Mie sijatetea ila nimesema ukweli ambao jamii haitaki kusikia,
Kuhusu suala la ushoga anayejua ni muhusika mwenyewe, wee usie husika deal na mambo yako binafsi,
Nashangaa sana ushoga ni jambo linalopingwa kwa nguvu zote, ila ni jambo linalokua na kuenea kwa kasi zaidi. Sasa pingamizi halifanyi kazi ipasavyo au ndo ngonjera za maneno tu na sio vitendo?
Mtu kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni matakwa yake binafsi na anatumia viungo vya mwili wake ambaye ndiye mwenye dhamana hiyo, wala hamuazimi mtu, na jambo hilo linafanywa faragha sasa kero za watu wasiohusika zinatoka wapi?
Kwa mantiki hiyo ushoga ni suala pana na mtambuka ambalo linapaswa kujadiliwa kwa kina na ufasaha sio kwa muhemko, vinginevyo ni upotevu wa muda tu.
Sorry kwa maelezo haya.