Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Kuna siku moja Shahrukhan (mwigizaji wa Bollywood)alikuwa ndani ya ndege anasafiri kiti alichokuwa amekaa alikuwa na mzee mmoja anasoma kitabu kwenye ile sehemu kulikuwa na Abili wengine baada ya kugundua kuwa wapo na Shahrukhan wakaanza kumshobokea mara picha mara wanaomba kusainiwa kama kumbukumbu baada ya watu wote kwenye lile daraja lao kulidhika wakarudi kwenye viti vyao mjomba Shahrukhan kuna kitu kikamshangaza baada ya kujiuliza akashindwa kuvumilia ikabidi amuulize yule Abilia aliyekaa nae vipi mzee we hutaki picha na mimi kama kumbukumbu yako yule mzee akamjibu kwani unajua umekaa na nani Shahrukhan akamjibu hapana sifahamu yule mzee akamtajia jina lake kumbe bwana yule mzee ni Mmiliki wa kampuni ya Tata Nchini India ikabidi Shahrukhan awe mpole kimoyomoyo nadhani alisema kumbe mi ndo natakiwa kuomba picha.NB:Acha Dharau kwa Mtu usiyemfahamu.
Huyo Mzee anaitwa Sir Ratan Tata. Ni tajiri wa Kufa mtu.
 
Mwaka huu mwezi wa 6 nlikuwa natoka dom nataka nipande sgr sasa bahati mbaya skujua kama bei zinatofautiana nkawa nmepungukiwa kama 20k.

Kila nikijaribu kutoa hela crdb ili kulipia ngoma ikawa inagoma ikabidi nimuombe msaasa kuna jamaa alikuwa anapita na track suit kama atakuwa na 20k kwenye tigo pesa baada kama ya nusu saa kuna mtu anaenda kwa wakala atamrushia.

Jamaa akaniangaliaaa then akaniluliza una uhakika nikamwambia ndio bas akanambia ila kama utarudisha muamala sawa. Basi akanilipia nkachukua no baada ya kama dakika 10 treni ikaanza safari kila mmoja akiwa behewa lake.

Nikiuempa no amtumie hela yake akanipigia kuwa kishamtumia na yakutolea.basi safari hyo moro haoo mara Dar hyo sasa tunashuka tumaelekea nje mara namuona jama mbele yangu.

Alikuwa amefatwa na magari kama 5 hvi ni mwendo wa saluti tu anapewa kimoyo moyo nikasema doh ningefanya uhuni yangenikuta.

Baada ya mda ndo nikaja kumjua kuwa ni mtu fulani yupo PT kupitia mkasa wa dogo fulani pale ostar toka sku hiyo nmekuwa na adabu na watu ote hata mwokota takataka
 
Yes, niliunganishwa na senior wangu kazi moja hivi ambayo alialikwa akaifanye yeye, na kwa namna ilivyokuwa nilikuwa naimudu vizuri sababu nishawahi kufanya zaidi ya hiyo

Sasa baada ya kufika yule jamaa kugundua mwamba kanituma mimi akaanza kuongea maneno ambayo hayakuwa mazuri kwamba ameletewa mtu ambae hajui kazi hivyo nitaharibu

niliifanya ile kazi kwa huzuni kidogo sababu mwamba hakunichangamkia hata kidogo na hata ule ushirikiano wa kawaida sikupewa kivile

nilimaliza kile kimeo kikawa fresh na wateja wake (yeye alikuwa kama cordinator) wakatumiwa ile kazi na wakaifurahia, sijui kama yeye aliiona au la

Fast forward miaka kadhaa mbeleni nikaapply Mchongo kwenye kampuni yao na nikapata kwenye kada tofauti na yake ila Mungu si athumani kumbe kile kitengo mkiwa na project mnakuwa wasimamizi halafu wale wengine wanakuwa watekelezaji

Siku ya kwanza tunapishana korido nilimsalimia akauchubua (sa sijui alijua dogo kaja kutafuta ajira au hata intern maana taasisi ilikuwa kubwa sio poa)

Mara ya pili hivyo hivyo

Siku alipagawa tunakutana kwenye fingerprint anabonyeza nami nabonyeza
Hajakaa vizuri tunakutana kwenye ofisi ambayo wanaingia wafanyakazi peke yao halafu na mimi nimo

Sijui aliuliza huko akaambiwa ajira mpya huyo tupo nae hapa, maana ilikuwa full aibu alinikazia for no reason na bado akaleta mikunjo

Mpaka kesho jamaa hajawahi kuwa na amani tunapokuwa pamoja hata tukipiga stori za kiofisi na staff wengine maana anajua siku niki-raise tu ile stori wana watamwona mchawi sana
Watu design ya huyo unatakiwa wewee uwe kauzu zaidi yake mtu akianza wewe maliza.
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
Unatangaza kituo gani cha Radio au TV?
 
Mwaka huu mwezi wa 6 nlikuwa natoka dom nataka nipande sgr sasa bahati mbaya skujua kama bei zinatofautiana nkawa nmepungukiwa kama 20k.

Kila nikijaribu kutoa hela crdb ili kulipia ngoma ikawa inagoma ikabidi nimuombe msaasa kuna jamaa alikuwa anapita na track suit kama atakuwa na 20k kwenye tigo pesa baada kama ya nusu saa kuna mtu anaenda kwa wakala atamrushia.

