wanaharakati wa jenda ni kakundi kadogo ka wanawake kanakowadanganya wenzao walio wengi. Mimi na dada zangu tumezaliwa, tumelelewa, tumesomeshwa wote na kupendana kabisa, sijamsikia baba akisema wewe mwajuma usioge ili kaka yako aoge kwanza, sijasikia akisema wewe halima usiende shule ili kaka yako ada itoshe. NilikuWA nachunga mifugo ya familia yote, walikuwa wanapika chakula cha familia yote kuna ubaya gani hapo mimi kuchunga na yeye kupika? Ghafla ninamsikia mjinga anasema wewe halima utapata hiki na kile kwakuwa ni mwanamke, utakopeshwa, utawezeshwa, nk lakini mimi sipati. Najiuliza hivi hawa wanafanya kitu gani? kwanini wanafanya mambo ya jumlajumla namna hii? Kama kuna jamii inawakataza wanawake wao wasiende shule ni bora wa kahangaika na hilo kabila tu badala ya kusema wanawake wote, wanaume woote, nk. Mbona akina mama Mongela na wengine wamesoma na wako vizuri? nani anaweza kumyanyasa, kumuonea, kumdhulumu mama mongela? Wanawake amkeni hamuhitaji kuwezeshwa na mtu yeyote yule, wanaosema hivyo ni waganga njaa na makuwadi wa ushoga.