Ushindi wa Lissu ni muhimu sana kwa wachaga wote, wachaga walihitaji sana kujinasua na ndoano ya kubambikwa uchadema.

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
529
Reaction score
1,150
Miaka 20 iliyopita ya harakati za kiasiasa za Chadema, ama niseme ilitokea kwa bahati mbaya au ni kushindwa kwa viongozi wa Chadema, wachaga walijikuta wamejeuka kuwa 'collateral' ya kuvishwa uchadema isivo halali. Na ikaonekana na wengi kwamba, Chadema ni chama cha wachaga na wachaga wote ni Chadema.

Hili kwangu ni jambo baya na ni moja ya kushindwa kwa uongozi wa Mbowe kuondoa huu uongo ambao watu wengi wamekuwa kuaminishana. Kwa sisi watu tunaotokea maeneo ya uchagani na hata mababu zetu walikuwa active kwenye siasa, hakuna historia kwamba wachaga waliwahi kukubaliana kwa umoja wao ku support chama fulani cha kisiasa. Siasa za uchagani zimekuwa ni za ki ushindani baina ya vyama vingi vya upinzani na Chama cha Mapinduzi.

Ukiachana na ule upepo wa Slaa na Lowassa mwaka 2010 na 2015, Chadema ni chama ambacho hakikuwa na ushawishi mkubwa nje ya eneo dogo la Moshi mjini na Machame kuzidi Chama cha Mapinduzi na vyama vingine kama NCCR na TLP ambapo naweza kusema walikuwa na ushawishi nusu kwa nusu. Ukienda Rombo napo utashangaa, Chama cha Mapinduzi kimekita mzizi mkali sana na watu wa kule wengi ni CCM. Maeneo ya vunjo napo hakuna historia ya kwamba ni Chadema.

Mfano mmoja tu, maeneo ya Kibosho na Moshi vijijini, hii sehemu haikuwahi kuwa ngome ya upinzani kwa miaka mingi sana, na kwa asilimia kubwa watu wa haya maeneo wengi ni CCM wahafidhina ambao wana mizizi kutokea kuanzishwa kwa CCM na hata wazee wengi walikuwa CCM kindakindaki mpaka leo hii.

Sasa huu uchaguzi wa Chadema, kwa wachaga wengi, tunautazama kwa wivu mkubwa, ushindi wa Tundu Lissu unaenda kufungua jela ya wachaga kuvikwa kwa nguvu taji la uchadema isivo halali. Naamini Chedema inapaswa kujivua gamba la 'uchaga' na pia inapaswa kuwavua Wachaga uchadema.
 
Wapambe wa Mbowe saa hizi wanamlisha uongo.
"Hao wanao piga kelele mitandaoni uachie kiti ni watu wa CCM. Ndani ya chama una watu wengi mzee. Utashinda tu usiachie uongozi"
Huku rohoni wanasema ukiachia uongozi tutakula wapi?
Hawa ndiyo aliwatabiri Nyerere wanaomshawishi kiongozi asiachie nafasi kwa maslahi yao binafsi siyo ya nchi au chama chake.
 
Aisee! Mmeanza kujadili ukabila, ingawa ni kweli kuna mstari mwembamba sana wa kutenganisha CHADEMA na ukabila, ila siungi mkono uchaguzi huu mambo ya ukabila yatajwe
 
Mbowe akafanye biashara nyingine amuachie Lissu kasababisha shida kwa vijana wafuasi halafu yeye anaibukia Ikulu
Hii hoja ni ya msingi sana, kuna watu wamejitoa sadaka ya damu kwa ajili ya Chadema, halafu mwamba huyoo kwenye kuridhiana huku vijana wafia chama wakiendelea kula rungu za ugoko. Kaguta amefeli sana kwa hili, ni uhaini ndani ya chama
 
Mnakolelekea sasa siko kabisa kuingiza ukabila katika hizi kampeni.
Mbowe asome alama za nyakati aachie nafasi kabla hajakivuruga chama na heshima yake zaidi ya sasa.
Kubwa ni hilo tu, wakati unamkataa bwana Kaguta. Wakati haupo upande wake kabisa
 
wamemjaza achukue fomu wakasahau kumuandalia na hoja za ni kwanini achaguliwe kuwa Chair kwa mara ingine. Watu wabaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…