Pre GE2025 Ushindi wa Boniphace Mwabukusi unatupa matumaini huenda 2025 CCM ikaondoka kwa kishindo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hukumwelewa vzr tu...mko pamoja sana. Uchaguzi mkuu ni kitu kikubwa sana majizi ya kura ni ngumu kuyadhibiti kama kwenye uchaguzi mdogo wa TLS
 
Kwani lissu si alikuwaga raisi wa tls and what happened? Ccm kipo imara sana wapinzani wa tanzania bado sana ni kama vikundi vya vicoba
We Tumbili kaungane na ngedele pamoja na bundi kukata umeme wa SGR ili mabasi ya wakubwa yafanye kazi katika barabara ya Dsm moro na dosoma kima wewe
 
Tukipoteza woga wetu wanapoteza nguvu zao,
Huu ni msemo makini sana. Inafaa uujengee zege imara kuulinda

Uchaguzi huu wa TLS ni kielelezo muhimu sana cha mabadiliko yanayo kuja. Lakini ni muhimu sana kuchukua tahadhari kungali mapema, hasa kwa CHADEMA.
Maana ya matokeo haya ni kwamba CCM wametambua wazi kabisa kwamba siku zao sasa zimewadia. Kwa hiyo tusitegemee hawa CCM kuondoka bila ya mateke mengi.
Kwenye uchaguzi huu pekee, wamefanya juhudi kubwa kuzuia matokeo haya. Sasa nguvu kubwa watazitumia huko kwenye chaguzi za serikali za mitaa na kwenye uchaguzi mkuu. Kazi kubwa wananchi watakayo kuwa nayo ni kuzuia uchafu utakaonezwa miongoni mwao kubadili matokeo ya chaguzi hizo.
 
Hukumwelewa vzr tu...mko pamoja sana. Uchaguzi mkuu ni kitu kikubwa sana majizi ya kura ni ngumu kuyadhibiti kama kwenye uchaguzi mdogo wa TLS
Sikubaliani na wewe.
Chukulia Kila kituo cha kupigia kura kiwe ni kama mfano wa TLS, bado huoni uwezekano wa kuwabana?
 
Sikubaliani na wewe.
Chukulia Kila kituo cha kupigia kura kiwe ni kama mfano wa TLS, bado huoni uwezekano wa kuwabana?
Mkuu...hivi unajua jinsi( namna gani) waliiba uchaguzi wa 2020? Vyombo vya dola ndo vilishiriki ule wizi. Imagine mlinzi wa nyumba yako ndo anakuibia
 
Mwabukusi watu wana matumaini makubwa sana na wewe, usiwaangushe.
Dah!

Mbona unamtwisha mzigo mzito kiasi hicho. Unajua majukumu ya nafasi hiyo kweli?

Usije kumtwisha lawama ambazo hastahili kwa kudhani amepewa madaraka makubwa ya uamzi wa jambo lolote lile juu ya watawala.

Mpe ushirikiano katika maeneo aliyo na uwezo nayo; kama kuwafichuwa watenda maovu ndani ya serikali.
 
SINA MATUMAINI, MARGIN NI NDOGO SANA KUSHINDANA NA MTU WA CCM
 
Mkuu...hivi unajua jinsi( namna gani) waliiba uchaguzi wa 2020? Vyombo vya dola ndo vilishiriki ule wizi. Imagine mlinzi wa nyumba yako ndo anakuibia
Hakuna "chombo" cha dola hata kimoja kinachoweza kushindana na nguvu za wananchi. Kwanza Hicho unachokiita "chombo cha dola" siyo cha "dola", ni chombo cha wananchi wenyewe.
Kukosa ufahamu huu ni sababu kubwa inayofanya hivi vyombo vionekane kuwa vya kikandamizi. Hivi vyombo havipo kulinda uhalifu, vipo kuzuia uhalifu.
 
Mungu atamlinda na yale masheitwani mauaji !

God bless Mwabukusi in Jesus name. AMEN.
 
wananchi tukiamua kuzisimamia kura zetu mwanzo mwisho, kitaeleweka! tukiamua kuuweka woga pembeni changes will come, na mabafiliko ni maendeleo!
 
Nakuelewa vzr sana! Awareness ya sisi wana nchi ni ndogo sana. Lakini watu kama kina Kingai sio rahisi pia kukubali CCM ing'oke kirahisi.....! Kafara ya baadhi yetu kumwaga damu ndo suluhisho
 
Nakuelewa vzr sana! Awareness ya sisi wana nchi ni ndogo sana. Lakini watu kama kina Kingai sio rahisi pia kukubali CCM ing'oke kirahisi.....! Kafara ya baadhi yetu kumwaga damu ndo suluhisho
Ni rahisi kudai kafara, ngumu kujitoa kafara.
Are you ready to become a sacrifice lamb?
 
Mungu ashukuriwe sana!!! Kwa ushindi wa huyu Mwamba, kuna mambo mazuri yanakuja.
 
Cheo ni dhamana, hakuna cha mzigo mzito wala nini.
 
Kwani lissu si alikuwaga raisi wa tls and what happened? Ccm kipo imara sana wapinzani wa tanzania bado sana ni kama vikundi vya vicoba
Lissu alikuwa Rais kwa miezi mitano pekee yake Tena na hapo walimchukulia form tu yeye alikuwa yupo belgium kimatibabu na akaomba kujiuzulu kumuachia mwengine…………na ukumbuke nyakati hizo zilkuwa ni za Mwendazake so,ilikuwa ni ngumu sana kufanya siasa kutokana na kufungiwa kwa shughuli za kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…