Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya nishati mpya wahimiza maendeleo ya Afrika

Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya nishati mpya wahimiza maendeleo ya Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1785811427116011167.jpg

Katika majira ya joto ya mwaka huu, sehemu kubwa ya eneo la kaskazini mwa dunia ilikuwa na joto kali kiasi kwamba katika baadhi ya maeneo barabara ziliyeyuka, misitu iliwaka moto, watu walipoteza maisha na hata kuyumbisha baadhi ya mifumo ya nishati. Hali hii imekumbusha tena umuhimu wa kuharakaisha utekelezaji wa sera zinazohusu nishati, ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.

Joto kali na madhara yake kwa binadamu, mazingira na miundombinu, vimekumbusha tena kuwa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ipo, inatuathiri na itaendelea kutuathiri. Pamoja na kuwa madhara ya mabadiliko ya tabia nchi hayajaonekana kwa kiwango cha kutisha katika nchi za Afrika kama ilivyo kwenye eneo la kaskazini mwa dunia, hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ili kuendana na mabadiliko hayo.

Maandalizi hayo yanaonekana kwenye uwekezaji unaofanywa kwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika. Kwa sasa kuna miradi mikubwa ya nishati inayoungwa mkono na China inayoendelea kujengwa kote barani Afrika. Nchini Mali kuna maeneo makubwa ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua, nchini Zambia kuna mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme kwa maji Zambia, na katika nchi za Afrika kuna miradi kadhaa ya umeme unaozalishwa kwa gesi, jua, maji na joto la ardhini. Miradi hii yote kwa ujumla, inachangia juhudi za dunia za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa, lakini pia inapunguza gharama za nishati zinazotokana na uagizaji wa mafuta.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya watu milioni 600 barani Afrika — katika eneo la kusini mwa Sahara—wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme. Hata katika maeneo yenye umeme, umeme si wa uhakika na watu wengi maskini wanashindwa kumudu gharama za umeme. China imekuwa ni mshirika muhimu katika kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto hiyo.

Katika ushirikiano wa nishati kati ya China na Afrika, miradi ya nishati mbadala ndio inayotawala. Umeme unaozalishwa kwa maji na jua ndio unaongoza, ukifuatiwa na gesi, upepo, makaa ya mawe, jotoardhi, biomasi, na nishati ya mawimbi. Utofauti huu unaangazia msisitizo wa kimkakati wa China kwenye uendelevu na mahitaji ya ndani ya nchi za Afrika.

Ikilinganishwa na uwekezaji uliofanywa na nchi za magharibi, uwekezaji unaofanywa na China unazidi kuonyesha ufanisi kupitia miundo rahisi ya ufadhili, ikiwa ni pamoja na mifumo mseto inayochanganya mtaji wa China na kimataifa. Makampuni ya China pia yanafanya kazi ya ujenzi na usambazaji wa vifaa, kuendana na mazingira ya nchi tofauti.

Hata hivyo licha ya maendeleo makubwa, miradi kadhaa inakabiliwa na ucheleweshaji au kusimama kutokana na changamoto za kiufundi, kifedha, au kisiasa. Vizuizi hivi vinaonesha a ugumu wa maendeleo makubwa ya miundombinu ya nishati barani Afrika. Hata hivyo kupitia mifumo mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika, utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea hatua kwa hatua.
 
Back
Top Bottom