Pre GE2025 Ushindi wa Boniphace Mwabukusi unatupa matumaini huenda 2025 CCM ikaondoka kwa kishindo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Huyu Mtu alishajipatia umaarufu kwa kupinga maamuzi ya Serikali kuingia Mikataba mibovu, kitendo cha kumuengua kugombea Urais wa TLS na hatimaye kushinda Rufaa ya kupinga kuenguliwa kulimuongezea umaarufu mara dufu.

Hili ni somo zuri kwa Serikali kwa kuwa wameona jinsi gani Watu ambao huwa Wapinzani wa Serikali hasa kwenye mambo ya hovyo yanayofanywa na Serikali jinsi wanavyopendwa, licha ya nguvu kubwa iliyotumika ili kumuangusha lakini "Mwamba"ameshinda.

Hongera sana kwake.
 
ni matumaini makubwa sana, wamba unaweza kuweka mamluki, ukatoa na funds ila wananchi wakatoa kura kwengine. aibu iliyoje.
 
Kwani lissu si alikuwaga raisi wa tls and what happened? Ccm kipo imara sana wapinzani wa tanzania bado sana ni kama vikundi vya vicoba
 
Sahau.
Fikiria kura 2000+ zimehesabiwa kuanzia saa 8 mchana hadi saa 4 usiku.
 
Too early, kama unadhani Nape was joking kama alivyosema, endelea kuamini kwenye mabadiliko, the determinant of victory kwenye matokeo ya kura za chaguzi zetu, is not the vote cast, but the vote count!, hivyo anaye determine mshindi sio mpiga kura wala kura zilizopigwa but muhesabu kura!.
Keep hoping!.
Hongera sana kwa Wakili Boniface Mabukusi.
P
 
Sielewi ulifuata nini kuwa wakili..a learned lawyer hawezi kusema upuuzi km huu! leo wameshindwa nini kufanya hiyo principle ya Nape! mnatishwa tishwa na vitoto vidogo kisa wana cover ya dola..woga wa aina hii ni laana kwa generation yako! ulienda shule kufanya nini? si bora ungezaliwa ukimbizane na swala kwenye mapori ya wahadzabe..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…