia
"Tatizo lenu vijana mnaharibu kwanza ndo mnakuja kutushirikisha, yule binti kama angekua hana mimba ningekushauri uachane nae tu"
Interesting..Nini sasa
Nimeshaimaliza. Jifunze kupitia hii storyMtani na wewe unaburudika na story
Mjifunze nyie msiotulia😀Weka neno Demi, weka neno 😄
Kina Mary walikuwa wa kulia lia, alihitaji wakakamavu kama kina Rahel, hata nyoka akikatiza ndani anabondwa..😁😁Ee si kija Mary uliwakataa recho ndio anakufaa 😂😂
Yaan na anajua kusimulia kweli 😂😂Kina Mary walikuwa wa kulia lia, alihitaji wakakamavu kama kina Rahel, hata nyoka akikatiza ndani anabondwa..😁😁
Wacha akili ikae sawa.
Sana.Yaan na anajua kusimulia kweli 😂😂
ChomoaNdefu
ImeumaAisee
NyokonyaSamira naye anakulaani🤣🤣🤣