Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Miaka 20 iliyopita ya harakati za kiasiasa za Chadema, ama niseme ilitokea kwa bahati mbaya au ni kushindwa kwa viongozi wa Chadema, wachaga walijikuta wamejeuka kuwa 'collateral' ya kuvishwa uchadema isivo halali. Na ikaonekana na wengi kwamba, Chadema ni chama cha wachaga na wachaga wote ni Chadema.
Hili kwangu ni jambo baya na ni moja ya kushindwa kwa uongozi wa Mbowe kuondoa huu uongo ambao watu wengi wamekuwa kuaminishana. Kwa sisi watu tunaotokea maeneo ya uchagani na hata mababu zetu walikuwa active kwenye siasa, hakuna historia kwamba wachaga waliwahi kukubaliana kwa umoja wao ku support chama fulani cha kisiasa. Siasa za uchagani zimekuwa ni za ki ushindani baina ya vyama vingi vya upinzani na Chama cha Mapinduzi.
Ukiachana na ule upepo wa Slaa na Lowassa mwaka 2010 na 2015, Chadema ni chama ambacho hakikuwa na ushawishi mkubwa nje ya eneo dogo la Moshi mjini na Machame kuzidi Chama cha Mapinduzi na vyama vingine kama NCCR na TLP ambapo naweza kusema walikuwa na ushawishi nusu kwa nusu. Ukienda Rombo napo utashangaa, Chama cha Mapinduzi kimekita mzizi mkali sana na watu wa kule wengi ni CCM. Maeneo ya vunjo napo hakuna historia ya kwamba ni Chadema.
Mfano mmoja tu, maeneo ya Kibosho na Moshi vijijini, hii sehemu haikuwahi kuwa ngome ya upinzani kwa miaka mingi sana, na kwa asilimia kubwa watu wa haya maeneo wengi ni CCM wahafidhina ambao wana mizizi kutokea kuanzishwa kwa CCM na hata wazee wengi walikuwa CCM kindakindaki mpaka leo hii.
Sasa huu uchaguzi wa Chadema, kwa wachaga wengi, tunautazama kwa wivu mkubwa, ushindi wa Tundu Lissu unaenda kufungua jela ya wachaga kuvikwa kwa nguvu taji la uchadema isivo halali. Naamini Chedema inapaswa kujivua gamba la 'uchaga' na pia inapaswa kuwavua Wachaga uchadema.