Jamaa akaniangaliaaa then akaniluliza una uhakika nikamwambia ndio bas akanambia ila kama utarudisha muamala sawa. Basi akanilipia nkachukua no baada ya kama dakika 10 treni ikaanza safari kila mmoja akiwa behewa lake.

Nikiuempa no amtumie hela yake akanipigia kuwa kishamtumia na yakutolea.basi safari hyo moro haoo mara Dar hyo sasa tunashuka tumaelekea nje mara namuona jama mbele yangu.

Alikuwa amefatwa na magari kama 5 hvi ni mwendo wa saluti tu anapewa kimoyo moyo nikasema doh ningefanya uhuni yangenikuta.

Baada ya mda ndo nikaja kumjua kuwa ni mtu fulani yupo PT kupitia mkasa wa dogo fulani pale ostar toka sku hiyo nmekuwa na adabu na watu ote hata mwokota takataka
Alivaa Jezi ya simba na pensi ya khaki?😂😂
 
Wakuu, habari za jioni,

Katika maisha, mtu anaweza kuwa na kariba ya kawaida kabisa kiasi cha mtu mwingine kutojua au kutozoea tabia yake, hali inayoweza kusababisha kudharauliwa. Hata hivyo, baadaye watu hao huweza kugundua kwamba mtu waliyemdhani si wa kawaida kabisa na mawazo yao yanabadilika.

Iliwahi kunitokea siku moja nilipoenda ofisi fulani na kuwakuta wafanyakazi wote wakiwa wanawake. Nilipowasalimia, mmoja tu alijibu, tena kwa nyodo sana. Nilipowaambia kwamba nilihitaji bahasha zilizoachwa na bosi wao, waliniangalia kwa dharau. Wakati huo, nilikuwa nimevaa mavazi rahisi—pensi na sandle—na waliniuliza, "Wewe unazichukua kama nani?" Nikajibu kuwa nimeagizwa, lakini bado walinidharau na kuniambia, "Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi."

Kumbe nilikuwa nimekuja na BMW nje ya ofisi. Walipokuwa wakijiandaa kuondoka, nikashuka ngazi na kwenda kwenye gari langu. Nilipofika kwenye eneo la kuegesha, walionekana kushangaa. Kwa heshima, nikawaambia, "Ingieni niwasogeze." Walikubali, lakini ndani ya gari walikuwa kimya kama wamemwagiwa maji. Walianza kucheka na kutabasamu huku wakifurahia upepo wa AC. Mmoja aliyekaa mbele aliniomba namba yangu ya simu, lakini sikufanya juhudi zozote za kuendelea mazungumzo naye, nikalipotezea tu.

Je, wewe umewahi kudharauliwa na watu, familia, au marafiki kutokana na mwonekano au hali fulani katika harakati za maisha?
Huu ni ujchi wa moto
 
Kuna jamaa nilisoma nae chuo kimoja na alikuwa mbele miaka miwili na tulikuwa tunakaa nae hostel chumba kimoja. Alipo maliza akaajiriwa Halmashauri moja huko kusini. Na mimi nilipomaliza nikaja kupata ajira kwenye kampuni binafsi ambayo ilipewa majengo na hiyo Halmashauri kama ofisi.

Sasa asubuhi moja nikiwa naelekea ofisini nikiwa nimevaa kisite site nikamuona jamaa nikamchangamkia ila jamaa hakunichangamkia halafu punde akawa anaongea na simu. Nikahisi labda atakuwa amenisahau ,basi nikasogea pembeni nikimsubiri amalize kuongea na simu halafu nimkumbushe. Lakini jamaa alipomaliza kuongea na simu hakunisogelea,alinipuuza na kuanza kuongea na wengine.Baada ya kupuuzwa nikajiondokea.

Basi siku zilizofuata akawa ananiona naingia ofisini. Akawa anataka kuniongelesha ila mimi nikakaza. Siku moja akaniongelesha na kujifanya ananifahamu, sikumpa ushirikiano kivile. Mpaka naondoka nilimchukulia kama mtu ambae sijuani nae. Ukiniletea dharau nakudharau zaidi.
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
hii inaumiza sana ndicho kinachonitokea,jina kubwa mfukoni hakuna kitu...inakata sana.
 
Nakumbuka mwaka 2006 tulikua na Meja General jirani yetu sasa ni marehemu na alikua Mkurugenzi Mkuu wa Costech enzi hizo, tulikua tunatoka Arusha kwenda Musoma via Serengeti .
Tukavuka vizuri geti la Ngorongoro, kufika Nabi geti ni saa 12 jioni, Walinzi wa gate wakatupiga mkwara kuwa hawafungui gate ,turudi Ngorongoro..
Meja General akawa ametulia kwa kipindi hicho alikua na cheo cha Brigedea , tukabishana nao yeye mzee ametulia tu kwenye gari ilikua Nissan Patrol- PLATE NUMBER ya shirika maaa alikua anatumia gari ya Costech kutembelea wakati wa liki, kama dakika 15 mzee akashuka kwenye gari akatoa kitambulisho.

Hiyo siku ndo nilijua watu wenye vyeo vya chini wanavyojua kupaparika, yaani Askari game alimwambia mwenzake kwa sauti fungua geti haraka tumekwishaaaaaaaa ni kama alitaka kujinyea saluti akawa anapiga hovyo hovyo tu kila Mara kwa kila mtu..
Hapo, "tumekwishaaaaaaaa" ni chai ya rangi.
 
Nilisema mimi ccm ni wapumbavu sana😁😁😁
 
Back
Top Bottom